Zaburi 133

Zaburi 133

Baraka za kuwa na umoja

1Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza,[#Mwa 13:8; 1 Kor 1:10]

Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.

2Ni kama mafuta mazuri kichwani,[#Kut 30:25]

Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni,

Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.

3Ni kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni.[#Kum 4:48; 28:8; Law 25:11; Dan 12:2,3; Mt 25:34,46; Yn 4:14; 17:3; Ebr 7:25; 1 Yoh 5:20]

Maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka,

Naam, uzima hata milele.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 
Published by: Bible Society of Tanzania