The chat will start when you send the first message.
1Mfalme Dawidi akauambia ule mkutano wote: Mwanangu Salomo, huyu mmoja, Mungu aliyemchagua, ujana wake ungali mchanga bado, nayo kazi hii ni kubwa, kwani si mtu anayejengewa jumba hili tukufu, ila ni Bwana Mungu.[#1 Mambo 22:5.]
2Kwa nguvu zangu zote nimeitengenezea nyumba ya Mungu wangu dhahabu za vyombo vya dhahabu na fedha za vyombo vya fedha na shaba za vyombo vya shaba na vyuma vya vyombo vya chuma na miti ya mijengo, tena vito vya Sardio na vito vyenye dhahabu ukingoni na vito vyeusi na vito vya rangi nyinginenyingine na vito vya kila namna vyenye kima na mawe mengi meupe.
3Tena kwa kupendezwa na nyumba ya Mungu wangu, dhahabu na fedha zilizo mali zangu nimeitolea nyumba ya Mungu wangu, niziongeze hizo zote, nilizoitengenezea nyumba hiyo takatifu.
4Vipande vya dhahabu 3000 vya dhahabu ya Ofiri, ndio frasila 9000, na vipande vya fedha zilizong'azwa 7000, ndio frasila 21000 za kuzifunikiza kuta za nyumba.
5napo panapopaswa na dhahabu papate dhahabu, napo panapopaswa na fedha papate fedha, napo, mafundi watakapozitumia za kazi zo zote. Sasa hivi kwenu yuko nani anayetaka kukijaza mwenyewe kiganja chake, apate kumpa Bwana?[#2 Mose 35:5.]
6Ndipo, wakuu wa milango wa wakuu wa mashina ya Waisiraeli na wakuu wa maelfu na wa mamia nao wakuu wa kazi za mfalme walipochanga kwa kupendezwa,
7wakatoa vya kutumiwa nyumbani mwa Mungu vipande vya dhahabu 5000, ndio frasila 15000, na robo za dhahabu 10000, ndio shilingi kama 400000, na vipande vya fedha 10000 kumi, ndio frasila 30000, na vipande vya shaba 18000, ndio frasila 54000, na vipande vya chuma 100000 ndio frasila 300000.
8Nao walioonekana kuwa wenye vito wakavitia katika vilimbiko vya nyumba ya Bwana mkononi mwa Mgersoni Yehieli.[#2 Mose 35:27.]
9Watu wakavifurahia hivyo, walivyovitoa kwa kupenda wenyewe, kwani kila alimtolea Bwana kwa kupenda kwa moyo wote mzima, naye mfalme Dawidi alifurahi na kuona furaha kubwa.
10Ndipo, Dawidi alipomtukuza Bwana mbele ya mkutano wote, yeye Dawidi akisema: Utukuzwe wewe Bwana Mungu wa baba yetu Isiraeli toka kale hata kale!
11Wewe Bwana ndiwe mwenye ukuu na uwezo na utukufu na ung'avu na urembo, kwani yote yaliyomo mbinguni na nchini ni yako, Bwana, ndiwe mfalme wao na kichwa chao yote kwa kuwa huko juu.[#Ufu. 4:11; 5:13.]
12Mali na macheo hutoka kwako, wewe unayatawala yote pia, mkononi mwako zimo nguvu na uwezo, nao mkono wako ndio unaowapatia wote ukubwa na nguvu.[#2 Mambo 20:6.]
13Sasa Mungu wetu, sisi tunakushukuru na kulishangilia Jina lako tukufu.
14Kwani mimi ni mtu gani wao watu wangu ni watu gani, tukijipatia nguvu za kutoa mali kama hizi kwa kupenda wenyewe? Haya yote yametoka kwako, tumeyatoa mkononi mwako, tukakupa tena.
15Kwani sisi tu wageni mbele yako wanaojikalia tu, kama baba zetu wote, siku zetu za kuwapo huku nchini ni kama kivuli tu kisicho na kingojeo cha kukaa.[#Sh. 39:13; Ebr. 11:13; Iy. 14:2.]
16Bwana Mungu wetu, wingi huu wote wa mijengo yo yote, tuliyoitengeneza ya kulijengea Jina lako takatifu nyumba, umetoka mkononi mwako, kwa maana yote pia ni yako wewe.
17Ninajua, Bwana, ya kuwa unaijaribu mioyo, ukapendezwa nao wanyokao. Mimi nami kwa hivyo, moyo wangu unavyonyoka, nimeyatoa haya yote kwa kupenda mwenyewe; sasa nao hawa walio ukoo wako waliopo hapa nimewaona na kuwafurahia, ya kuwa wamekutolea mali zao kwa kupenda wenyewe.[#1 Mambo 28:9.]
18Bwana Mungu wa baba zetu Aburahamu na Isaka na Isiraeli, yaangalie mambo haya kale na kale kuwa mawazo, walio ukoo wako watakayoyatunga mioyoni mwao, kaishupaze mioyo yao, ikuelekee wewe!
19Naye mwanangu Salomo mpe moyo usiogawanyika, ayaangalie maagizo yako na mashuhuda yako na maongozi yako, ayafanye yote, alijenge hilo jumba, nililolitengenezea mijengo!
20Dawidi akauambia huo mkutano wote: Mtukuzeni Bwana Mungu wenu! Ndipo, watu wote wa mkutano walipomtukuza Bwana Mungu wa baba zao na kujiinamisha na kumwangukia Bwana na mfalme.
21Wakamtolea Bwana ng'ombe za tambiko; kesho yake siku hiyo wakamteketezea Bwana madume ya ng'ombe elfu na madume ya kondoo elfu na wana kondoo elfu pamoja na kumtolea vinywaji vya tambiko na ng'ombe nyingi nyingine za tambiko kwa ajili ya Waisiraeli wote.
22Wakala, wakanywa mbele ya Bwana siku hiyo na kufurahi sana. Kisha wakamchukua Salomo, mwana wa Dawidi, mara ya pili, awe mfalme wao, wakampaka mafuta, awe mkuu aliye mtu wa Bwana, naye Sadoki wakampaka mafuta, awe mtambikaji.[#1 Mambo 23:1.]
23Ndipo, Salomo alipokaa katika kiti cha kifalme cha Bwana, akawa mflame mahali pa baba yake Dawidi, akafanikiwa, nao Waisiraeli wote wakamtii.[#1 Mambo 28:5; 1 Fal. 1:35,39.]
24Hata wakuu wote na mafundi wa vita nao wana wote wa mfalme Dawidi wakajiweka mkononi mwa Salomo, wamtii.
25Bwana akampatia Salomo ukuu uliozidi machoni pao Waisiraeli wote, akampa hata urembo wa kifalme kuupita wote, walioupata wengine waliokuwa mbele yake wafalme wa Waisiraeli.[#2 Mambo 1:1.]
26Dawidi, mwana wa Isai, alikuwa mfalme wa Waisiraeli wote.
27Nazo siku, alizokuwa mfalme wao Waisiraeli, zilikuwa miaka 40; Heburoni alikaa mwenye ufalme miaka 7, namo Yerusalemu alikaa mwenye ufalme miaka 33.[#1 Fal. 2:11.]
28Akafa mwenye miaka mingi alipokuwa ameshiba siku na mali na macheo, naye mwanawe Salomo akawa mfalme mahali pake.
29Nayo mambo ya mfalme Dawidi, ya kwanza na ya mwisho tunayaona, yameandikwa penye mambo ya mtazamaji Samweli na penye mambo ya mfumbuaji Natani na penye mambo ya mchunguzaji Gadi;[#1 Mambo 21:9.]
30ndimo, yalimo mambo yote ya ufalme wake na ya uwezo wake nazo siku zilizompata yeye na Waisiraeli na nchi zote za kifalme.