The chat will start when you send the first message.
1Roho yangu imezimia, siku zangu zimekoma,[#Zab 88:3,4]
Kaburi li tayari kunipokea.
2Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka,[#1 Sam 1:6]
Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao.
3Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe;[#Mit 6:1]
Kuna nani atakayeniwekea dhamana?
4Kwa kuwa umezifumba akili zao ufahamu;
Kwa hiyo hutawaacha wanishinde.
5Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo,
Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi.
6Amenifanya niwe mithali kwa watu;[#1 Fal 9:7]
Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.
7Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi,
Na viungo vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.
8Wanyofu watayastaajabia hayo,
Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu.
9Lakini mwenye haki ataishika njia yake,[#Mit 4:18; Zab 24:4]
Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.
10Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa;[#Ayu 6:29]
Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu.
11Siku zangu zimepita, makusudi yangu yamevunjika,[#Ayu 7:6; Isa 38:10]
Hata hayo niliyo nayo moyoni mwangu.
12Wabadili usiku kuwa mchana;
Wasema, Mwanga u karibu kwa sababu ya giza.
13Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu;
Nikitandika malazi yangu gizani;
14Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu;
Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na dada yangu;
15Basi, tumaini langu liko wapi?
Na tumaini langu, ni nani atakayeliona?
16Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu,[#2 Kor 1:9; Zab 88:4-8; Ayu 3:17]
Itakapokuwapo raha mavumbini.