The chat will start when you send the first message.
1Hayo yalipokwisha, Abisalomu akajipatia magari na farasi na watu 50, wamtangulie na kupiga mbio.[#1 Fal. 1:5.]
2Kila siku Abisalomu hujidamka, kisha husimama mjini kando kwenye lango la mji. Basi, kila mtu aliyepita mwenye shauri la kwenda kwa mfalme kuamuliwa, Abisalomu humwita kwake na kumwuliza: Wewe unatoka mji gani? Aliposema: Mtumishi wako ni mmoja wao wa mashina ya Waisiraeli,
3Abisalomu humwambia: Tazama, shauri lako ni zuri, linapasa, lakini kwa mfalme hakuna atakayekusikiliza.
4Kisha Abisalomu husema: Kama wangeniweka mimi kuwa mwamuzi katika nchi hii, ningeyakata vema mashauri ya kila mtu atakayekuja kwangu mwenye neno la kugombana na mwenye shauri lo lote.
5Napo, mtu alipomkaribia, amwangukie, hukunjua upesi mkono wake, apate kumnonea.
6Hivyo ndivyo, Abisalomu alivyowafanyizia Waisiraeli wote waliokwenda shaurini kwa mfalme, navyo ndivyo, alivyoiiba mioyo ya waume wa Waisiraeli.
7Miaka 40 ilipokwisha, Abisalomu akamwambia mfalme: Na niende kumlipa Bwana huko Heburoni, niliyomwapia ya kumtolea.
8Kwani mtumishi wako ameapa kiapo, nilipokaa Gesuri kwa Washami, cha kwamba: Kama Bwana atanirudisha Yerusalemu, nitamtumikia Bwana.[#1 Mose 28:20; 2 Sam. 13:38.]
9Mfalme akamwambia: Nenda na kutengemana! Basi, akaondoka, akaenda Heburoni.[#1 Sam. 20:42.]
10Kisha Abisalomu akatuma wapelelezi kwa mashina yote ya Waisiraeli kwamba: Mtakaposikia, mabaragumu yakilia, semeni: Abisalomu amepata ufalme Heburoni!
11Pamoja na Abisalomu walikwenda toka Yerusalemu watu 200 walioalikwa naye, waliokwenda pasipo mawazo mabaya yo yote, maana hawakujua neno lo lote.
12Abisalomu akatuma kumchukua Ahitofeli wa Gilo aliyekuwa mmoja wao waliomwongoza Dawidi mashaurini; akamtoa huko Gilo mjini kwake, alipochinja ng'ombe za tambiko. Hivyo lile fujo likapata nguvu, nao watu waliorudi upande wa Abisalomu wakaendelea kuwa wengi zaidi.[#2 Sam. 23:34.]
13Mtu alipofika kwa Dawidi na kumpasha habari ya kwamba: Mioyo ya waume wa Waisiraeli imegeuka kumfuata Abisalomu,
14Dawidi akawaambia watumishi wake wote, aliokuwa nao Yerusalemu: Haya! Ondokeni, tukimbie! Kwani hatutapata kupona, Abisalomu akitujia. Pigeni mbio, twende, asitukamate upesi na kutufanyizia mabaya, akiwaua waliomo humu mjini kwa ukali wa panga.[#Sh. 3:1.]
15Watumishi wa mfalme wakamwambia mfalme: Yote yampendezayo bwana wetu mfalme, basi, sisi watumishi wako tuko.
16Kisha mfalme akatoka pamoja nao wote waliokuwamo nyumbani mwake, wakienda kwa miguu yao; mfalme akaacha masuria kumi tu wa kuiangalia nyumba.
17Mfalme alipokwisha kutoka hivyo pamoja na watu wake wote, wakienda kwa miguu, wakasimama penye nyumba ya mwisho.
18Ndipo, watumishi wake wote walipopita kando yake, nao Wakreti wote na Wapuleti wote na Wagati wote, watu 600 waliotoka Gati wakienda kwa miguu, wote pia wakapita hapo mbele ya mfalme.[#2 Sam. 8:18.]
19Mfalme akamwuliza Itai wa Gati: Mbona wewe nawe utakwenda pamoja na sisi? Rudi, ukae kwa mfalme! Kwani wewe u mgeni aliyefukuzwa kwao; haya! Nenda zako![#2 Sam. 18:2.]
20Umefika jana; basi, leo nitawezaje kukusumbua na kukuchukua kwenda na sisi? Mimi ninakwenda na kutangatanga po pote, nitakapokwenda, lakini wewe rudi! Nao ndugu zako warudishe pamoja na wewe, nao upole na welekevu na uwakalie!
21Itai akamjibu mfalme akisema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, tena bwana wangu mfalme alivyo mzima, mahali, bwana wangu mfalme atakapokuwa, kama ni pa kufia, au kama ni pa kuponea, ndipo, mtumishi wako naye atakapokuwa.
22Ndipo, Dawidi alipomwambia Itai: Basi, nenda nawe, upite! Naye Itai wa Gati akapita na watu wake wote na wake na watoto wote waliokuwa naye.
23Watu wote wa nchi hiyo wakalia na kuzipaza sauti zao pamoja na watu wote walipita hapo, mfalme alipouvuka mto wa Kidoroni pamoja na wale watu wote waliopita mbele yake, wakajielekeza kushika njia ya kwenda nyikani.[#Yoh. 18:1.]
24Mara akaja naye Sadoki pamoja na Walawi wote waliolichukua Sanduku la Agano la Mungu; wakalitua Sanduku la Agano, naye Abiatari akatambika, mpaka watu wote walipokwisha kupita na kutoka mjini.
25Mfalme akamwambia Sadoki: Lirudishe mjini Sanduku la Mungu! Kama nitaona upendeleo machoni pa Bwana, atanirudisha, nipate kuliona tena napo mahali, linapokaa.
26Lakini kama ataniambia hivi: Sipendezwi na wewe, basi, niko, anifanyizie atakayoyaona kuwa mema.[#1 Sam. 3:18; 2 Sam. 10:12.]
27Kisha mfalme akamwambia mtambikaji Sadoki: Je? Wewe siwe mtazamaji? Rudi mjini na kutengemana pamoja na mwanao Ahimasi na Yonatani, mwana wa Abiatari, hawa wana wenu wawili waende nanyi.[#1 Fal. 1:42.]
28Tazameni, mimi nitakawilia penye mbuga za nyikani, mpaka itafika kwangu habari toka kwenu.
29Kwa hiyo Sadoki na Abiatari wakalirudisha Sanduku la Mungu Yerusalemu, wakakaa huko.
30Dawidi akapapanda pa kuukwelea mlima wa michekele, akaenda akilia, nacho kichwa chake kilikuwa kimefunikwa, naye mwenyewe alikwenda pasipo kuvaa viatu; hata watu wote waliokuwa naye walikuwa wamekifunika kila mtu kichwa chake, nao wakawa wakipanda na kulia.
31Walipompasha Dawidi habari ya kwamba: Ahitofeli yuko kwa Abisalomu pamoja nao waliovunja maagano, Dawidi akasema: Bwana na aligeuze shauri la Ahitofeli kuwa ujinga!
32Dawidi alipofika pale juu, watu wanapomtambikia Mungu, mara akaja Mwarki Husai akimwendea njiani mwenye kanzu iliyoraruliwa na mwenye mchanga kichwani pake.
33Dawidi akamwambia: Ukienda pamoja nami safari yangu, ndipo, utakaponilemea.
34Lakini ukirudi mjini na kumwambia Abisalomu: Mimi nitakuwa mtumishi wako, mfalme; kama nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tangu kale, ndivyo, nitakavyokuwa sasa mtumishi wako. Basi, ndivyo, utakavyolitengua shauri la Ahitofeli.[#2 Sam. 17:7.]
35Je? Mle mjini hunao wale watambikaji Sadoki na Abiatari? Iwe hivyo: kila neno, utakalolisikia nyumbani mwa mfalme, uwasimulie wale watambikaji Sadoki na Abiatari.
36Tazama, wanao mle mjini wana wao wawili: Sadoki anaye Ahimasi, Abiatari anaye Yonatani. Kwa kuwatumia hao mtaweza kuniletea kila neno, mtakalolisikia.[#2 Sam. 17:15-17.]
37Ndipo, Husai aliyekuwa rafiki yake Dawidi aliporudi mjini, Abisalomu alipoingia Yerusalemu.[#1 Mambo 27:33.]