The chat will start when you send the first message.
1Lakini tulipokwisha kuagana nao tukatweka na kukielekeza chombo kwenda Ko kwa tanga moja; tulipofika, kesho yake tukaenda hapo Rodo; toka hapo tukafika Patara.
2Tukaona chombo cha kuvukia hata Ufoniki, tukajipakia humo, tukatweka.
3Tulipokuona kule Kipuro tukakuacha kushotoni, tukaendelea mpaka Ushami, tukashukia Tiro; kwani ndiko, chombo kilikoagiziwa kuipakua mizigo yake.
4Tulipowaona wanafuanzi tukakaa lhuko siku saba. Nao wakamwambia Paulo kwa nguvu ya Roho, asipande kwenda Yerusalemu.[#Tume. 20:23; 21:11-12.]
5Lakini tulipoziishiliza siku zetu tukaondoka kwenda zetu; wakatusindikiza wote pamoja na wanawake na watoto mpaka weuni pa mji; hapo wakapiga magoti pwani, wakatuombea.[#Tume. 20:25.]
6Tukaagana nao, tukaingia chomboni, lakini wale wakarudi kwao.
7Nasi tulipokwisha kuimaliza safari ya baharini tukatoka Tiro, tukafika Putolemai, tukawaamkia ndugu, tukakaa kwao siku moja.
8Kesho yake tukaondoka, tukafika Kesaria, tukaingia nyumbani mwa mpiga mbiu njema Filipo aliyekuwa miongoni mwao wale saba, tukakaa kwake.[#Tume. 6:5; 8:40.]
9Mtu huyu alikuwa na wana wa kike wanne, walikuwa wasichana wenye kufumbua.[#Tume. 2:17.]
10Nasi tulipokaa siku nyingi kwake, pakashuka mfumbuaji toka Yudea, jina lake Agabo.[#Tume. 11:28.]
11Akatujia, akauchukua mshipi wa Paulo, akajifunga miguuni na mikono, akasema: Ndivyo, asemavyo Roho Mtakatifu: Mwenye mshipi huu Wayuda watamfunga Yerusalemu vivyo hivyo, wamtie mikononi mwa wamizimu.[#Tume. 20:23.]
12Tulipoyasikia haya sisi na wenyeji wa hapo tukambembeleza, asipande kwenda Yerusalemu.[#Mat. 16:22.]
13Ndipo, Paulo alipojibu: Huku kulia kwenu na kuniponda moyo kuna maana gani? Kwani mimi nimejielekeza siko kufungwa tu, ila hata kufa huko Yerusalemu kwa ajili ya Jina la Bwana Yesu.[#Tume. 20:24.]
14Alipokataa kutusikia, tukanyamaza tukisema: Bwana ayatakayo na yafanyike![#Mat. 26:39.]
15Siku hizi zilipopita, tukatengeneza yote, tukapanda kwenda Yerusalemu.
16Kulikuwa na wanafunzi Kesaria waliofuatana nasi, wakatupeleka kwa mtu aliyeitwa Mnasoni wa Kipuro aliyekuwa mwanafunzi wa kale, tufikie kwake.
17Tulipofika Yerusalemu, ndugu wakatupokea kwa furaha.[#Tume. 15:13; Gal. 1:19.]
18Kesho yake Paulo akaingia mwa Yakobo pamoja nasi, nao wazee wote walikuwamo.
19Akawaamkia, akawasimulia moja kwa moja mambo yote, Mungu aliyoyafanya kwa wamizimu kwa ile kazi yake, aliyoitumikia.
20Walipoyasikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia Paulo: Ndugu yetu, unaona, ya kuwa Wayuda walioanza kumtegemea Bwana ni elfu nyingi na nyingi, hao wote hujikaza kuyashika Maonyo.[#Tume. 15:1.]
21Lakini kwa ajili yako wewe wameambiwa ya kwamba: Unawafundisha Wayuda wote wanaokaa kwa wamizimu, wambeze Mose, ukiwaambia, wasiwatahiri watoto, wala wasiyafuate mambo yaliyo mazoezo tu.[#Tume. 16:3; Rom. 10:4.]
22Basi, iko nini inayofaa? Sharti kundi hilo zima likusanyike, kwani hawatakosa kusikia, ya kuwa umekuja.
23Kwa hiyo ufanye, tutakavyokuambia! Tunao waume wanne wenye jambo, waliloliagana na Mungu.
24Wachukue hao ujieue pamoja nao, uwalipie, wanyolewe vichwa! Hivyo wote watatambua, ya kuwa waliyoambiwa kwa ajili yako ni uwongo tu, ya kuwa wewe mwenyewe unaendelea na kuyashika Maonyo.[#Tume. 18:18; 4 Mose 6.]
25Lakini kwa ajili ya wamizimu walioanza kumtegemea Bwana tumewaandikia, tulivyopatana ya kwamba, waushike mzio wa nyama za tambiko na wa damu na wa nyamafu na wa ugoni.[#Tume. 15:20,29.]
26Ndipo, Paulo alipowachukua wale watu, kesho yake akaeuliwa pamoja nao, akapaingia Patakatifu, akatangaza, siku za weuo wao zitakapomalizika, kwamba ni hapo, kila mmoja atakapokwisha kutolewa kipaji cha weuo.[#4 Mose 6:9-20.]
27Siku zile saba ziliposalia kidogo kutimia, Wayuda walitoka Asia wakamwona Paulo hapo Patakatifu, wakalichanganya kundi lote la watu, wakamkamata kwa mikono yao,
28wakapiga kelele kwamba: Waume na Isiraeli, tusaidieni! Huyu ndiye yule mtu anayefundisha po pote watu wote, waubeze ukoo wetu nayo Maonyo, hata mahali hapa! Tena ameingiza Wagriki hapa Patakatifu, ndivyo, alivyopapatia uchafu mahali hapa Patakatifu.[#Tume. 6:13; Ez. 44:7.]
29Kwani kwanza walikuwa wamemwona mjini pamoja na Tirofimo wa Efeso, wakamwazia, ya kuwa Paulo amemwingiza napo Patakatifu.[#Tume. 20:4; 2 Tim. 4:20.]
30Mji wote ukatukutishwa, watu wote wakapakimbilia hapohapo, wakamkamata Paulo, wakamtoa hapo Patakatifu na kumburura; kisha milango yote ikafungwa papo hapo.
31Nao walipotaka kumwua, uvumi ulikuwa umemfikia mkuu wa kikosi cha askari, ya kuwa mji wote wa Yerusalemu umevurugika.
32Mara hiyo akachukua askari na wakubwa wao, akashuka kwao mbiombio. Wale walipomwona mkuu na askari, wakaacha kumpiga Paulo.
33Hapo, mkuu alipowafikia, akamshika, akaagiza, afungwe kwa minyororo miwili, akauliza: Nani huyu? Tena amefanya nini?[#Tume. 20:23; 21:11.]
34Lakini watu kwa hivyo, walivyokuwa wengi, wengine wakapiga kelele hivyo, wengine hivyo. Asipoweza kuyatambua yaliyo kweli kwa ajili ya makelele akaagiza, apelekwe bomani.
35Alipofika pa kupandia akachukuliwa na askari, wamkingie ukorofi wa watu;
36kwani watu wengi mno walimfuata wakipiga kelele kwamba: Mwondoe huyu![#Tume. 22:22; Luk. 23:18.]
37Walipotaka kumwingiza bomani, Paulo akamwambia mkuu wa askari: Niko na ruhusa kukuambia neno? Naye aliposema: Unajua Kigriki?
38Wewe si yule Mmisri aliyefanya kishindo siku hizi akichukua watu 4000 waliokuwa wauaji na kuwapeleka nyikani?
39Paulo akasema: Mimi ni mtu wa Kiyuda toka mji wa Tarso, ni mwenyeji wa mji huo wa Kilikia usio mdogo; nakuomba, nipe ruhusa ya kusema na watu.[#Tume. 9:11.]
40Alipompa ruhusa, Paulo akasimama juu hapo pa kupandia, akawapungia watu mkono; nao walipokuwa kimya kabisa, akasema nao Kiebureo, akawaambia: