The chat will start when you send the first message.
1Benyamini akamzaa mwanawe wa kwanza Bela, wa pili Asibeli, wa tatu Ahara,[#1 Mose 46:21.]
2wa nne Noha, wa tano Rafa.
3Wanawe Bela walikuwa: Adari na Gera na Abihudi
4na Abisua na Namani na Ahoa
5na Gera na Sefufani na Huramu.
6Nao hawa ndio wana wa Ehudi; ndio waliokuwa vichwa vya milango ya baba zao waliokaa Geba, waliowahamisha kwenda Manahati:
7Namani na Ahia na Gera; huyu ndiye aliyewahamisha. Kisha akamzaa Uza na Ahihudi.
8Saharaimu alizaa katika mashamba ya Wamoabu alipokwisha kuwatuma wakeze Husimu na Baara kwenda zao;
9kisha akazaa na mkewe Hodesi: Yobabu na Sibia na Mesa na Malkamu
10na Yeusi na Sakia na Mirma. Hawa ndio wanawe waliokuwa vichwa vya milango ya baba zao.
11Pamoja na Husimu alikuwa amemzaa Abitubu na Elpali.
12Nao wana wa Elpali: Eberi na Misamu na Semeri; huyu ndiye aliyejenga Ono na Lodi na vijiji vyake.
13Naye Beria na Sema ndio waliokuwa vichwa vya milango ya baba zao iliyokaa Ayaloni, walipokwisha kuwafukuza wenyeji wa Gati.
14Nao ndugu zao ni Sasaki na Yeremoti.
15Naye Zebadia na Aradi na Ederi
16na Mikaeli na Isipa na Yoha wlaikuwa wana wa Beria.
17Naye Zebadia na Mesulamu na Hiziki na Heberi
18na Isimerai na Izilia na Yobabu walikuwa wana wa Elpali.
19Naye Yakimu na Zikiri na Zabudi
20na Elienai na Siltai na Elieli
21na Adaya na Beraya na Simurati walikuwa wana wa Simei.
22Naye Isipani na Eberi na Elieli
23na Abudoni na Zikiri na Hanani
24na Hanania na Elamu na Anitotia
25na Ifudia na Penueli walikuwa wana wa Sasaki.
26Naye Samuserai na Seharia na Atalia
27na Yaresia na Elia na Zikiri walikuwa wana wa Yerohamu.
28Hawa ndio vichwa vya milango ya baba zao na wakuu wa vizazi vyao, nao walikaa Yerusalemu.
29Huko Gibeoni alikaa babake Gibeoni, nalo jina la mkewe ni Maka.[#1 Mambo 9:35-44.]
30Naye mwanawe wa kwanza alikuwa Abudoni, tena Suri na Kisi na Baali na Nadabu
31na Gedori na Ayo na Zekeri
32na Mikloti aliyemzaa Simea. Nao hawa walikaa ng'ambo ya ndugu zao kule Yerusalemu kwao ndugu zao.
33Naye Neri akamzaa Kisi, naye Kisi akamzaa Sauli, naye Sauli akamzaa Yonatani, tena Malkisua na Abinadabu na Esibaali.[#1 Sam. 14:51.]
34Naye mwana wa Yonatani alikuwa Meribu-Baali, naye Meribu-Baali akamzaa Mika.
35Nao wana wa Mika ni Pitoni na Meleki na Tarea na Ahazi.
36Ahazi akamzaa Yoada, naye Yoada akamzaa Alemeti, tena Azimaweti na Zimuri, naye Zimuri akamzaa Mosa.
37Naye Mosa akamzaa Bina; mwanawe huyo alikuwa Rafa, mwanawe huyo Elasa, mwanawe huyo Aseli.
38Naye Aseli alikuwa mwenye wana sita, nayo haya ndiyo majina yao: Azirikamu, Bokeru na Isimaeli na Saria na Obadia na Hanani; hawa wote ndio wana wa Aseli.
39Nao wana wa ndugu yake Eseki: wa kwanza Ulamu, wa pili Yeusi, wa tatu Elifeleti.
40Wana wa Ulamu walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu waliojua kuvuta pindi, nao walikuwa wenye wana wa wajukuu wengi, hesabu yao ni 150. Hawa wote walikuwa wana wa wana wa Benyamini.[#1 Mambo 12:2.]