2 Mambo 27

2 Mambo 27

Yotamu ni mfalme mwema.

(Taz. 2 Fal. 15:32-36,38.)

1Yotamu alikuwa mwenye miaka 25 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 16 mle Yerusalemu. Jina la mama yake ni Yerusa, binti Sadoki.

2Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana kama yote, aliyoyafanya baba yake Uzia, namo Jumbani mwa Bwana hakuingia; lakini watu wakaendelea kuyafanya yasiyofanywa.[#2 Mambo 26:16.]

3Yeye ndiye aliyelijenga lango la juu la Nyumba ya Bwana, hata kuta za Ofeli akazijenga vema.

4Hata milimani katika nchi ya Yuda akajenga miji, nako miituni akajenga ngome na minara.[#2 Mambo 26:10.]

5Tena akapiga vita na mfalme wa wana wa Amoni akawashinda. Kwa hiyo wana wa Amoni hawakuwa na budi kumpa katika mwaka huo vipande 100 vya fedha, ndio shilingi milioni na 200000 na ngano frasila 100000 na mawele vilevile frasila 100000. Hata mwaka wa pili na wa tatu wana wa Amoni wakamtolea yayo hayo.

6Yotamu akendelea kupata nguvu, kwa kuwa njia zake, alizozishika, zilimwelekea Bwana Mungu wake.

Kufa kwake Yotamu.

7Mambo mengine ya Yotamu na vita vyake vyote na njia zake tunaziona, zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Waisiraeli na wa Wayuda.

8Alikuwa mwenye miaka 25 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 16 mle Yerusalemu.

9Kisha akaja kulala na baba zake, wakamzika mjini mwa Dawidi, naye mwanawe Ahazi akawa mfalme mahali pake.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania