The chat will start when you send the first message.
1Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.
2Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha wengine vile vile.
3Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.[#2 Tim 1:8; 4:5]
4Askari aliye vitani hajiingizi katika shughuli za dunia, maana lengo lake ni kumpendeza yeye aliyemweka kuwa askari.
5Hata mwanariadha hapewi taji, asiposhindana kwa kufuata sheria.[#2 Tim 4:8]
6Yampasa mkulima mwenye bidii ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la mavuno.[#1 Kor 9:7,10]
7Yatafakari sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa ufahamu katika mambo yote.
8Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo Injili yangu.[#Rum 1:3; 2:16; 1 Kor 15:4,20; 2 Sam 7:12]
9Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi.[#Efe 3:1,13; Flp 1:12-14; 2:17]
10Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.[#Kol 1:24]
11Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana,[#2 Kor 4:11]
Kama tukifa pamoja naye,
tutaishi pamoja naye pia;
12Kama tukistahimili,[#Mt 10:33; Lk 12:9]
tutamiliki pamoja naye;
Kama tukimkana yeye,
yeye naye atatukana sisi;
13Kama sisi hatuamini,[#Rum 3:2,3; Hes 23:19]
yeye hudumu wa kuaminiwa.
Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
14Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wanaoyasikia.[#1 Tim 6:4; Tit 3:9]
15Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtendakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.[#1 Tim 4:6; Lk 12:42; Tit 2:7,8]
16Jiepushe na maneno machafu yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,[#1 Tim 4:7]
17na neno lao litaenea kama donda ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,[#1 Tim 1:20]
18waliopotoka kutoka kwenye kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha tokea, hata kuipindua imani ya watu kadhaa.
19Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye mhuri huu,[#Hes 16:5,26; Yn 10:14; Isa 26:13; 28:16,17]
Bwana awajua walio wake.
Na tena,
Kila aliitaye jina la Bwana na auache uovu.
20Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.[#1 Kor 3:12]
21Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.[#2 Tim 3:17]
22Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.[#1 Tim 6:11; 1:5]
23Lakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo ya elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.[#1 Tim 4:7]
24Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;[#Tit 1:7]
25akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awajalie ili watubu na kuijua kweli;[#1 Tim 2:4]
26wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambaye amewanasa, hata wakayafanya mapenzi yake.