The chat will start when you send the first message.
1Elisa alikuwa amesema na yule mwanamke, aliyemfufulia mwanawe, akamwambia: Ondoka, uende wewe na mlango wako, ukae ugenini kutakakokufalia kukaa ugenini! Kwani Bwana ameita njaa, ije kuiingia hata nchi hii miaka saba.[#2 Fal. 4:35.]
2Ndipo, yule mwanamke alipoondoka, akafanya, kama yule mtu wa Mungu alivyomwambia, akaenda yeye na mlango wake, akakaa ugenini katika nchi ya Wafilisti miaka saba.
3Hiyo miaka saba ilipokwisha pita, yule mwanamke akaondoka tena katika nchi ya Wafilisti, akarudi, akamtokea mfalme kumlilia kwa ajili ya nyumba yake na ya shamba lake.
4Hapo mfalme alikuwa akisema na Gehazi aliyekuwa naye yule mtu wa Mungu kwamba: Nisimulie matendo makubwa yote, Elisa aliyoyafanya!
5Naye akawa akimsimulia mfalme, jinsi alivyomrudisha yule mfu uzimani, mara yule mwanamke, aliyemfufulia mwanawe, akawako akimlilia mfalme kwa ajili ya nyumba yake na ya shamba lake. Ndipo, Gehazi alipomwambia: Bwana wangu mfalme, huyu ndiye yule mwanamke, naye huyu ndiye mwanawe, Elisa aliyemfufua.
6Mfalme alipomwuliza huyu mwanamke, naye akamsimulia yote. Ndipo, mfalme alipompa mtumishi mmoja wa nyumbani, akamwagiza: Mrudishie yote yaliyokuwa yake nayo mapato yote ya shamba yaliyopatikana tangu sike ile, alipoiacha nchi hii, hata sasa.
7Kisha Elisa akaja Damasko, naye Benihadadi, mfalme wa Ushami, alikuwa mgonjwa, akapashwa habari, ya kuwa yule mtu wa Mungu amefika huko.
8Ndipo, mfalme alipomwambia Hazaeli: Chukua matunzo mkononi mwako, uende kuonana na yule mtu wa Mungu, umwombe, aniulizie kwa Bwana, kama nitapona ugonjwa huu.
9Hazaeli akaenda kuonana naye akichukua mkononi mwake matunzo yote yaliyokuwa vitu vizuri vya Damasko, ya kuchukuliwa na ngamia 40. Alipofika akaja kusimama mbele yake, akamwambia: Mwanao Benihadadi, mfalme wa Ushami, amenituma kwako kukuuliza kwamba: Nitapona ugonjwa huu?
10Elisa akamjibu: Nenda kumwambia: Kupona utapona; lakini Bwana amenionyesha, ya kuwa atakufa.
11Kisha yule mtu wa Mungu akamng'arizia macho na kulia machozi, hata mwenyewe akiona soni kwa kufanya hivyo.[#Luk. 19:41.]
12Hazaeli akamwuliza: Mbona bwana wangu analia machozi? Akajibu: Kwani ninajua, ya kama utawafanyizia wana wa Isiraeli mabaya, miji yao yenye maboma utaiteketeza kwa moto, vijana wao wenye nguvu utawaua kwa panga, wachanga wao utawaponda nao wanawake wao wenye mimba utawatumbua.[#2 Fal. 10:32.]
13Hazaeli akasema: Mtumwa wako, huyu mbwa, ni mtu gani, aweze kufanya mambo makuu kama hayo? Elisa akasema: Bwana amenionyesha, ya kuwa wewe utakuwa mfalme wa Ushami.[#1 Sam. 24:15; 1 Fal. 19:15.]
14Kisha akatoka kwake Elisa, akaja kwa bwana wake, naye akamwuliza: Elisa amekuambia nini? Akajibu: Ameniambia, ya kuwa utapona.
15Kesho yake akachukua tandiko la kitanda, akalichovya majini, kisha akamfunika uso nalo, hata akafa. Naye Hazaeli akawa mfalme mahali pake.
16Katika mwaka wa 5 wa Yoramu, mwana wa Ahabu, mfalme wa Waisiraeli, Yosafati alipomaliza kuwa mfalme wa Wayuda, Yoramu, mwana wa Yosafati, akapata kuwa mfalme wa Wayuda.[#1 Fal. 22:51.]
17Alikuwa mwenye miaka 32 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 8.
18Naye akaendelea katika njia za wafalme wa Waisiraeli, kama wale wa mlango wa Ahabu walivyofanya, kwani binti Ahabu alikuwa mkewe, akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana.[#2 Fal. 8:26.]
19Lakini Bwana hakutaka kuwaangamiza Wayuda kwa ajili ya mtumishi wake Dawidi, kwa kuwa alimwambia, ya kama atampa yeye na wanawe kuwa taa iwakayo siku zote.[#2 Sam. 7:11-16; 1 Fal. 11:36.]
20Katika hizo siku zake Waedomu wakalivunja agano wakijitoa mikononi mwa Wayuda, wakajiwekea mfalme wa kuwatawala.
21Ndipo, Yoramu alipoondoka kwenda Sairi akiyachukua magari yote; ikawa, alipoondoka usiku, akawapiga Waedomu waliomzunguka yeye na wakuu wa magari lakini watu walikuwa wameyakimbilia mahema yao.
22Lakini Waedomu wakalivunja agano tena, wakajitoa mikononi mwa Wayuda mpaka siku hii ya leo. Kisha nao wa Libuna wakalivunja agano siku zilezile.
23Mambo mengine ya Yoramu nayo yote, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
24Yoramu akaja kulala na baba zake, akazikwa kwa baba zake mjini mwa Dawidi, naye mwanawe Ahazia akawa mfalme mahali pake.
25Katika mwaka wa 12 wa Yoramu, mwana wa Ahabu, mfalme wa Waisiraeli, Ahazia, mwana wa Yoramu, akapata kuwa mfalme wa Wayuda.
26Ahazia alikuwa mwenye miaka 22 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu mwaka mmoja. Jina la mama yake ni Atalia, binti Omuri, mfalme wa Waisiraeli.[#2 Fal. 8:18; 11:1.]
27Naye akaendelea katika njia ya mlango wa Ahabu, akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama mlango wa Ahabu. Kwani yeye alikuwa mkwe wao wa mlango wa Ahabu.
28Akaenda pamoja na Yoramu, mwana wa Ahabu, kumpelekea Hazaeli, mfalme wa Ushami, vita huko Ramoti wa Gileadi, lakini Washami wakamwumiza Yoramu.
29Kwa hiyo mfalme Yoramu akarudi Izireeli, apate watakaomponya vidonda, Washami walivyompiga kule Rama, alipopigana na Hazaeli, mfalme wa Ushami. Ndipo, Ahazia, mwana wa Yoramu, mfalme wa Wayuda, aliposhuka kumtazama Yoramu, mwana wa Ahabu, huko Izireeli, kwani ndiko, alikougulia.[#2 Fal. 9:15-16,21.]