The chat will start when you send the first message.
1Basi, wenzangu, kwa sababu tumepewa viagio kama hivyo, na tujitakase na kuondoa madoa yote ya miili na ya roho! Hivyo tutautimiza utakatifu, maana tutamwogopa Mungu.*
2Tupatieni kao mioyoni mwenu! Hakuna tuliyempotoa, hakuna tuliyemponza, hakuna tuliyemdanganya.[#2 Kor. 12:17; Tume. 20:33.]
3Siyasemei kwamba: Niwapatilize. Kwani nimesema kwanza, ya kuwa mmo mioyoni mwetu, tufe pamoja, kisha tupate kuishi pamoja.[#2 Kor. 6:11-13.]
4*Nikisema nanyi nasema waziwazi kabisa, tena yako mengi yenu, ninayojivunia. Moyo wangu umetulia wote, ukafuliza kuchangamka, hata tukipatwa na maumivu mengi.
5Kwani tulipofika Makedonia, miili yetu haikuweza kupumzikia kwa ajili ya maumivu yaliyotupata po pote, nje yalikuwako magombano, ndani mahangaiko.[#Tume. 20:1-2.]
6Lakini Mungu anayewatuliza wanyenyekevu mioyoni mwao, alitutuliza sisi kwa kuja kwake Tito.[#2 Kor. 1:3-4; 2:13.]
7Lakini kulikotutuliza siko kuja kwake tu, ila nao utulivu, mwenyewe aliotulizwa nao alipowaona, mlivyo. Naye akatusimulia, mnavyotunukia kutuona, mnavyosikitika, mnavyofanya bidii kwa ajili yangu mimi. Hivi vikanifurahisha kuliko vingine.
8Nami ikiwa nimewasikitisha na barua yangu sijuti sasa. Na kama nalijuta hapo, nilipoona, ya kuwa ile barua imewasikitisha kitambo,[#2 Kor. 2:4.]
9sasa nafurahi, si kwa sababu mmesikitishwa, ila kwa sababu masikitiko, mliyoyapata, yamewafundisha majuto. Kwani mmesikitishwa Kimungu, maana msiponzwe na jambo lo lote litokalo kwetu.
10Kwani sikitiko la Kimungu humpeleka mtu penye wokovu, likimpatia majuto yasiyojutika tena. Lakini sikitiko la kiulimwengu humpeleka mtu penye kufa.*[#Mat. 27:3-5; Yoh. 21:17; Ebr. 12:11.]
11Kwani tazameni, kule kusikitishwa Kimungu kuko huko ndiko kulikowahimiza hivyo, mjikanie kwa kuona machukivu na woga, mkatunukia kulilipiza lile neno upesi. Mlipoyafanya hayo yote mmejitokeza wenyewe, ya kuwa hammo katika jambo lile.
12Nami hapo, nilipowaandikia, sikuandika kwa ajili yake aliyepotoa, wala kwa ajili yake aliyepotolewa, ila naliandikia kwamba: Kwenu kuonekane, ninyi mnavyojihimiza kwa ajili yetu mbele ya Mungu.
13Kwa hiyo tumetulizwa mioyo; na kwa hivyo, mioyo yetu ilivyotulia, furaha yetu ikaongezwa na furaha, Tito aliyokuwa nayo, kwani roho yake imepozwa kwenu po pote.
14Kama liko jambo la kwenu, nililojivunia kwake, halikunitokeza kuwa mwongo; lakini kama tulivyowaambia nanyi yote yaliyo ya kweli, vivyo hivyo hata yale, tuliyojivunia kwake Tito, yaliyokuwa ya kweli.
15Ndipo, moyo wake ulipowageukia, ukafuliza kuwapenda, akiwakumbuka, ninyi nyote mlivyomtii, mlivyompokea, woga ukiwatetemesha.[#2 Kor. 2:9.]
16Nafurahi, ya kuwa ninaweza kuwatazamia ninyi katika mambo yo yote.