2 Wakorinto 10

2 Wakorinto 10

Paulo alivyosingiziwa.

1Nawaonya ninyi kwa upole na kwa utu wa Kristo mimi Paulo mwenyewe niliye mnyenyekevu kwenu nikiwaona, nikawatolea makali nikiwa mbali![#1 Kor. 2:3.]

2Nawaomba, msinishurutishe kuyatumia hayo makali nitakapofika. Mwenyewe nadhani, yafaa kuwaendea na nguvu wale wachache wanaotudhania, ya kwamba sisi huendelea na kufuata tamaa za miili.[#2 Kor. 10:11; 1 Kor. 4:21.]

3Kwani hata tunapoendelea katika miili hatujigombei, kama miili itakavyo.

4Kwani mata ya magombano yetu si ya kimwili, lakini yako na nguvu ya Kimungu, yaweza kubomoa ngome kama hapo, yanaponyenyekeza mawazo yote[#Ef. 6:13-17.]

5ya kujikweza na kuuinukia utambuzi wa Mungu, au yanapoteka mawazo yote, yaje kumtii Kristo.[#Rom. 8:39.]

6Nasi tuko tayari kumlipiza kila mtu asiyetii, hapo mtakapokuwa mmemaliza kutii.

7Yatazameni yanayoonekana machoni! Mtu akijishikiza kwa kwamba: Ni wa Kristo, na atie hili nalo moyoni la kwamba: Kama yeye alivyo wa Kristo, vivyo hivyo nasi!

8Ikiwa nafuliza kujivunia nguvu yetu, Bwana aliyotupa, tuwajenge, tusiwajengue, napo hapo sitashindika kuwa mwongo,[#2 Kor. 12:6; 13:10; 1 Kor. 5:4-5.]

9wala sitafanana na mtu anayewaogopesha tu kwa barua.

10Kwani wako wanisengenyao kwamba: Barua zake ni ngumu zenye nguvu, lakini akiwapo kwa mwili ni mnyonge, nayo maneno yake hubezeka.[#2 Kor. 10:1.]

11Aliye hivyo na alifikiri hili: tunavyovisema kwa barua tusipokuwapo, ndivyo, tutakavyovitimiza tutakapokuwapo.[#2 Kor. 13:2,10.]

12Kwani hatujipi moyo wa kujihesabu au kujifananisha nao walioko, wakijisifu wenyewe. Lakini hao hakuna, wajuacho maana, kwani kipimo chao cha kujipima ndio wenyewe tu, nao mfano wa kujifananisha nao ndio wenyewe tu.[#2 Kor. 3:1; 5:12.]

13Lakini sisi hatutaki kujivuna pasipo kipimo, ila kipimo chetu ni mpaka, Mungu aliotukatia; hivyo tulifika hata kwenu.[#Rom. 12:3.]

14Kwani hatujitanui wenyewe kama wasiowafikia, maana hata kwenu ni sisi waliotangulia kuwatangazia Utume mwema wa Kristo.

15Nasi hatuupiti mpaka, tujivunie masumbuko yao wengine, lakini kumtegemea Mungu kutakapokulia kwenu, papo hapo tunangojea mipaka yetu, tuliyowekewa, ikuzwe kuipita ile ya kwenza,[#Rom. 15:20; Gal. 1:16; 2:7.]

16tupate kuutangaza Utume mwema hata kwao wakaao mbali kuwapita ninyi. Lakini hatutafuti majivuno tukiingia nchi iliyoisha kupigiwa hiyo mbiu njema na wengine.[#Tume. 19:21.]

17Lakini mwenye kujivuna na ajivunie kuwa wa Bwana![#Yer. 9:23-24; 1 Kor. 1:31.]

18Kwani anayejisifu mwenyewe siye mkweli, ila yule anayesifiwa na Bwana.[#1 Kor. 4:5.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania