The chat will start when you send the first message.
1Wazee walioko kwenu nawaonya mimi niliye mzee mwenzao na shahidi wa mateso yake Kristo, nitakayekuwa mwenziwe hata katika utukufu utakaofunuliwa.[#Rom. 8:17; 2 Yoh. 1.]
2Nawaonya kwamba: Lichungeni kundi la Mungu lililoko kwenu, si kwa shuruti, ila kwa kuyapenda wenyewe, Mungu ayatakayo, wala si kwa kufuata machumo mabaya, ila kwa mioyo![#Yoh. 21:16; Tume. 20:28; 1 Tim. 3:2-7.]
3Msiwatawale wateule, ila mwe vielezo vya kikundi cha kwenu![#Ez. 34:2-10; 2 Kor. 1:24; Tit. 2:7.]
4Mkiwa hivyo mtapewa kilemba chenye utukufu kisichonyauka, hapo, mchungaji mkuu atakapotokea waziwazi.[#1 Petr. 2:25; 1 Kor. 9:25; 2 Tim. 4:8; Ebr. 13:20.]
5Vilevile ninyi mlio watu wazima, watiini wazee!* Nyote tumikianeni kila mtu na mwenziwe, kama ni mtumwa wake kwa kujinyenyekeza!
Kwani wenye kujikweza Mungu huwapingia,
lakini wanyenyekevu huwapatia huruma.
6Kwa hiyo unyenyekeeni mkono wa Mungu ulio wenye nguvu, yeye awakweze, siku yake itakapofika![#Iy. 22:29; Yak. 4:10.]
7Mtupieni Mungu yote, myahangaikiayo! Kwani yeye huwatunza.[#Sh. 55:23; Mat. 6:25; Luk. 22:31; Fil. 4:6.]
8Levukeni, mkeshe! Kwani mpingani wenu Satani huzunguka kama simba anayenguruma akitafuta, atakayemmeza.[#1 Tes. 5:6.]
9Huyo mgombanisheni kwa nguvu ya kumtegemea Mungu mkijua, ya kuwa mateso yayo hayo huwapata nao ndugu zenu walioko ulimwenguni![#Ef. 6:11-13.]
10Naye Mungu mwenye mema yote ya kuwagawia, aliyewaitia nanyi utukufu wake wa kale na kale uliomo katika Kristo, atawalinganya mwenyewe, mkiteseka kidogo, na kuwapa uwezo na nguvu na msingi mgumu.[#1 Petr. 1:6.]
11Wake yeye ni utukufu na uwezo kale na kale pasipo mwisho! Amin.*
12Nimewaandikia kidogo kwa mkono wa ndugu Silwano, ninayemwona kuwa mwelekevu. Nimewaonya na kuwashuhudia kwamba: Mmegawiwa mema ya Mungu yaliyo ya kweli. Nayo yakalieni![#Ebr. 13:22.]
13Wateule waliomo humu Babiloni pamoja nasi wanawasalimu, hata mwanangu Marko.[#Tume. 12:12,25; 2 Tim. 4:11.]
14Mwamkiane na kunoneana kwa kupendana! Utengemano uwakalie nyote mlio wake Kristo![#1 Kor. 16:20.]