1 Mambo 25

1 Mambo 25

Mafungu 24 ya waimbaji.

1Kisha Dawidi na wakuu wa vikosi wakawatenga kwao wana wa Asafu na kwao wa Hemani na kwao wa Yedutuni wao waliolifumbua Neno kwa kupiga mazeze na mapango na matoazi, waje kutumika hivyo. Hesabu yao walioitumikia kazi hiyo ni hii:[#1 Mambo 15:19.]

2kwa wana wa Asafu walikuwa Zakuri na Yosefu na Netania na Asarela; hawa wana wa Asafu waliongozwa na Asafu aliyelifumbua Neno kwa kuongozwa na mfalme.

3Kwa Yedutuni walikuwa wana wa Yedutuni: Gedalia na Seri na Yesaya, Hasabia na Matitia (na Simei), watu sita; hawa waliongozwa kupiga mazeze na baba yao Yedutuni aliyelifumbua Neno kwa kumshukuru na kumtukuza Bwana.

4Kwa Hemani walikuwa wana wa Hemani: Bukia, Matania, Uzieli, Sebueli na Yerimoti, tena Hanania, Hanani, Eliata, Gidalti na Romamuti-Ezeri, tena Yosibekasa, Maloti, Hotiri, Mahazioti.

5Hawa wote walikuwa wana wa Hemani aliyekuwa mchunguzaji wa mfalme; kwa hivyo, Mungu alivyomwambia, ya kuwa ataitukuza pembe yake, Mungu alikuwa amempa wana kumi na wanne wa kiume na watatu wa kike.[#1 Mambo 21:9; 2 Mambo 35:15.]

6Hawa wote waliongozwa na baba zao kuimba nyumbani mwa Bwana na kupiga matoazi na mapango na mazeze, wakatumika hivyo nyumbani mwa Mungu kwa hivyo, mfalme alivyowaongoza akina Asafu na Yedutuni na Hemani.

7Walipohesabiwa pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia Bwana, wote walioijua kazi hii walikuwa 288.

8Wakazipigia zamu zao kura, mdogo sawasawa kama mkubwa, naye mfunzi sawasawa kama mwanafunzi.[#1 Mambo 24:31.]

9Hapo kura ya kwanza ya Asafu ikamwangukia Yosefu; ya 2 ikamwangukia Gedalia na ndugu zake na wana wake, pamoja watu 12.

10Ya 3 Zakuri na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

11Ya 4 Isiri na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

12Ya 5 Netania na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

13Ya 6 Bukia na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

14Ya 7 Yesarela na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

15Ya 8 Yesaya na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

16Ya 9 Matania na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

17Ya 10 Simei na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

18Ya 11 Azareli na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

19Ya 12 Hasabia na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

20Ya 13 Subaeli na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

21Ya 14 Matitia na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

22Ya 15 Yeremoti na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

23Ya 16 Hanania na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

24Ya 17 Yosibekasa na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

25Ya 18 Hanani na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

26Ya 19 Maloti na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

27Ya 20 Eliata na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

28Ya 21 Hotiri na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

29Ya 22 Gidalti na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

30Ya 23 Mahazioti na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

31Ya 24 Romamuti-Ezeri na wana wake na ndugu zake, pamoja watu 12.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania