The chat will start when you send the first message.
1Mambo yalipokatwa, kwamba tutweke kwenda Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine mikononi mwa bwana askari, jina lake Yulio aliyekuwa wa kikosi kilichomlinda mfalme aliye mkuu peke yake.[#Tume. 25:12.]
2Tukaingia chomboni kilichotoka Adaramiti, kilichotaka kwenda katika miji ya Asia, tukaondoka. Tukawa na Aristarko wa Tesalonike wa Makedonia.[#Tume. 19:29; 20:4.]
3Kesho yake tukafikia Sidoni; Yulio aliyemtunza Paulo kwa upole akampa ruhusa kwenda kwa rafiki zake, apate kugawiwa nao pamba za njiani.[#Tume. 24:23; 28:16.]
4Tulipotweka huko tukakielekeza chombo kwenda kandokando ya Kipuro, kwa sababu pepo zilitujia mbele.
5Tulipokwisha kuivuka bahari ya Kilikia na ya Pamfilia, tukafika Mira wa Likia.
6Huku bwana askari akaona chombo kilichotoka Alekisandria kwenda Italia, akatupakia mle.
7Lakini siku nyingi tukasumbuka sana kukiendesha kidogo tu, tupate kufika upande wa Kinido, kwani upepo ulituzuia. Tukapita kandokando ya Kreta upande wa Salmone.
8Hapo ikawa kazi kubwa kukielekeza chombo baharini, kisha tukafika mahali panapoitwa Matuo Mazuri, ni karibu ya mji wa Lasea.
9Hivyo siku zilizopita zikawa nyingi, tena kwenda baharini siku zile kukaponza watu wana, kwa sababu hata siku za kufunga zilikuwa zimepita. Paulo akawaonya[#3 Mose 16:29; 2 Kor. 11:25-26.]
10akiwaambia: Waume wenzangu, naona, ya kuwa mwendo wa sasa utakuwa wa maumivu, tena vitakavyopotea ni vingi, si mizigo tu na chombo, ila na sisi wenyewe.
11Lakini bwana askari akamsikiliza mwelekeze chombo na mwenye chombo, asiyafuate yaliyosemwa na Paulo.
12Kwa sababu kituo hakikufaa vema kukaa huko siku za kipupwe, walio wengi walitaka kabisa kuondoka huko, wajisumbuesumbue kukifikisha chombo Foniki, wakae huko siku za kipupwe, kwani ilikuwa bandari ya Kreta iliyokinga pepo za machweoni kwa jua upande wa kusini na wa kaskazini.
13Upepo wa kusini ulipoanza kuvuma, wakawaza, ya kuwa wamavipata, walivyovitaka, wakang'oa nanga, wakaendelea kandokando ya pwani pa Kreta.
14Lakini kitambo kidogo kilipopita, wakatokewa na upepo mkali wenye ngurumo unaoitwa kwao Mkweza Mawimbi.
15Chombo kikapokonywa nao, kisiweze kuushinda upepo huo na kuuelekea, kwa hiyo tukakiacha, kichukuliwe nao.
16Tukaenenda na kukimbizwa na upepo, tukafika kwenye kisiwa kidogo, jina lake Klauda, hapo tukakaza nguvu zote, tupate kuipandisha mashua; palisalia kidogo tu, tungeshindwa.
17Lakini walipokwisha kuipandisha wakaitumia, iwasaidie; wakaifunga chomboni na kuikinga, wakapitisha kamba hata chini. Tena woga ukawaingia wa kutumbukia panapoitwa Sirti, kwa hiyo wakalishusha tanga, chombo kikaendeshwa hivyo.
18Kesho yake upepo ukizidi kutuvumia kwa nguvu zote, wakatupa mizigo baharini.
19Siku ya tatu tukatupa kwa mikono yetu hata vitu vya chombo.
20Lakinia zilipokuwa siku nyingi, lisituonekee wala jua wala nyota, upepo ukikaza vivyo hivyo, basi, mwisho hakuwako tena mwenye moyo wa kwamba: Tutaokoka.
21Walipoacha kula vyakula siku nyingi, ndipo, Paulo alipoinuka katikati yao, akasema: Waume wenzangu, kama mngalilifuata neno langu, mkaacha kuondoka huko Kreta, hatungaliyapata maumivu na mapotevu haya.
22Lakini na sasa nawaonya, mtulie mioyo; kwani miongoni mwenu ninyi hamna atakayeangamia hata mmoja, kisipokuwa chombo hiki tu.
23Kwani malaika wa Mungu wangu, ninayemtumikia, amesimama usiku huu hapo, nilipo,
24akasema: Usiogope, Paulo, wewe sharti usimame mbele ya Kaisari! Tena tazama, Mungu amekupa wote waliomo humu chomboni pamoja nawe.[#Tume. 23:11.]
25Kwa hiyo tulieni mioyo, waume wenzangu! Kwani namtegemea Mungu, ya kwamba: Itakuwapo vivyo hivyo, kama nilivyoambiwa.
26Lakini sharti tupwelewe kisiwani kulikokuwa kote.[#Tume. 28:1.]
27Usiku wa kumi na nne ulipofika, nasi tulipotupwa huko na huko katika bahari ya Adiria, usiku wa manene wabaharia wakawaza kwamba: Nchi iko karibu.
28Walipokishusha kipimo, wakapaona, pana mikono 60. Walipoendelea kidogo, wakakishusha kipimo tena, wakapaona, pana mikono 45.
29Tukaogopa, tusitupwe mahali penye miamba, kwa hiyo wakatia nanga nne za nyuma, wakangoja, kuche.
30Lakini wabaharia walitaka kukimbia na kukiacha chombo. Kwa hiyo wakaishusha mashua baharini, wakasema: Twataka kuzitia hata nanga za mbele.
31Ndipo, Paulo alipomwambia bwana askari nao askari wenyewe: Hawa wasipokaa humu chomboni, ninyi hamtaweza kuokoka.
32Ndipo, askari walipozikata kamba za masha, wakaiacha, ianguke baharini.
33Kulipopambazuka, Paulo akawabembeleza wote, wale chakula, akisema: Leo ni siku ya kumi na nne, mkikaa kwa kungoja na kufunga; hakuna kitu cho chote, mlichokitia vinywani.[#Tume. 27:27.]
34Kwa hiyo nawabembeleza, mle chakula, kwani hiki kitaufalia wokovu wenu. Kwani kwenu hakuna hata mmoja atakayeangamiza hata unywele mmoja tu wa kichwani.[#Mat. 10:30.]
35Naye alipokwisha kuyasema haya, akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega, akaanza kula.[#Yoh. 6:11; 1 Tim. 4:4.]
36Ndipo, wote walipotulia mioyo, wakala chakula nao.
37Nasi sote tuliokuwa humo chomboni wote pamoja tulikuwa watu 276.
38Waliposhiba vyakula wakaupunguza uzito wa chomboni wakitupa ngano baharini.
39Kulipokucha, hawakuitambua nchi. Lakini walipoona kituo penye ufuko, wakataka kukiingiza chombo huko, ikiwezekana.
40Wakazikata kamba za nanga, wakaziacha baharini; hapohapo wakazilegeza nazo kamba zilizofunga sukani, wakatweka tanga dogo na kulielekezea upepo, wakaufuata ufuko.
41Lakini tulitupwa funguni, chombo kikakwama mbele, kikachimba mchangani, kikashikwa kabisa, kisitukutike hata kidogo, lakini nyuma kikavunjwa kwa nguvu ya mawimbi.
42Askari walipotaka kuwaua wafungwa, maana mtu asipate kukimbia kwa kuogelea,
43bwana askari alitaka kumwokoa Paulo, akawazuia, wasivifanye, walivyovitaka; kisha akawaagiza wanaojua kuogelea, wajitupe wa kwanza baharini, wafike pwani.
44Waliosalia waliambiwa, wajiokoe na kutumia mbao au miti minginemingine ya chomboni. Hivyo wote wakapata kuokoka na kufika salama penye nchi kavu.[#Tume. 27:22-25.]