The chat will start when you send the first message.
1Hii itakuwa mara ya tatu, nikija kwenu. Hapo kila jambo litamalizika kwa kusemewa na mashahidi wawili au watatu.[#5 Mose 19:15; Mat. 18:16; 1 Tim. 5:19.]
2Nimekwisha kusema kale, nilipokuwako kwenu mara ya pili, tena nayasema sasa, nisipokuwako kwenu, kwamba: Waliokosa kale nao wote wengine, hapo, nitakapokuja tena sitawapatia upole.
3Kwani mwataka kujaribu, kama ni Kristo kweli anayesema kinyuwani mwangu; naye hawaendei kwa unyonge, ila hutenda nguvu kwenu.[#Rom. 15:17-19.]
4Kweli amewambwa msalabani kama mnyonge, lakini anaishi kwa nguvu ya Mungu. Nasi ijapo tuwe wanyonge kwa kuwa wake, ninyi mtaona, tutakavyoishi pamoja naye kwa nguvu ya Mungu.
5Jijaribuni, kama mnakuwa mnamtegemea! Jionyesheni kuwa wakweli! Au hamjitambui wenyewe, kama Yesu Kristo mnaye mwenu? Msipoyajua, ham wa kweli.[#1 Kor. 11:28.]
6Lakini nangojea, mtutambue sisi kuwa wenye kweli.
7Lakini twamwomba Mungu, ninyi msifanye uovu wo wote, siko kwamba sisi tuonekane kuwa wakweli, ila ni kwamba ninyi myafanye yaliyo mazuri, nasi tuwe kama waongo.
8Kwani hakuna, tunachokiweza tukiyazuia yaliyo ya kweli, ila sisi hujipingia yaliyo ya kweli.
9Kwani twachangamika, tukiwa wanyonge sisi, ninyi mkiwa wenye nguvu. Nalo hili ndilo, tuliombalo: ninyi mtengenezeke!
10Sasa nisipokuwako kwenu, nayaandikia haya kwamba: Nitakapokuwako kwenu nisitumie ukali wa kukata maneno; nguvu ya kuvifanya hivyo nimepewa na Bwana, lakini ni ya kujenga, siyo ya kujengua.[#2 Kor. 10:8,11.]
11Mwisho, ndugu, furahini, mtengenezane, mwonyane, mioyo yenu iwe mmoja, mpate kutengemana! Ndipo, Mungu aliye mwenye upendo na matengemano atakapokuwa pamoja nanyi.[#Rom. 15:33; Fil. 4:4.]
12Mwamkiane mkinoneana, kama watakatifu walivyozoea! Watakatifu wote wanawasalimu.[#1 Kor. 16:20.]
13Upole wa Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu na bia ya Roho Mtakatifu iwakalie ninyi nyote! Amin.