The chat will start when you send the first message.
1Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.[#Isa 11:14; Yer 9:26; Hes 21:28; Isa 25:10-12; Yer 48:1-47; Eze 25:8-11; Amo 2:1-3; Sef 2:8-11]
2Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.
3Wanajivika nguo za magunia katika njia kuu zao; juu ya madari yao, na katika mitaa yao, kila mtu analia, anamwaga machozi.
4Heshboni analia na Eleale; mpaka Yahasa sauti ya kulia kwao inasikiwa; hata watu wa Moabu waliovaa silaha wanapiga kelele sana kwa sababu hiyo; nafsi yake inatetemeka ndani yake.[#Hes 32:3]
5Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.[#Yer 48:5]
6Kwa maana maji ya Nimrimu yamekuwa mahali palipoharibika, kwa kuwa majani yamekauka, miche imenyauka, majani mabichi yamekoma.
7Kwa hiyo vitu walivyojipatia tele, na akiba yao, wanavichukua hadi kijito cha Mierezi.
8Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu.
9Maana maji ya Dimoni yamejaa damu; maana ninatayarisha msiba mpya juu ya Dimoni, simba juu ya watu wa Moabu waliokimbia, na juu ya mabaki yao.