1 Mambo 2

1 Mambo 2

Wana wa Yakobo na wa Yuda.

(Taz. 1 Mambo 4.)

1Wana wa Isiraeli ndio hawa: Rubeni, Simeoni, Lawi na Yuda, Isakari na Zebuluni,[#1 Mose 35:22-26.]

2Dani, Yosefu na Benyamini, Nafutali, Gadi na Aseri.

3Wana wa Yuda: Eri na Onani na Sela; hawa watatu alizaliwa na Mkanaani binti Sua. Naye Eri, mwanawe wa kwanza wa Yuda, akawa mbaya machoni pa Bwana, kwa hiyo akamwua.[#1 Mose 38:1-7.]

4Naye mkwewe Tamari akamzalia Peresi na Zera. Hivyo wana wote wa Yuda walikuwa watano.[#1 Mose 38:29-30.]

5Wana wa Peresi ni Hesironi na Hamuli.[#1 Mose 46:12.]

6Nao wana wa Zera ni Zimuri na Etani na Hemani na Kalkoli na Dara, wao wote ni watano.

7Nao wana wa Karmi ni Akari aliyewaponza Waisiraeli kwa kuuvunja mwiko wa kuchukua mali.[#Yos. 7.]

8Nao wana wa Etani ni Azaria.

9Nao wana wa Hesironi, aliozaliwa, ni Yerameli na Ramu na Kelubai.[#1 Mambo 2:18,42; Ruti 4:19-22; Mat. 1:3.]

10Naye Ramu akamzaa Aminadabu, naye Aminadabu akamzaa Nasoni aliyekuwa mkuu wa wana wa Yuda.

11Naye Nasoni akamzaa Salma, naye Salma akamzaa Boazi,

12naye Boazi akamzaa Obedi, naye Obedi akamzaa Isai,

13naye Isai akamzaa mwanawe wa kwanza Eliabu na wa pili Abinadabu na wa tatu Simea,[#1 Sam. 16:6-10.]

14wa nne Netaneli, wa tano Radai,[#1 Sam. 17:12.]

15wa sita Osemu, wa saba Dawidi.

16Nao maumbu zao ni Seruya na Abigaili. Nao wana wa Seruya ni Abisai na Yoabu na Asa-Eli, hawa watatu.[#2 Sam. 2:18.]

17Naye Abigaili akamzaa Amasa, naye babake Amasa ni Mwisimaeli Yeteri.[#2 Sam. 17:25.]

18Naye Kalebu, mwana wa Hesironi, akazaa wana naye mkewe Azuba naye Yerioti; nao wanawe huyo ni hawa: Yeseri na Sobabu na Ardoni.[#1 Mambo 2:9,42.]

19Azuba alipokufa, Kalebu akamchukua Efurati, naye akamzalia Huri.[#1 Mambo 2:50.]

20Naye Huri akamzaa Uri, naye Uri akamzaa Besaleli.[#2 Mose 31:2.]

21Halafu Hesironi akaingia kwa binti Makiri, babake Gileadi; naye akamchukua alipokuwa mwenye miaka 60, akamzalia Segubu.

22Naye Segubu akamzaa Yairi; huyu Yairi akawa mwenye miji 23 katika nchi ya Gileadi.[#Amu. 10:3.]

23Lakini Wagesuri na Washami wakavichukua vijiji vya Yairi kwao, Kenati na vijiji vyake, vyote pamoja ni miji 60. Hawa wote ni wana wa Makiri, babake Gileadi.[#1 Fal. 4:13.]

24Hesironi alipokwisha kufa mle Kalebu-Efurata, ndipo, Abia, mkewe Hesironi, alipomzalia Ashuri, babake Tekoa.[#1 Mambo 4:5.]

25Wana wa Yerameli, mwanawe wa kwanza wa Hesironi, walikuwa: wa kwanza Ramu, tena Buna na Oreni na Osemu wa Ahia.[#1 Mambo 2:9.]

26Yerameli akawa na mke mwingine, jina lake Atara, naye ni mamake Onamu.

27Nao wana wa Ramu, mwanawe wa kwanza wa Yerameli, walikuwa: Masi na Yamini na Ekeri.

28Nao wana wa Onamu walikuwa Samai na Yada; nao wana wa Samai ni Nadabu na Abisuri.

29Nalo jina la mkewe Abisuri ni Abihaili, naye akamzalia Abani na Molidi.

30Nao wana wa Nadabu ni Seledi na Apaimu; naye Seledi alipokufa hakuwa na wana.

31Nao wana wa Apaimu: Isi; nao wana wa Isi: Sesani; nao wana wa Sesani: Alai.

32Nao wana wa Yada, nduguye Samai: Yeteri na Yonatani; naye Yeteri alipokufa hakuwa na wana.

33Nao wana wa Yonatani: Peleti na Zaza. Hawa walikuwa wana wa Yerameli.

34Sesani hakuwa na wana wa kiume, ila wa kike tu. Naye Sesani alikuwa na mtumwa wa Misri, jina lake Yariha.

35Sesani akamwoza huyo mtumwa wake Yariha mwanawe wa kike, akamzalia Atai.

36Naye Atai akamzaa Natani, naye Natani akamzaa Zabadi.

37Naye Zabadi akamzaa Efulali, naye Efulali akamzaa Obedi.

38Naye Obedi akamzaa Yehu, naye Yehu akamzaa Azaria.

39Naye Azaria akamzaa Helesi, naye Helesi akamzaa Elasa.

40Naye Elasa akamzaa Sisimai, naye Sisimai akamzaa salumu.

41Naye Salumu akamzaa Yekamia, naye Yekamia akamzaa Elisama.

42Nao wana wa Kalebu, nduguye Yarameli: Mwanawe wa kwanza Mesa aliye babake Zifu, tena wana wa Maresa aliye babake Heburoni.[#1 Mambo 2:18.]

43Nao wana wa Heburoni: Kora na Tapua na Rekemu na Sema.

44Naye Sema akamzaa Rahamu, babake Yorkamu. Naye Rekemu akamzaa Samai.

45Naye mwana wa Samai ni Maoni; naye Maoni ni babake Beti-Suri.

46Naye Efa, suria ya Kalebu, akamzaa Harani na Mosa na Gazezi; naye Harani akamzaa Gazezi.

47Nao wana wa Yadai: Regemu na Yotamu na Gesani na Peleti na Efa na safu.

48Maka, Suria ya Kalebu, akamzaa Seberi na Tirihana.

49Tena akamzaa Safu, babake Madimana, na Sewa, babake Makibena, na babake Gibea; naye Akisa ni mwana wa kike wa Kalebu.[#Yos. 15:16; Amu. 1:12.]

50Hawa walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri aliyekuwa mwana wa kwanza wa Efurata ni Sobali, babake Kiriati-Yearimu,[#1 Mambo 2:19.]

51na Salma, babake Beti-Lehemu, na Harefu, babake Beti-Gaderi.

52Nao wana wa sobali, babake Kiriati-Yearimu, walikuwa Haroe, ndio nusu yao wa Menuhoti.

53Nazo koo za Kiriati-Yearimu ndio Waitiri na Waputi na Wasumati na Wamisirai; kwao hao ndiko, walikotoka Wasorati na Waestauli.[#1 Mambo 4:2.]

54Wana wa Salma: Beti-Lehemu na Wanetofati, Atiroti, Beti-Yoabu nayo nusu yao Wamanahati, ndio wasori;[#1 Mambo 9:16.]

55nazo koo za waandishi waliokaa Yabesi ndio Watirati, Wasimati, Wasukati. Hawa ndio Wakini waliotoka kwa Hamati, baba yao mlango wa Rekabu.[#Amu. 1:16; Yer. 35.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania