The chat will start when you send the first message.
1Ndugu, hampaswi na kuandikiwa, kama itakuwa mwaka gani au siku gani, hayo yatakapokuwapo.[#Mat. 24:36.]
2Kwani wenyewe mwajua sana: siku ya Bwana itafika, kama mwizi anavyokuja usiku.
3Watakaposema: Pametengemana, pametulia, ndipo, watakapogunduliwa na mwangamizo, kama uchungu wa kuzaa unavyompata mwenye mimba; kwa hiyo hawataweza kukimbia.[#Mat. 24:42-44; 2 Petr. 3:10; Ufu. 3:3; 16:15.]
4Lakini ninyi, ndugu, hammo gizani, kwa hiyo siku ile hitawafumania kama mwizi.[#Yer. 6:14; Mat. 24:39.]
5Kwani ninyi wote ni wana wa mwanga na wana wa mchana; sisi hatu wa usiku, wala wa giza.[#Rom. 13:12; Ef. 5:9.]
6Kwa sababu hii tusilale usingizi, kama wale wengine wanavyolala usingizi, ila tukeshe na kulevuka!
7Kwani wanaolala usingizi hulala usiku, nao wanaolewa hulewa usiku.
8Lakini sisi tulio wa mchana tulevuke! Kisha tujivike mata: kumtegemea Mungu na kupendana kuwe kanzu zetu za chuma, nako kuungojea wokovu kuwe kofia zetu ngumu.[#Ef. 6:14-17.]
9Kwani Mungu hakutuweka, tuishie kwa makali yake, ila alituweka, tuupate wokovu kwa kazi ya Bwana wetu Yesu Kristo
10aliyekufa kwa ajili yetu sisi, tupate kuishi pamoja naye yeye, tukiwa tuko macho, au tukiwa tumelala usingizi.[#1 Tes. 4:14; Rom. 14:8-9.]
11Kwa hiyo mtulizane na kujengana kila mmoja na mwenzake, kama mnavyofanya![#Yuda 20.]
12Ndugu, twawaomba sana, mwajue wale wanaojisumbua kwenu ninyi wakiwasimamia, mkae naye Bwana, tena wakiwaonya.[#1 Kor. 16:18.]
13Jipigieni sana kuwapa macheo na kuwapenda kwa ajili ya kazi yao! Pataneni ninyi kwa ninyi!
14*Lakini twawahimiza ninyi, ndugu: Waaonyeni wenye mambo ya ovyo tu, watulizeni wenye mioyo miepesi, wasaidieni wanyonge, wo wote waendeeni kwa uvumilivu![#2 Tes. 3:15.]
15Mwangalie, mtu asimlipe mwenziwe uovu kwa uovu! Ila siku zote myafuate yaliyo mema, myapatiane ninyi kwa ninyi, hata wengine wote![#Fano. 20:22; Rom. 12:17,21; 1 Petr. 3:9.]
16Changamkeni siku zote![#Fil. 4:4.]
17Mwombeni Mungu pasipo kukoma![#Luk. 18:1-8; Rom. 12:12; Kol. 4:2.]
18Katika mambo yote toeni shukrani! Kwani haya ndiyo, Mungu ayatakayo, myafanye, kwa kuwa wake Kristo Yesu.[#Ef. 5:20.]
19Roho msimzime![#1 Kor. 14:30,39.]
20Mafumbuo msiyabeze![#1 Kor. 14:1.]
21Ila yote yapambanueni, kisha lishikeni lililo jema![#1 Kor. 14:29; 1 Yoh. 4:1.]
22Yote yaonekanayo kuwa mabaya yaepukeni!
23Lakini yeye Mungu aliye mwenye utengemano awatakase ninyi nyote miili na mioyo, kwamba roho zenu zote nzima pamoja na mioyo na miili zilindwe, zikae pasipo doadoa lo lote, mpaka Bwana wetu Yesu Kristo atakaporudi!
24Naye aliyewaita ni mwelekevu, naye ndiye atakayeyafanya.*[#1 Kor. 1:9; 2 Tes. 3:3.]
25Ndugu, tuombeeni kwake Mungu!
26Wasalimuni ndugu wote na kunoneana, kama watakatifu walivyozoea![#1 Kor. 16:20.]
27Nawaapisha ninyi kwa Bwana, barua hii isomewe ndugu wote.
28Upole wa Bwana wetu Yesu Kristo uwakalie! Amin.