The chat will start when you send the first message.
1Haya ndiyo maneno ya mwisho ya Dawidi:
Hivyo ndivyo, asemavyo Dawidi, mwana wa Isai,
haya ndiyo, aliyoyasema mtu aliyetukuka sana, Mungu wa Yakobo alimpaka mafuta, kwa kuwatungia Waisiraeli nyimbo alipendeza.
2Roho ya Bwana hunitumia kuwa wa kusema,
Neno lake limo kinywani mwangu.
3Mungu wa Isiraeli aliniambia neno, aliye mwamba wa Waisiraeli alisema kwamba: Awatawalaye watu kwa wongofu, awatawalaye kwa kumcha Mungu,
4hufanana na mwanga wa asubuhi, jua linapokucha, huwa kama mapema ya asubuhi yasiyo na mawingu, majani mabichi huchipuka nchini, mvua ikiisha kuanuka; ni kwa nguvu za kuangaza kwake, vikiwa hivyo.
5Kumbe sivyo, mlango wangu ulivyo kwake Mungu?
Kwani aliniwekea agano kuwa la kale na kale, lilitengenezwa, yote yawe sawa, lipate kuangaliwa. Kwa hiyo asiyachipuze yote yawezayo kuniokoa, nayo yote pia yapendezayo?
6Lakini wao wote wasiofaa ni kama miiba inayotupwa tu, kwani haishikiki mikononi mwa watu.
7Mtu atakaye kuwajia hutumia vyuma tele na uti wa mkuki, kisha huteketezwa kwa moto papo hapo, walipokuwa.
8Haya ndiyo majina ya mafundi wa vita, Dawidi alio kuwa nao: Yosebu-Basebeti wa Takemoni, mkuu wa thelathini; yeye aliuchezesha mkuki wake juu ya watu 800; ndio, aliowaua kwa mara moja.
9Aliyemfuata ni Elazari, mwana wa Dodo, mwana wa mtu wa Ahohi; huyu alikuwa mmoja wao wale mafundi wa vita watatu waliokuwa na Dawidi, Wafilisti walipowatukana na kujipanga huko kupigana nao. Watu wa Waisiraeli walipokwenda zao mahali pa juu,
10yeye akainuka, akawapiga Wafilisti, mpaka mkono wake ukimlegea kwa kugandamana na upanga. Ilikuwa siku hiyo, Bwana alipowapatia wokovu mkubwa, kisha watu wakarudi na kumfuata, wateke nyara.
11Aliyefuata ni Sama, mwana wa Age, wa Harari. Wafilisti walipokusanyika wengi mno mahali palipokuwa na kipande cha shamba lenye kunde, watu wakawakimbia Wafilisti;
12ndipo, yeye alipokuja kusimama katikati ya hicho kipande cha shamba, akakiponya akiwapiga Wafilisti. Ndivyo, Bwana alivyowapatia wokovu mkubwa.
13Ikawa, hawa wakuu watatu waliomo miongoni mwao wakuu wa 30 wakashuka siku za mavuno, wafike kwa Dawidi penye pango la Adulamu; navyo vikosi vya Wafilisti vilikuwa vimepiga makambi Bondeni kwa Majitu.
14Naye Dawidi siku zile alikuwa ngomeni, nacho kikosi cha walinzi wa Wafilisti kilikuwamo Beti-Lehemu.
15Hapo Dawidi akaingiwa na tamaa, akasema: Yuko nani atakayeninywesha maji ya kisima cha Beti-Lehemu kilichoko langoni?
16Ndipo, wale mafundi wa vita watatu walipojipenyeza makambini mwa Wafilisti, wakachota maji katika kisima cha Beti-Lehemu kilichoko langoni, wakayachukua, wakamletea Dawidi, lakini hakutaka kuyanywa, akammwagia Bwana kuwa kinywaji cha tambiko,
17akasema: Bwana na anizuie, nisifanye kama hayo! Kumbe siyo damu za waume hao waliokwenda kwa kujitoa wenyewe? Kwa hiyo hakutaka kuyanywa. Haya waliyafanya wale mafundi wa vita watatu.
18Naye Abisai, ndugu yake Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu miongoni mwa watu watatu; yeye ndiye aliyeuchezesha mkuki wake juu ya watu 300; ndio, aliowaua, akawa mwenye macheo kwa hao watatu.[#2 Sam. 21:17.]
19Kwao hao watatu aliheshimiwa kweli kuliko wengine, akawa mkuu wao, lakini wale watatu wa kwanza hakuwa sawa nao.
20Benaya, mwana wa Yoyada, mwana wa mtu mwenye nguvu, alifanya matendo makuu, nako kwao kulikuwa Kabuseli. Yeye aliwaua wana wawili wa Arieli wa Moabu, tena siku moja, theluji ilipokuwa imeanguka, akashuka shimoni, akaua simba mlemle.[#Yos. 15:21; Neh. 11:25.]
21Naye ndiye aliyemwua mtu wa Misri aliyetisha kwa kutazamwa tu; namo mkononi mwake huyu Mmisri alishika mkuki. Lakini akamshukia na kushika fimbo tu, akampokonya yule Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa huo mkuki wake.
22Haya aliyafanya Benaya, mwana wa Yoyada, kwa hiyo alipata macheo kwa hao mafundi wa vita watatu.
23Kwa wale 30 aliheshimiwa kuliko wenziwe, lakini wale watatu wa kwanza hakuwa sawa nao. Naye Dawidi akamweka kuwa mkuu wa walinzi wake.
24Miongoni mwao wakuu wa 30 walikuwa: Asaheli, ndugu yake Yoabu; Elihanani, mwana wa Dodo wa Beti-Lehemu;[#2 Sam. 2:18.]
25Sama wa Harodi, Elika wa Harodi;
26Helesi wa Palti, Ira, mwana wa Ikesi, wa Tekoa;[#1 Mambo 27:9-10.]
27Abiezeri wa Anatoti, Mebunai wa Husa;
28Salmoni wa Ahohi, Maharai wa Netofa;
29Helebu, mwana wa Baana, wa Netofa, Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini;
30Benaya wa Piratoni, Hidai wa Nahale-Gasi;
31Abi-Alboni wa Araba, Azimaweti wa Barihumu;
32Eliaba wa Salaboni, Yonatani wa wana wa Yaseni;
33Sama wa Harari, Ahiamu, mwana wa Sarari, wa Arari;
34Elifeleti, mwana wa Ahasibai, mwana wa mtu wa Maka, Eliamu, mwana wa Ahitofeli, wa Gilo;[#2 Sam. 15:12.]
35Hesirai wa Karmeli, Parai wa Arabu;
36Igali, mwana wa Natani wa Soba, Bani wa Gadi;
37Mwamoni Seleki, Naharai wa Beroti aliyekuwa mchukua mata wa Yoabu, mwana wa Seruya;
38Mwitiri Ira, Mwitiri Garebu;
39Mhiti Uria. Wote pamoja ni 37.[#2 Sam. 11:3.]