The chat will start when you send the first message.
1Wenyeji wa Yerusalemu wakampa mwanawe mdogo Ahazia ufalme mahali pake, kwani wakubwa wake wote waliuawa na kikosi kilichokuja na Waarabu kambini. Ndivyo, Ahazia, mwana wa Yoramu, alivyopata kuwa mfalme wa Wayuda.
2Alikuwa mwenye miaka 22, alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu mwaka mmoja. Jina la mama yake ni Atalia, binti Omuri.
3Yeye naye akaendelea katika njia za mlango wa Ahabu, kwani mama yake ndiye aliyemwongoza kuyafanya yaliyo maovu.
4Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama mlango wa Ahabu, kwani hao ndio waliomwongoza, baba yake alipokwisha kufa, wampatie mwangamizo.
5Kwa kuongozwa nao akaja kwenda na Yoramu, mwana wa Ahabu, mfalme wa Waisiraeli, kumpelekea Hazaeli, mfalme wa Ushami, vita huko Ramoti wa Gileadi. Washami walipomwumiza Yoramu,
6akarudi Izireeli, apate watakao mponya vidonda, walivyompiga kule Rama, alipopigana na Hazaeli, mfalme wa Ushami. Ndipo, Azaria, mwana wa Yoramu, mfalme wa Wayuda, aliposhuka kumtazama Yoramu, mwana wa Ahabu, huko Izireeli, kwani ndiko, alikougulia.
7Hili lilitoka kwake Mungu kuwa mwangamizo wake Ahazia, alipofika kwa Yoramu: kwani alipokwisha kufika akatoka pamoja na Yoramu kwenda kupigana na Yehu, mwana wa Nimusi, Bwana aliyempaka mafuta, aung'oe mlango wa Ahabu.[#1 Fal. 19:16; 2 Fal. 9:6.]
8Ikawa, Yehu alipoupatiliza mlango wa Ahabu, akawaona nao wakuu wa Wayuda na wana wa ndugu zake Ahazia waliomtumikia Ahazia, akawaua.[#2 Fal. 10:12-14.]
9Alipoagiza kumtafuta Ahazia, wakamkamatia Samaria, alikojificha, wakampeleka kwa Yehu, wakamwua, wakamzika, kwani walisema: Yeye ni mwana wa Yosafati aliyemtafuta Bwana kwa moyo wake wote. Lakini katika mlango wa Ahazia hakuwako mwenye nguvu aliyeweza kuwa mfalme.[#2 Fal. 9:27-29.]
10Atalia, mamake Ahazia, alipoona, ya kuwa mwanawe amekufa, akaondoka, akawaua wazao wote wa kifalme wa mlango wa Yuda.
11Lakini Yosabati, binti mfalme, akamchukua Yoasi, mwana wa Ahazia, akamwiba katikati ya wana wa mfalme waliokwenda kuuawa, akamweka pamoja na mnyonyeshaji wake katika chumba cha kulalia. Ndivyo, Yosabati, binti mfalme Yoramu, mkewe mtambikaji Yoyada, aliyekuwa umbu lake Ahazia, alivyomficha Yoasi, Atalia asimwone, asipate kumwua.
12Akakaa kwao Nyumbani mwa Mungu na kufichwa miaka sita, Atalia alipokuwa mfalme wa kike wa nchi hiyo.