The chat will start when you send the first message.
1Mwanawe Yosafati akawa mfalme mahali pake, akajipatia nguvu za kuwatawala Waisiraeli.[#1 Fal. 15:24.]
2Akaweka vikosi vya askari katika miji yote ya Yuda iliyokuwa na maboma, kisha akaweka wenye amri katika nchi ya Yuda, namo katika miji ya Efuraimu, baba yake Asa aliyoiteka.
3Bwana akawa naye Yosafati, kwani aliendelea katika njia ya kwanza ya babu yake Dawidi, asiitafute miungu ya Baali,
4ila alimtafuta Mungu wa baba yake, akaendelea na kuyashika maagizo yake, asifanye matendo ya Waisiraeli.
5Kwa hiyo Bwana akaushupaza ufalme wake mkononi mwake, Wayuda wote wakampa Yosafati matunzo, akapata mali na macheo mengi.[#2 Mambo 18:1.]
6Kwa kuzishika njia za Bwana moyo wake ukawa mkuu, kisha akayaondoa matambiko ya vilimani na miti ya Ashera katika nchi ya Yuda.
7Katika mwaka wa tatu wa ufalme wake akatuma watu wake Benihaili na Obadia na Zakaria na Netaneli na Mikaya, waende kufundisha watu katika miji ya Yuda;
8pamoja nao walikuwa Walawi Semaya na Netania na Zebadia na Asaheli na Semiramoti na Yonatani na Adonia na Tobia na Tobu-Adonia; pamoja nao hawa Walawi walikuwa watambikaji Elisama na Yoramu.
9Wakawafundisha watu katika nchi ya Yuda wakikishika kitabu cha Maonyo ya Bwana, wakazunguka katika miji yote ya Yuda na kufundisha watu.
10Stusho la Bwana likaziguia nchi zote zenye wafalme zilizoizunguka nchi ya Yuda, wasipigane na Yosafati.
11Kwao Wafilisti wakatoka wajumbe, wakamletea Yosafati matunzo na fedha, walizozichanga, Waarabu nao wakamletea mbuzi na kondoo, madume ya kondoo walikuwa 7700, hata madume ya mbuzi 7700.[#1 Fal. 14:21.]
12Ndivyo, Yosafati alivyoendelea kuwa mkuu zaidi, akajenga katika nchi ya Yuda ngome na miji yenye vilimbiko.
13Akawa na mapato mengi mle mijini mwa Yuda, namo Yerusalemu akawa na watu wa kupiga vita waliokuwa mafundi wenye nguvu.
14Wakijipanga kwa milango ya baba zao, ikawa hivyo: Wayuda walikuwa na wakuu wa maelfu, mkuu mwenyewe ni Adina, pamoja naye wakawa mafundi wa vita wenye nguvu 300000.
15Wa pili ni mkuu Yohana, pamoja naye wakawa watu 280000.
16Akafuatwa na Amasia, mwana wa Zikiri, aliyejitoa mwenyewe kuwa mtu wa Bwana, pamoja naye wakawa mafundi wa vita wenye nguvu 200000.
17Kwao Wabenyamini Eliada alikuwa fundi wa vita mwenye nguvu, pamoja naye wakawa watu 200000 waliochukua pindi na ngao.
18Wa pili alikuwa Yozabadi, pamoja naye wakawa watu 180000 wenye mata ya vita.
19Hawa ndio waliomtumikia mfalme kuliko wale, mfalme aliowaweka katika miji yenye maboma katika nchi yote ya Yuda.