The chat will start when you send the first message.
1Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
2Bwana anayapenda malango ya Sayuni
kuliko makao yote ya Yakobo.
3Mambo matukufu yanasemwa juu yako,
ee mji wa Mungu:
4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli[#87:4 jina la ushairi la Misri]
miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:
Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,
nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”
5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,
“Huyu na yule walizaliwa humo,
naye Aliye Juu Sana mwenyewe
atamwimarisha.”
6Bwana ataandika katika orodha ya mataifa:
“Huyu alizaliwa Sayuni.”
7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,
“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”