The chat will start when you send the first message.
1Sisi Paulo na Silwano na Timoteo tunawaandikia ninyi mlio wateule wa Tesalonike katika Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo![#1 Tes. 1:1.]
2Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo![#Rom. 1:7.]
3*Sharti tumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu; hii inatupasa, kwa sababu nguvu zenu za kumtegemea Mungu zinaongezeka sana, nao upendano unakua, maana ninyi nyote kila mmoja wenu humpenda mwenzake.[#2 Tes. 2:13; 1 Tes. 1:2-3.]
4Kwa hiyo hata sisi wenyewe twajivuna kwa ajili yenu katika wateule wa Mungu, kwamba mwavumilia, tena mwamtegemea Bwana katika mafukuzo na maumivu yenu yote, mnayojitwika.[#2 Kor. 7:4.]
5Humu ndimo, hukumu yake Mungu itakamoonekana kuwa ya kuongoka: ninyi mtaambiwa: Ufalme wa Mungu umewapasa kwa hivyo, mnavyoteswa kwa ajili yake huo.[#Luk. 21:36; Fil. 1:28.]
6Kwani wongofu wa Kimungu ndio huu: wenye kuwaumiza atawalipizia maumivu,[#Rom. 12:19; Ufu. 18:6-7.]
7nanyi mwumizwao mtapata kutulizwa pamoja nasi, Bwana Yesu atakapotokea waziwazi toka mbinguni pamoja na malaika wa nguvu zake.[#Mat. 16:27; 25:31-46; 1 Tes. 4:16.]
8Naye atashuka mwenye moto uwakao sana, awalipize wale wasiomjua Mungu, kwamba walikataa kuutii Utume mwema wa Bwana wetu Yesu.[#Yes. 66:15; Rom. 2:8.]
9Nalo lipizi, watakalolipata, ni mwangamizo wa kale na kale, maana watatupwa, wasiuone uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake.[#Yer. 2:10,19,21.]
10Hivi vitakuwa siku ileile, atakapokuja kutukuzwa kati ya watakatifu wake na kustaajabiwa kati yao wote wamtegemeao; kwani mambo hayo, tuliyoyashuhudia, yalipata kwenu wenye kuyategemea.*[#Kol. 3:4.]
11Kwa ajili ya neno hili twawaombea ninyi siku zote, Mungu wetu awape kufanya mwenendo uupasao wito wenu, mpate nguvu za kuyatimiza mema yote yaliyowapendeza na za kufanya matendo yafanyikayo kwa kumtegemea.
12Hivyo ndivyo, Jina la Bwana wetu Yesu litakavyotukuzwa mwenu, nanyi mtatukuzwa mwake, yatakapotimia yale, Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo aliyowagawia.