The chat will start when you send the first message.
1Miaka saba itakapopita, mwachiliane madeni![#2 Mose 23:10-11.]
2Nalo jambo hili la kuachaliana madeni liwe hivyo: kila mkopeshaji aliyemkopesha mwenziwe asimwendee kumdai huyo mwenziwe au ndugu yake, kwani maachilio ya Bwana yametangazwa.
3Asiye wa Kiisiraeli utaweza kumwendea, umtoze, lakini aliye ndugu yako utamwachilia.
4Kweli kwako asingekuwako mkopaji, kwani Bwana atakubariki sana katika hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa, uichukue, iwe fungu lako mwenyewe,
5kama wewe ungeisikia tu sauti ya Bwana Mungu wako, uyaangalie na kuyafanya hayo maagizo yote, mimi ninayokuagiza leo.
6Kwani Bwana Mungu wako atakubariki, kama alivyokuambia. Kwa hiyo utaweza kukopesha mataifa mengi, lakini mwenyewe hutakopa; hivyo utatawala mataifa mengi, lakini wewe hawatakutawala.[#5 Mose 28:12.]
7Itakapokuwa, ndugu yako mmoja aliopo malangoni pako pawapo pote katika nchi yako, Bwana Mungu wako atakayokupa, akose mali, usiushupaze moyo wako, wala usiufunge mkono wako ukimnyima ndugu yako anayetaka kukukopa.[#1 Yoh. 3:17.]
8Ila umfungulie mkono wako na kumkopesha yatoshayo kuukomesha ukosefu wake, alioukosa.[#Luk. 6:34-35.]
9Jiangalie sana, moyoni mwako lisiingie shauri lisilofaa kabisa la kwamba: Mwaka wa saba, ndio mwaka wa kuachilia madeni, uko karibu, ukamtazama ndugu yako anayetaka kukukopa kwa macho yenye ubaya wa kumnyima; hili kosa litakukalia hapo, atakapomlilia Bwana kwa ajili yako.
10Kwa hiyo sharti ujihimize kumpa, wala moyo wako usiwe mbaya kwa kumpa; kwani kwa jambo kama hili Bwana Mungu wako atakubarikia matendo yako yote na mapato yote ya mikono yako.
11Kwani wenye kukosa mali hawatakoma katika nchi hii; kwa sababu hii mini ninakuagiza kwamba: Ndugu yako aliye mnyonge na mkosa mali kwako katika nchi yako umfungulie mkono wako kabisa![#Mat. 26:11; Yes. 58:7; Yak. 2:15-16.]
12Ndugu yako mume au mke wa Kiebureo akijiuza kwako, akakutumikia miaka sita, sharti umwache katika mwaka wa saba, atoke kwako kuwa mwungwana tena.[#2 Mose 21:2.]
13Tena ukimwacha, atoke kwako kuwa mwungwana tena, usimwache, ajiendee mikono mitupu!
14Ila umgawie mali kwenda nazo, ukitoa mbuzi na kondoo na mapato ya purio lako, nayo ya kamulio lako. Kwa hivyo, Bwana Mungu wako alivyokubariki, umgawie naye.
15Ukumbuke, ya kama ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, naye Bwana Mungu wako akakukomboa. Kwa sababu hii mimi ninakuagiza leo neno hili.[#5 Mose 5:15.]
16Lakini atakapokuambia: Sitaki kutoka kwako, kwani ninakupenda wewe nao waliomo nyumbani mwako, kwa kuwa ninaona mema kwako,
17basi, uchukue shazia, ulitoboe sikio lake nalo, kisha umpigilie hivyo mlangoni; ndipo, atakapokuwa mtumwa wako kale na kale. Hata kijakazi utamfanyizia vivyo hivyo.[#2 Mose 21:6.]
18Usiyawazie kuwa magumu kumwacha, aondoke kwako kuwa mwungwana tena, kwani atakuwa amekutumikia miaka sita na kufanya kazi za watu wawili wa mshahara, naye Bwana Mungu wako atakubarikia yote, utakayoyafanya.
19Wana wote wa kwanza watakaozaliwa, wao wa ng'ombe wako na wa mbuzi na wa kondoo wako, kama ni wa kiume, sharti uwatakase kuwa wake Bwana Mungu wako, usimtumie kazini mwana wa kwanza wa ng'ombe wako, wala usimkate manyoya mwana wa kwanza wa kondoo wako.[#2 Mose 13:2.]
20Ila utamla mbele ya Bwana Mungu wako, wewe pamoja nao waliomo nyumbani mwako, mwaka kwa mwaka mahali pale, Bwana atakapopachagua.[#5 Mose 14:23.]
21Lakini akiwa mwenye kilema, kama ni kiwete au kipofu au mwenye kilema kibaya cho chote, usimchinjie Bwana Mungu wako,[#3 Mose 22:20.]
22ila utamla malangoni pako, mwenye uchafu na mwenye kutakata pamoja, kama unavyokula paa au kulungu.[#5 Mose 12:15.]
23Damu yake tu usiile, ila uimwage mchangani kama maji.[#3 Mose 3:17; 5 Mose 12:16,23-24.]