The chat will start when you send the first message.
1Hii ndiyo hesabu yao wana wa Isiraeli wakuu wa milango na wakuu wa maelfu na wa mamia nao wenye amri waliomtumikia mfalme katika mambo yote yayapasayo hayo mafungu, wakiingia, tena wakitoka mwezi kwa mwezi miezi yote ya mwaka, nalo fungu moja lilikuwa watu 24000.
(2-15: 1 Mambo 11:11-31.)2Mkuu wa fungu la kwanza la mwezi wa kwanza alikuwa Yasobamu, mwana wa zabudieli; nalo fungu lake lilikuwa lenye watu 24000.
3Alikuwa mmoja wao wana wa Peresi, akawa kichwa chao wakuu wote wa vikosi vya mwezi wa kwanza.
4Naye mkuu wa fungu la mwezi wa pili alikuwa Mwahohi Dodai, naye mkubwa wa fungu lake alikuwa Mikloti; hata fungu lake lilikuwa lenye watu 24000.
5Mkuu wa kikosi cha tatu cha mwezi wa tatu alikuwa Benaya, mwana wa mtambikaji Yoyada, yeye alikuwa kichwa, nalo fungu lake lilikuwa lenye watu 24000.
6Huyu Benaya alikuwa fundi wa vita kwao wale thelathini, naye alikuwa mkuu wao wale thelathini. Aliyeliongoza fungu lake alikuwa mwanawe Amizabadi.
7Mkuu wa nne wa mwezi wa nne alikuwa Asaheli, ndugu yake Yoabu, naye mwanawe Zebadia alimfuata. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
8Mkuu wa tano wa mwezi wa tano alikuwa mkuu Mwizirahi Samuhuti, fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
9Mkuu wa sita wa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikesi wa Tekoa, fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
10Mkuu wa saba wa mwezi wa saba alikuwa Mpuloni Helesi aliyekuwa mmoja wao wana wa Efuraimu. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
11Mkuu wa nane wa mwezi wa nane alikuwa Sibekai wa Husa aliyekuwa mmoja wao Wazera. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.[#1 Mambo 20:4.]
12Mkuu wa tisa wa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri wa Anatoti aliyekuwa mmoja wao Wabenyamini. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
13Mkuu wa kumi wa mwezi wa kumi alikuwa Maharai wa Netofa aliyekuwa mmoja wao Wazera. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
14Mkuu wa kumi na moja wa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya wa Piratoni aliyekuwa mmoja wao wana wa Efuraimu. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
15Mkuu wa kumi na mbili wa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai wa Netofa aliyekuwa wa mlango wa Otinieli. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
16Wakuu wa mashina ya Isiraeli walikuwa hawa: kwa Warubeni alikuwa mkubwa Eliezeri, mwana wa zikiri; kwa Wasimeoni Sefatia, mwana wa Maka;
17kwa Lawi Hasabia, mwana wa Kemueli; kwa Haroni Sadoki;
18kwa Yuda Elihu aliyekuwa mmoja wao ndugu zake Dawidi; kwa Isakari Omuri, mwana wa Mikaeli;
19kwa Zebuluni Isimaya, mwana wa Obadia; kwa Nafutali Yerimoti, mwana wa Azirieli;
20kwa wana wa Efuraimu Hosea, mwana wa Azazia; kwa nusu ya shina la Manase Yoeli, mwana wa Pedaya;
21kwa nusu ya Manase kule Gileadi Ido, mwana wa Zakaria, tena kwa Benyamini Yasieli, mwana wa Abineri;
22kwa Dani Azareli, mwana wa Yerohamu. Hawa walikuwa wakuu wa mashina ya Isiraeli.
23Lakini wao waliokuwa wa miaka ishirini nao wasioipata bado Dawidi hakuwahesabu, kwani Bwana alisema, ya kuwa atawaongeza Waisiraeli, wawe wengi kama nyota za mbinguni.[#1 Mose 22:17.]
24Yoabu, mwana wa Seruya, alianza kuwahesabu, lakini hakumaliza, maana kwa ajili hii mapatilizo makali yaliwapata Waisiraeli. Kwa hiyo hesabu hiyo haikutiwa katika hesabu ya Mambo ya siku za mfalme Dawidi.[#1 Mambo 21:14.]
25Mtunza vilimbiko vya mfalme alikuwa Azimaweti, mwana wa Adieli; naye mtunza vilimbiko vilivyokuwa mashambani na mijini na mizabibuni na ngomeni alikuwa Yonatani, mwana wa Uzia.
26Msimamizi wa wafanya kazi za kulima mashambani alikuwa Eziri, mwana wa Kelubu.
27Msimamizi wa mizabibu alikuwa Simei wa Rama, naye mtunza mvinyo zilizolimbikwa mizabibuni alikuwa Msifumi Zabudi.
28Msimamizi wa michekele na wa mikuyu iliyokuwako katika nchi ya tambarare alikuwa Baali-Hanani wa Gaderi, naye mtunza mafuta yaliyolimbikwa alikuwa Yoasi.
29Msimamizi wa ng'ombe waliolisha Saroni alikuwa Sitirai wa Saroni, naye msimamizi wa ng'ombe walioko mabondeni alikuwa Safati, mwana wa Adilai.
30Msimamizi wa ngamia alikuwa Mwisimaeli Obili, naye msimamizi wa punda wake alikuwa Yehedia wa Meronoti.
31Msimamizi wa mbuzi na kondoo alikuwa Mhagri Yazizi. Hawa wote walikuwa watunza mali za mfalme Dawidi.
32Yonatani, mjomba wake Dawidi, alikuwa mwenye kula njama na mfalme, naye alikuwa mwenye utambuzi na mjuzi wa vitabu. Naye Yehieli, mwana wa Hakemoni, alikuwa mkuza wana wa mfalme.
33Naye Ahitofeli alikuwa mwenye kula njama na mfalme, naye Mwarki Husai alikuwa rafiki yake mfalme.[#2 Sam. 15:12,37.]
34Waliomfuata Ahitofeli walikuwa Yoyada, mwana wa Benaya, na Abiatari. Mkuu wa vikosi vya mfalme alikuwa Yoabu.[#2 Sam. 8:16.]