Amosi 5

Amosi 5

Ombolezo

1Lisikieni neno hili, ninalowatolea mimi!

Ni ombolezo la kuwaombolezea ninyi mlio mlango wa Isiraeli:

2Ameanguka, hatainuka tena mwanamwali wa Isiraeli,

amebwagwa, alale juu ya nchi yake, hakuna atakayemwinua.

3Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema:

Mji unaopeleka elfu vitani utasaza mia tu,

nao unaopeleka mia utasaza kumi tu kwao walio mlango wa Isiraeli.

4Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyowaambia walio mlango wa

Isiraeli:

Nitafuteni! Ndipo, mtakapopona.

5Lakini msinitafute huko Beteli! Wala msije kuingia

Gilgali!

Wala msiondoke kwenda Beri-Seba!

Kwani Gilgali utatekwa na kuhamishwa,

nao Beteli utageuka kuwa si kitu.

6Mtafuteni Bwana! Ndipo, mtakapopona.

Asiujie mlango wa Yosefu kama moto utakaouteketeza,

kwa kuwa Beteli hakuna atakayeweza kuuzima.

7Mashauri yapasayo mnayageuza kuwa uchungu,

nayo yaongokayo mnayakanyaga uvumbini.

8Yeye ndiye aliyezifanya nyota,

zile za Kilimia nazo zake Choma, nikuchome!

Yeye ndiye anayeigeuza giza kuwa mapema,

tena mwanga wa mchana huugeuza kuwa giza ya usiku!

Yeye ndiye anayeyaita maji ya bahari,

akayafurikisha juu ya nchi! Bwana ni Jina lake.

9Yeye ndiye anayewaletea wanguvu mwangamizo, uwatokee kama umeme,

nayo miji yenye maboma ya nguvu iingiliwe na mwangamizo.

10Wao humchukia ayakataye mashauri ya langoni sawasawa,

naye asemaye ya kweli huwachafua mioyo.

11Kwa kuwa mnamkanyaga mnyonge, mkamtoza kodi ya ngano,

mmepata kujijengea nyumba za mawe ya kuchonga,

lakini hamtakaa ndani yao;

mkajipandia mashamba mazuri ya mizabibu,

lakini hamtazinywa mvinyo zao.

12Kwani ninayajua mapotovu yenu yaliyo mengi

nayo makosa yenu yanayozidi.

Mnamsonga aliye mwongofu mkitaka kupenyezewa,

mkawapotoa maskini, wasishinde shaurini.

13Kwa hiyo aliye mwenye akili hunyamaza siku hizi,

kwani siku hizi ni mbaya kweli.

14Yatafuteni yaliyo mema mkiyaacha yaliyo mabaya, mpate kupona!

Ndipo, Bwana Mungu Mwenye vikosi atakapokuwa nanyi,

kama mlivyosema wenyewe.

15Yachukieni yaliyo mabaya! Yapendeni yaliyo mema!

Simamisheni langoni mashauri yaliyo sawa!

Ndipo, Bwana Mungu Mwenye vikosi atakapowahurumia

walio masao yake Yosefu.

16Kweli Bwana Mungu Mwenye vikosi, yeye Bwana anasema hivi:

Katika viwanja vyote yatakuwako maombolezo,

napo barabarani po pote watalia kwamba: Hoi! Hoi!

Mkulima watamwita shambani, aje kuingia matanga,

nao wajuao maombolezo watawaita, waje kuwalilia.

17Katika mashamba yote ya mizabibu yatakuwako

maombolezo,

kwani nitapita kwako katikati;

ndivyo, Bwana anavyosema.

18Yatawapata wanaoitamani siku ya Bwana!

Ninyi siku ya Bwana itawafaliaje? Ndiyo giza, siyo

mwanga.

19Itakuwa, kama mtu akimkimbia simba, akaja kukutana na

chui,

au kama mtu akiingia nyumbani, akauegemeza mkono wake

ukutani,

kisha akatokea nyoka, akamwuma.

20Je? Siku ya Bwana siyo giza? Ndio, haina mwanga;

ni yenye weusi, hauangazi kabisa.

Mungu hataki matambiko yasiyotoka mioyoni.

21nimechukizwa na sikukuu zenu, sizitaki;

wala mnuko wa mikutano yenu ya kunitambikia usinijie!

22Ingawa mnitolee ng'ombe za kuteketezwa nzima

pamoja na vipaji vyenu vya tambiko, sitapendezwa,

wala vinono vyenu vya kunishukuru sitavitazama.

23Iondoe kwangu milio ya nyimbo zako!

Nazo sauti za mapango yako sitaki kuzisikia.

24Lakini mashauri yaliyo sawa na yaendelee kama maji,

nayo yaongokayo na yawe kama mto usiokupwa!

25Je? Ng'ombe na vipaji, mlivyovitoa nyikani miaka

arobaini,

vilikuwa vya kunitambikia mimi, ninyi mlio mlango wa

Isiraeli?

26Kwa kuwa mlimchukua Sikuti, awe mfalme wenu,

navyo vinyua vyenu vya Kiyuni, mlivyojifanyizia wenyewe,

viwe nyota zake mungu wenu:

27basi, kwa hiyo nitawahimisha, mwende mbali kuliko

Damasko.

Ndivyo, Bwana anavyosema; Mungu Mwenye vikosi ni Jina

lake.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania