The chat will start when you send the first message.
1*Jivueni uovu wote na udanganyi wote na ujanja na kijicho na mateto yote![#Ef. 4:22.]
2Kwa kuwa m vitoto vichanga vilivyozaliwa siku hizi, yatakeni maziwa ya kweli yasiyodanganya, mkuzwe nayo, mpaka mwufikie wokovu,[#Mat. 18:3; Ebr. 5:12-13.]
3mkiwa mmeonja, mkaona, ya kuwa Bwana ni mwema![#Sh. 34:9.]
4Huyu mjieni! Maana ni jiwe lenye uzima. Kweli watu walilikataa, lakini Mungu amelichagua kuwa lenye heshima.[#Sh. 118:22; Mat. 21:42.]
5Nanyi mlio kama mawe yenye uzima mjengwe kuwa nyumba ya Kiroho, mwe watambikaji watakatifu wa kumtolea Mungu vipaji vya tambiko vya kiroho vimpendezavyo kwa ajili ya Yesu Kristo![#1 Petr. 2:9; Rom. 12:1; Ef. 2:21-22.]
6Kwa hiyo imeandikwa katika Maandiko kwamba:
Tazameni, naweka humu Sioni jiwe la pembeni
lililochaguliwa kuwa lenye heshima,
naye alitegemeaye hatatwezeka.
7Kwa hiyo ninyi mlitegemealo hupata heshima,
lakini wasiolitegemea jiwe hili, waashi walilolikataa,
hilihili huwa kwao jiwe la pembeni
kwamba:
8Ni jiwe la kujigongea
na mwamba wa kujikwalia.
Nao hujigonga, kwa sababu hawalitii Neno; navyo ndivyo, walivyowekewa.
9Lakini ninyi m ukoo uliochaguliwa, m watambikaji wa kifalme, m chama kitakatifu, m watu wakombolewao, mpate kuyatangaza mema yake yeye aliyewaita, mtoke gizani, mwingie mwangani mwake mlimo na mastaajabu.[#2 Mose 19:6; Ufu. 1:6.]
10Kale hamkuwa ukoo mmoja,
lakini sasa mmekuwa ukoo wake Mungu.
Tena kale mlikuwa hamjui kuhurumiwa, lakini sasa mmekwisha kuhurumiwa.*
11*Wapendwa, kwa sababu m wageni wanaopita tu, nawaonya ninyi, mziepuke tamaa za miili zinazozigombanisha roho zenu![#3 Mose 25:23; Sh. 39:13; Yak. 4:1.]
12Fanyeni mwenendo ulio mzuri kwa wamizimu! Hivyo wale wanaowasingizia ninyi kuwa watenda maovu, wanapoziona kazi zenu nzuri, watamtukuza Mungu siku ile, atakapowatokea kuwakagua.[#Mat. 5:16.]
13Kwa ajili ya Bwana utiini ukuu wote uliowekwa na watu: Akiwa mfalme, maana huwapita wote![#Rom. 13:1-7; Tit. 3:1.]
14Wakiwa viongozi, maana hutumwa naye kulipiza watenda maovu na kuwapa sifa watenda mema!
15Nayo ndiyo, Mungu ayatakayo, matendo yenu mema yaunyamazishe upuzi wa watu wajinga.[#1 Petr. 3:16.]
16Kwani mmekwisha kukombolewa, lakini huko kukombolewa, msikugeuze kuwa kifuniko cha kuuficha uovu, ila mjulike kuwa watumwa wake Mungu![#Gal. 5:13; 2 Petr. 2:19.]
17Wote waheshimuni! Wapendeni ndugu! Mwogopeni Mungu! Mheshimuni mfalme![#Fano. 24:21; Mat. 22:21; Rom. 12:10.]
18Ninyi watumishi, watiini mabwana zenu na woga wote! Msiwatii wale tu walio wema na wapole, ila nao walio wakali![#Ef. 6:5; Tit. 2:9.]
19Kwani huko ni kugawiwa chema, mtu ateswaye kwa kupotolewa akiyavumilia hayo masikitiko kwa kuwa wake Mungu.
20Kwani ni chema gani cha kukivumisha, mkiyavumilia mapigo, myapatayo kwa sababu ya kukosa? Lakini mkiyavumilia mateso yawapatayo kwa sababu ya kutenda mema, hiki ndicho chema, Mungu alichowagawia.*[#1 Petr. 3:14,17; 4:13,14; Mat. 5:10.]
21*Maana ndiyo mliyoitiwa. Kwani Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachilia kielezo, mpate kufuata nyayo zake.[#Mat. 16:24.]
22Yeye hakufanya lenye kukosa, uwongo tu haukuonekana kinywani mwake.[#Yes. 59:3; Yoh. 8:46; 2 Kor. 5:21.]
23Alipotukanwa hakutukana naye, alipoteseka hakutisha, ila aliyapeleka kwake yeye anayehukumu kwa kweli.
24Aliyachukua mwenyewe makosa yetu, nao mwili wake ndio ulioyakweza mtini, sisi tupate kuyaepuka makosa na kuukalia wongofu, namo katika mavilio yake ndimo, mlimoponea.[#Yes. 53:4-5; Rom. 6:8,11; 1 Yoh. 3:5.]
25Kwani mlikuwa kama kondoo waliopotea. Lakini sasa mmegeuzwa, mmwelekee mchungaji na mkaguzi wa roho zenu.*[#1 Petr. 5:4; Yes. 53:6; Ez. 34:5; Yoh. 10:12.]