The chat will start when you send the first message.
1Pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu;
2na iwe, ikimpasa kupigwa yule mwovu, alazwe chini na mwamuzi, na kupigwa mbele ya uso wake, kwa kadiri ya uovu wake, kwa kuhesabu.[#Lk 12:48; Mit 19:29; Mt 10:17]
3Aweza kumpiga fimbo arobaini asizidishe asije akaonekana nduguyo kuwa amedharauliwa kwako, azidishapo kwa kumpiga fimbo nyingi juu ya hizi.[#2 Kor 11:24; Ayu 18:3]
4Ng'ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa.[#1 Kor 9:9; 1 Tim 5:18; Mit 12:10]
5Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe.[#Mt 22:24; Mk 12:19; Lk 20:28; Mwa 38:8; Rut 1:12]
6Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli.[#Mwa 38:9]
7Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu.[#Rut 4:7-8]
8Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu,
9ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi.[#Rut 4:7; Isa 20:2]
10Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu.[#Mit 6:33; 1 Tim 3:7]
11Wapiganapo wanaume wao kwa wao, akakaribia mke wa mmojawapo, ili kumwokoa mumewe katika mkono wa ampigaye, yule mke akatoa mkono wake, na kumkamata tupu yake;
12umkate ule mkono wake, lisiwe na huruma jicho lako.[#Kum 19:13]
13Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako.[#Law 19:35-36; Mit 11:1; 20:23; Eze 45:10; Amo 8:5; Mik 6:11]
14Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako.
15Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.[#Kut 20:12]
16Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.[#Mit 11:1; 20:23; Amo 8:5-7; 1 Kor 8:9-11; 1 The 4:6; Ufu 21:27]
17Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri;[#Kut 17:8-14; 1 Sam 15:2-9]
18jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu.[#Neh 5:9,15; Zab 36:1; Mit 16:6; Rum 3:18]
19Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha BWANA, Mungu wako, katika adui zako wote walio kandokando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.[#1 Sam 15:3]