The chat will start when you send the first message.
1Uangalie mwezi wa Abibu, ule sikukuu ya Pasaka ya Bwana Mungu wako! Kwani ulikuwa mwezi wa Abibu, Bwana Mungu wako alipokutoa huko Misri na usiku.[#2 Mose 12.]
2Ndipo umchinjie Bwana Mungu wako kondoo ya Pasaka, ndio ng'ombe na mbuzi na kondoo, mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake.
3Sikukuu hiyo usile cho chote kilichochachwa, ila siku zake saba sharti ule mikate isiyochachwa kuwa mikate ya matesoni, kwa kuwa ulitoka upesiupesi na kiwogawoga katika nchi ya Misri, upate kuikumbuka siku hiyo ya kutoka katika nchi ya Misri siku zote za maisha yako.
4Siku hizo saba isionekane chachu katika mikate yako, wala nyama za yule kondoo, utakayemchinja siku ya kwanza jioni, zisilale usiku huo hata asubuhi.
5Huwezi kuichinja kondoo ya Pasaka malangoni pako miongoni mwa miji, Bwana Mungu wako atakayokupa.
6Ila mahali pale tu, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, ndipo, utakapoichinja kondoo ya Pasaka jioni, jua likiisha kuchwa, ndio saa zilezile zilizokuwa, ulipotoka Misri.
7Napo mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua, ndipo, utakapoipika na kuila palepale; kisha asubuhi yake na ugeuke nyuma kwenda hemani kwako.
8Siku sita sharti ule mikate isiyochachwa, nayo siku ya saba na mkutanie kumheshimu Bwana Mungu wenu; hapo msifanye kazi yo yote.
9Jihesabie majuma saba! Watu wakianza kukata ngano kwa miundu, ndipo uanzie kuyahesabu hayo majuma saba.
10Kisha na ule sikukuu ya Majuma ya Bwana Mungu wako, mkono wako ukimtolea vipaji kwa furaha ya moyo ya kuvifurahia hivyo, Bwwana Mungu wako alivyokubariki.
11Ndipo, mtakapofurahi mbele ya Bwana mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, wewe na mwanao wa kiume na wa kike na mtumishi wako wa kiume na wa kike, naye Mlawi aliopo malangoni pako, nao wageni, nao waliofiwa na wazazi, nao wajane walioko kwako.[#2 Mose 20:24; 5 Mose 16:16.]
12Nawe ukumbuke, ya kama ulikuwa mtumwa kule Misri! Kwa hiyo angalia, uyafanye haya maongozi!
13Sikukuu ya Vibanda utaila siku saba utakapokwisha kuyakusanya yatokayo purioni pako na kamulioni pako.
14Hiyo sikukuu yako mtaifurahia, wewe na mwanao wa kiume na wa kike na mtumishi wako wa kike na wa kiume, naye Mlawi, nao wageni, nao waliofiwa na wazazi nao wajane waliopo malangoni pako.[#5 Mose 16:11; 26:11.]
15Siku saba utaila hiyo sikukuu ya Bwana Mungu wako mahali pale, Bwana atakapopachagua. Kwani Bwana Mungu wako atakubarikia mapato yako yote, nazo kazi zote za mikono yako, kwa hiyo utaweza kuwa mwenye furaha.
16Kila mwaka mara tatu watu wako wote walio wa kiume sharti watokee mbele ya Bwana Mungu wako mahali pale, atakapopachagua: penye sikukuu ya Mikate isiyochachwa na penye sikukuu ya Majuma na penye sikukuu ya Vibanda, lakini wasitokee mbele ya Bwana mikono mitupu!
17Kila mtu ashike mkononi mwake vipaji vya kuishuuru mbaraka, Bwana Mungu wako aliyokupatia.
18Jiwekee waamuzi na wenye amri malangoni pako pote, Bwana Mungu wako atakapokupa wewe kuwa pao mashina yako, wawaamue watu maamuzi yaongokayo.[#4 Mose 11:16; 5 Mose 20:8-9.]
19Usipotoe mashauri, wala usipendelee uso wa mtu, wala usitwae mapenyezo, kwani mapenyezo huyapofusha nayo macho yao werevu wa kweli, tena huyapotoa maneno ya waongofu.[#2 Mose 23:8; 5 Mose 1:17.]
20Jihimize kuyafuata yaongokayo kweli, upate kukaa uzimani na kuichukua hiyo nchi, iwe yako, Bwana Mungu wako atakayokupa.
21Usijipandie miti yo yote ya Ashera kandokando ya mahali pa kumtambikia Bwana Mungu wako, utakapojitengenezea.[#5 Mose 7:5.]
22Wala usijisimamishie nguzo za mawe za kutambikia, kwani Bwana Mungu wako anazichukia.[#3 Mose 26:1.]