The chat will start when you send the first message.
1Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2Hata leo malalamiko yangu yana uchungu;
Pigo langu ni zito zaidi ya kuugua kwangu.
3Laiti ningejua mahali niwezapo kumwona,
Nifike hata hapo anapokaa!
4Ningeiweka kesi yangu mbele yake,
Na kukijaza kinywa changu hoja.
5Ningeyajua maneno atakayonijibu,
Na kuelewa hayo atakayoniambia.
6Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake?[#Ayu 9:19; Isa 27:4]
La, lakini angenisikiliza.
7Hapo wanyofu wangepata kuhojiana naye;
Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.
8Tazama, naenda mbele, wala hayuko;[#Zab 10:1; 1 Tim 6:16]
Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;
9Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona;
Hujificha upande wa kulia, hata nisimwone.
10Lakini yeye aijua njia niendeayo;[#Zab 17:3; Yak 1:12]
Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
11Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake;[#Zab 44:18]
Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.
12Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake;
Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,
13Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza?[#Ayu 34:29; Mhu 3:14; Rum 9:19; Yak 1:17]
Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.
14Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamriwa;[#1 The 3:3]
Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye.
15Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake;[#Zab 119:120]
Nitakapofikiri, namwogopa.
16Kwa maana Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia,
Naye Mwenyezi amenitaabisha;
17Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza,[#Ayu 6:9]
Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.