The chat will start when you send the first message.
1Mimi Paulo niliye mtume wa Kristo Yesu kwa hayo, Mungu ayatakayo, nikitangaze kiagio cha uzima uliomo mwake Kristo Yesu, nakuandikia barua, wewe Timoteo, mwanangu mpendwa.
2Upole ukukalie na wema na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu, Bwana wetu!
3Namshukuru Mungu, ninayemtambikia tangu siku za baba zangu kwa moyo utakatao kwa kujua mema tu. Nakukumbuka pasipo kukoma nikiomba usiku na mchana.[#Tume. 23:1; 24:16; Fil. 3:5.]
4Nami nikiyakumbuka machozi yako, ninatunukia kukuona wewe, furaha zinifurikie.
5Maana nakukumbuka moyoni, unavyomtegemea Mungu pasipo ujanja; kwanza bibi yako Loi alikukalia kumtegemea Mungu vivyo hivyo, kisha mama yako Eunike naye, lakini moyo wangu unajua, ya kuwa hata wewe unako.[#Tume. 16:1.]
6Kwa sababu hii nakukumbusha, uyafuate yale mema yaliyomo mwako, uliyogawiwa hapo, nilipokubandikia mikono.[#1 Tes. 5:19; 1 Tim. 4:14.]
7Kwani Mungu hakutupa Roho ya kutuogopesha, ila ya kututia nguvu na upendo tuonyeke.[#Rom. 8:15.]
8Basi, usiingiwe na soni ya kumshuhudia Bwana wetu, hata mimi niliyefungwa kwa ajili yake! Ila ukiumizwa vibaya kwa ajili ya Utume mwema vumilia pamoja nami kwa nguvu za Mungu![#Rom. 1:16.]
9Maana ndiye aliyetuokoa, ndiye aliyetuitia kuwa watakatifu; naye hakutuitia kwa hivyo, matendo yetu yalivyo, ila kwa hiyovyo, alivyotaka mwenyewe toka kale kutugawia yale mema yaliyomo mwake Kristo Yesu; ni yayo hayo, tuliyolimbikiwa mbele ya mwanzo wa siku za kale.[#Tit. 3:5.]
10Lakini siku za sasa yametufunikia hapo, mwokozi wetu Kristo Yesu alipotokea; ndiye aliyezitangua nguvu za kifo, kisha akatokeza mwangani uzima usioangamika, kama tulivyoambiwa na Utume mwema;[#Rom. 16:26; 1 Kor. 15:55,57; Ebr. 2:14.]
11nami nikawekwa kuutangaza na kuutumikia na kuufundisha.[#1 Tim. 2:7.]
12Kwa sababu yake nateseka hivyo, lakini sivionei soni, kwani namjua, nimtegemeaye. Tena ninalo shikizo hili la kwamba: Yuko na nguvu ya kulilinda limbiko langu, mpaka siku ile itakapotimia.[#2 Tim. 1:8,14.]
13Uliyoyasikia kwangu mimi, shikamana nayo! Kwani ni kielezo cha kujifundishia yale maneno yatupayo uzima, tukimtegemea Kristo Yesu na kumpenda![#1 Tim. 6:3; Tit. 2:1.]
14Hilo limbiko zuri sharti ulilinde kwa nguvu za Roho takatifu ikaayo ndani yetu sisi![#1 Tim. 6:20.]
15Neno lile nalijua, ya kuwa wote walioko Asia wameniacha; miongoni mwao wamo Figelo na Hermogene.[#2 Tim. 4:16.]
16Bwana awahurumie wao wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa kuwa amenipoza moyo mara nyingi; hakuwa na soni ya mafungo yangu,
17ila alipofika Roma akajipingia kunitafuta, mpaka akiniona.
18Bwana ampe kuona huruma kwake Bwana siku ile! Nayo yote, aliyonitimikia huko Efeso, wewe umeyatambua kuliko mimi.