The chat will start when you send the first message.
1Mimi Paulo niliye mtume wa Kristo Yesu kwa hayo, Mungu ayatakayo, na ndugu Timoteo tunawaandikia ninyi wateule wa Mungu mlioko Korinto nanyi watakatifu nyote mlioko katika nchi yote ya Akea.[#1 Kor. 1:1.]
2Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo![#Rom. 1:7.]
3Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Ndiye Baba anayewaonea wote uchungu na Mungu anayeipoza mioyo yao wote.[#Rom. 15:5.]
4Naye ndiye anayetupoza nasi mioyo katika maumivu yetu yote. Kwa hiyo hata sisi twaweza kuwapoza mioyo wale walio katika maumivu yo yote, tukiwapoza mioyo, kama nasi wenyewe tulivyopozwa mioyo na Mungu.
5Kwani hivyo tunavyofuliza kuteseka, kama Kristo alivyoteseka, vivyo hivyo tunafuliza kupozwa mioyo yetu naye Kristo.[#Sh. 34:20; 94:19.]
6Ikiwa tunaumizwa, ni kwa kwamba: Ninyi mpate kupozwa mioyo na kuokoka; ikiwa tunapozwa mioyo, ni kwa kwamba: Ninyi mpozwe mioyo, mwipate ile nguvu inayoonekana hapo, mnapoyavumilia mateso yaleyale, tunayoteswa nasi.[#2 Kor. 4:15,17.]
7Navyo, tunavyongojea kwa ajili yenu, vina nguvu, kwani tumejua: kama mlivyogawiwa mateso, vivyo hivyo mtagawiwa nao upozi wa mioyo.
8Kwani hatutaki, ndugu, mkose kuyajua mambo ya maumivu yetu yaliyotupata huko Asia, ya kuwa tulilemewa nayo, yakituumiza kuzipita nguvu zetu, tukapotelewa kwamba: Hatutapona.[#Tume. 19:23-30; 1 Kor. 15:32.]
9Tukawa tumekata wenyewe mioyoni mwetu kwamba: Sisi tu watu wa kufa tu; tukakataa kujishikiza wenyewe, tupate kushikizwa naye Mungu anayewafufua wafu.
10Yeye aliyetuponya kufa kulikokuwa hivyo hataacha kutuponya tena; kwa hiyo tunamngojea kwamba: Atafuliza kutuponya vivyo hivyo.[#2 Tim. 4:18.]
11Humo hata ninyi mwatusaidia mkituombea; maana wakiwa wengi wanaotutazama, nayo matukuzo yatatoka mioyoni mwa wengi kwa ajili ya kipaji, nilichogawiwa kwa kuombewa nao wengi.
12Kwani majivuno yetu ndio ushahidi wa mioyo yetu inayoyajua ya kwamba: Tumeendelea ulimwenguni kuwa wenye utakatifu wa kweli wa Kimungu; huu hautoki penye werevu wa kimtu, ijapo uwe wa kweli, ila tumegawiwa naye Mungu; nako kwenu tumejikaza kuwa hivyo.[#2 Kor. 2:17; 1 Kor. 1:17; Ebr. 13:18.]
13Kwani hatuwaandikii menginemengine, ni yaleyale, mnayoyasoma na kuyatambua. Nami natumaini, ya kuwa mtayatambua maana pasipo kusaza,
14kama mlivyotutambua na sisi mafungufungu; kwani majivuno yenu ni sisi, kama ninyi mtakavyokuwa majivuno yetu siku ile ya Bwana wetu Yesu.[#2 Kor. 5:12; Fil. 2:16.]
15Kwa kushikizwa hivyo moyoni, nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ninyi mpate kuamkiwa mara mbili:
16hapo, nikipita kwenu kwenda Makedonia, tena nikitoka Makedonia kuja kwenu ninyi, nipate kusindikizwa nanyi, kwenda Yudea.[#1 Kor. 16:5-6.]
17Basi, nilipotaka hivyo, je? Nalijitakia juujuu tu? Au, nayatakayo, nayataka kimtu? Nikisema: Ndio, sharti iwe ndio? Au nikisema: Sio, sharti iwe sio?
18Lakini Mungu ni mwelekevu, amejua ya kuwa: Neno letu, tulilowaambia, halina maana mbili: kuitikia na kukataa.
19Kwani Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, aliyetangazwa kwenu na sisi, mimi na Silwano na Timoteo, hakuwa mwenye kuitikia na kukataa, ila mwake yeye mlikuwa kuitikia tu.
20Kwani viagio vyote vya Mungu vilivyoko vimeitikiwa naye, kisha vimetimizwa naye, Mungu apate kutukuzwa nasi.[#Ufu. 3:14.]
21Lakini Mungu ndiye anayetutia nguvu sisi pamoja na ninyi, tuungane na Kristo; tena ndiye aliyetupatia cheo sisi[#1 Yoh. 2:27.]
22na kututia muhuri alipotupa Roho, akae mioyoni mwetu, awe rehani yetu.[#2 Kor. 5:5; Rom. 8:16; Ef. 1:13-14.]
23Mimi namtaja Mungu, aushuhudie moyo wangu ya kuwa: Sujaja tena Korinto, nipate kuwajia mwenye upole.[#2 Kor. 11:31; Rom. 1:9.]
24Hatujiwazii kuwa mabwana wa kuwaagiza tu, mtakayoyategemea kwenu, ila sisi tu wenzenu wa kusaidiana nanyi, tupate kufurahi pamoja. Kwani mngaliko mkimtegemea Mungu![#1 Petr. 5:3.]