The chat will start when you send the first message.
1Atakapoinuka katikati yako mfumbuaji au mwota ndoto na kukutolea kielekezo au kioja,
2nacho hicho kielekezo au kioja, alichokuambia, kitakapotimia, ndipo, atakapokuambia: Twende, tufuate miungu mingine, msiyoijua, tuitumikie!
3Lakini usiyasikie maneno ya mfumbuaji huyo au ya mwota ndoto huyo! Kwani Bwana Mungu wenu atawajaribu tu, ajue, kama ninyi mnampenda Bwana Mungu wenu kwa mioyo yenu yote na kwa roho zenu zote.
4Mfuateni Bwana Mungu wenu na kumcha, myashike maagizo yake na kuisikia sauti yake, mmtumikie na kugandamana naye!
5Lakini yule mfumbuaji au yule mwota ndoto sharti auawe, kwa kuwa amesema, mmwache Bwana Mungu wenu aliyewatoa ninyi katika nchi ya Misri na kuwakomboa nyumbani, mlimokuwa watumwa; naye yule alitaka kukudanganya, uondoke katika hiyo njia, Bwana Mungu wako aliyokuagiza kuishika. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako![#5 Mose 18:20; 1 Kor. 5:9,13.]
6Itakuwa, ndugu yako aliyezaliwa na mama yako au mwanao wa kiume au wa kike au mkeo anayekaa kfuani pako au mwenzako, unayempenda, kama unavyojipenda mwenyewe, akuhimize penye njama kwamba: Twende, tutumikie miungu mingine, usiyoijua wewe, wasiyoijua nao baba zako!
7Nayo ndiyo iliyomo miongoni mwa miungu ya makabila yanayoaa na kuwazunguka ninyi pande zote, wengine wao wanakukalia karibu, wengine mbali toka mwanzo wa nchi hata mwisho wake.
8Basi itakapokuwa hivyo, usimwitikie, wala usimsikie, jicho lako lisimwonee machungu, usimhurumie, wala usimfiche,
9ila mwue kabisa! Mkono wako sharti uwe wa kwanza wa kumua, kisha mikono yao watu wote na ifuate.[#5 Mose 17:7.]
10Sharti umpige mawe, hata afe! Kwani alijaribu kukudanganya, umwache Bwana Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri nyumbani ulimokuwa mtumwa.
11Nao Waisiraeli wote watakapovisikia wataogopa, wasiendelee kufanya kwako mabaya kama nayo.
12Itakuwa, upate habari ya mmojawapo katika miji yako, Bwana Mungu wako atakayokupa ya kukaa humo, kwamba:
13Wako watu wasiofaa waliotoka katikati yako, waliowadanganya wenyeji wa miji yao kwamba: Twende, tutumikie miungu mingine, msiyoijua!
14Basi, utakapovisikia, sharti utafute na kuchunguza na kuuliza vema; kisha utakapoona, ya kama neno hili ni la kweli, ikaelekea, ya kama tapisho hilo limefanyika kweli katikati yako,
15huna budi kuwapiga wenyeji wa mji huo kwa ukali wa upanga na kuutia huo mji pamoja nayo yote yaliyomo mwiko wa kuwapo, nao nyama wao wa kufuga sharti uwaue kwa ukali wa upanga.[#4 Mose 21:2.]
16Kisha na uyakusanye mateka yote katikati ya uwanja wake, uuteketeze huo mji kwa moto pamoja na amteka yake yote kuwa ng'ombe ya tambiko ya Bwana Mungu wako ya kuteketezwa yote nzima, uwe chungu ya majivu kale na kale, usijengwe tena.
17Katika vile vyote vilivyotiwa mwiko wa kuwapo kisioneke cho chote kitakachogandamana na mkono wako, Bwana ayatulize tena makali yake yaliyowaka moto, akuonee machungu, akuhurumie na kukufanya kuwa wengi, kama alivyowaapia baba zako.[#Yos. 7.]
18haya yatakuwa, utakapoisikia sauti ya Bwana Mungu wako na kuyaangalia maagizo yake yote, mimi ninayokuagiza leo, uyafanye yanyokayo machoni pake Bwana Mungu wako.