The chat will start when you send the first message.
1Dawidi akauliza: Yuko bado aliyesalia wa mlango wa Sauli, nimgawie mema kwa ajili yake Yonatani?
2Kulikuwako mtumishi wa nyumbani mwa Sauli, jina lake Siba; wakamwita, aje kwa Dawidi, naye mfalme akamwuliza: Wewe ndiwe Siba? Akasema: Ndimi mtumishi wako.[#2 Sam. 16:1.]
3Mfalme akamwuliza: Yuko bado mtu wa mlango wa Sauli, nimgawie mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme: Yuko bado mwana wa Yonatani, naye amelemaa miguu.[#2 Sam. 4:4.]
4Mfalme akamwuliza: Yuko wapi? Siba akamwambia mfalme: Tazama, yumo nyumbani mwa Makiri, mwana wa Amieli, huko Lo-Debari.[#2 Sam. 17:27.]
5Ndipo, mfalme Dawidi alipotuma watu kumchukua nyumbani mwa Makiri, mwana wa Amieli, huko Lo-Debari.
6Mefiboseti, mwana wa Yonatani, mwana wa Sauli, alipofika kwake Dawidi akajiangusha usone pake kumwangukia; Dawidi akasema: Mefiboseti! Naye akasema: Mimi hapa mtumwa wako.
7Dawidi akamwambia: Usiogope! Kwani mimi nitakugawia mema kwa ajili ya baba yako Yonatani, nitakurudishia mashamba yote ya babu yako Sauli, tena wewe utakula chakula siku zote mezani pangu.
8Ndipo, alipomwangukia akisema: Mimi, mtumwa wako, ni nani, ukijielekeza kumtazama mbwa mfu, kama mimi nilivyo?[#1 Sam. 24:15.]
9Kisha Dawidi akamwita Siba, yule kijana wa Sauli, akamwambia: Yote yaliyokuwa mali zake Sauli na za mlango wake wote nimempa huyu mwana wa bwana wako.
10Nawe utamlimia shamba, wewe na wanao na watumishi wako, tena utamvunia mazao ya shambani, yawe chakula cha mwana wa bwana wako, ayale. Tena Mefiboseti, mwana wa bwana wako, atakula chakula siku zote mezani pangu. Naye Siba alikuwa mwenye wana 15 na watumishi 20.
11Siba akamwambia mfalme: Yote, bwana wangu mfalme anayomwagiza mtumwa wake, mtumwa wako atayafanya vivyo hivyo. Kwa hiyo Mefiboseti akawa akila mezani pa Dawidi kama mmoja wao wana wa mfalme.[#2 Sam. 19:28.]
12Naye Mefiboseti alikuwa na mwana mdogo, jina lake Mika, nao wote waliokaa nyumbani mwa Siba walikuwa watumishi wake Mefiboseti.
13Naye Mefiboseti akawa akikaa Yerusalemu, kwani alikuwa akila siku zote mezani pa mfalme, naye alikuwa amelemaa miguu yote miwili.[#2 Sam. 9:3.]