The chat will start when you send the first message.
1Hii ndiyo mbaraka, Mose, yule mtu wa Mungu, aliyowabariki wana wa Isiraeli kabla ya kufa kwake,[#1 Mose 49; Yuda 14.]
2akasema:
Bwana alitoka Sinai, akakuchelea kama jua toka Seiri, akautokeza mwanga wake toka mlimani kwa Parani, akaja na kutoka katikati yao maelfu kumi ya watakatifu, kuumeni kwake ukawaka moto uliowatokezea Maonyo.
3Kweli anayapenda makabila ya watu, watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; nao walipokaa miguuni pako, kila mmoja akapokea neno lake lililompasa.
4Mose akatuagiza Maonyo, yawe fungu lao mkutano wa Yakobo,
5akawa mfalme kwake Yeshuruni, vichwa vyao hao watu walipokusanyika kwake pamoja nao wale walio mashina ya Isiraeli.[#2 Mose 15:18; 19:7-8; Yes. 44:2.]
6Rubeni na awepo uzimani, asife, ijapo watu wake wahesabike.
7Nayo hii ni mbaraka ya Yuda, akasema: Bwana, uisikie sauti ya Yuda! Umwingize kwao walio ukoo wake! Kwani mikono yake itakapowapigia vita, nawe msaidie kuwashinda wapingani wake!
8Naye Lawi akamwambia: Mwanga wako na Kweli yako ni yao watu wako wamchao Mungu, uliowajaribu kule Masa na kuwagombeza kwenye Maji ya Magomvi.[#2 Mose 28:30; 17; 4 Mose 20.]
9Ndio wanaowaambia baba zao na mama zao: Hatukuwaona, nao ndugu zao hawawatazami, wala wana wao hawawajui, kwani huliangalia Neno lako, hulishika Agano lako.[#2 Mose 32:26-29; Mat. 10:37.]
10Wao na wawafundishe Wayakobo maamuzi yako, nao Waisiraeli Maonyo yako, tena na wavukize mavukizo, yapate kuingia puani mwako, wakitoa ng'ombe nzima za tambiko pako pa kukutambikia.
11Bwana, zibariki nguvu zao nazo kazi za mikono yao, zikupendeze! Wapingani na wachukivu uwavunje viuno, wasiwainukie tena!
12Benyamini akamwambia: Mpendwa wa Bwana na akae kwake na kutulia! Bwana humfunika mchana kutwa na kukaa kati ya mabega yake.
13Naye Yosefu akamwambia: Nchi yako na iwe imebarikiwa naye Bwana, akiipatia kipaji kizuri cha mbinguni, ndio umande, nayo maji mengi yakaayo ndani ya nchi.
14Na aipatie nacho kipaji kizuri cha mazao, jua linayoyaivisha, nacho kipaji kizuri cha matunda ya kila mwezi!
15Na aipatie nayo yatokayo juu ya milima iliyo ya zamani, nacho kipaji kizuri cha vilima vilivyo vya kale na kale!
16Navyo vipaji vizuri vya nchi, navyo vijaavyo ndani yake! Upendeleo wake akaaye porini na ukijie kichwa chake Yosefu, juu ya utosi wake yeye aliyewekwa kwa kutengwa na ndugu zake![#1 Mose 49:26; 2 Mose 3:2.]
17Mwanawe wa kwanza ni dume la ng'ombe lenye utukufu, kama pembe za nyati zilivyo, ndivyo, zilivyo nazo pembe zake; atakapozitumia atawakumba makabila ya watu, waanguke chini wote pia walioko huku hata mapeoni kwa nchi, kwani ndivyo, walivyo makumi ya maelfu ya Efuraimu, tena ndivyo, walivyo nayo maelfu ya Manase.
18Naye Zebuluni akamwambia: Zebuluni, zifurahie safari zako za baharini, nawe Isakari, yafurahie mahema yako!
19Wataalika makabila ya watu kuja mlimani; ndiko, watakakochinja ng'ombe za tambiko zilizo za kweli, kwani mafuriko ya bahari yatawanyonyesha, mpaka washibe, nazo zile mali nyingi zilizofichika mafukoni zitakuwa zao.
20Naye Gadi akamwambia: Atukuzwe aliyempatia Gadi nchi iliyo pana! Huota kama jike la simba, apate kurarua mikono na vichwa.
21Alipoiona nchi ya kwanza, ikawa yake, kwani huko aliwekewa kazi ya mwongozi. Lakini naye akaja kwao waliokuwa vichwa vya watu hawa, akaishindisha haki ya Bwana na kuyatimiza mashauri yake akiwa pamoja nao hao Waisiraeli.[#4 Mose 32.]
22Naye Dani akamwambia: Dani ni mwana mchanga wa simba, hushambulia na kutoka Basani.
23Nafutali akamwambia: Nafutali atashiba yampendezayo, azidishiwe mbaraka ya Bwana; chukua nchi ya baharini na ya kusini, iwe yako!
24Naye Aseri akamwambia: Aseri ndiye katika hawa wana atakayepata mbaraka zaidi, tena atakuwa mpendwa wao ndugu zake, nao mguu wake atauchovya katika mafuta;
25makomeo yake yatakuwa ya chuma na ya shaba, nazo nguvu zako ziwe zizo hizo siku zote, utakazokuwapo.
26Mungu wake Yeshuruni, hakuna wa kufanana naye, ndiye anayepita juu mbinguni, akusaidie, namo mawinguni, auonyeshe utukufu wake.[#Yes. 44:2.]
27Yeye Mungu wa kale ni kimbilio, chini yako imekunjuliwa mikono iliyo ya kale na kale. Atawafukuza adui mbele yako akikuambia: Angamiza tu!
28Kwa hiyo Waisiraeli watakaa na kutulia vema, watakuwa pake yao kwenye chemchemi yake Yakobo katika nchi yenye ngano na mvinyo mbichi, nazo mbingu zake zitadondoa umande.[#4 Mose 23:9.]
29Mwenye shangwe ni wewe, Isiraeli! Yuko nani aliyeokolewa na Bwana kama wewe? Yeye ni ngao inayokusaidia, tena ni upanga unaokupatia utukufu. Kwa hiyo adui zako watakunyenyekea, lakini wewe utatembea na kuvikanyaga vilima vyao.[#5 Mose 4:7-8; Sh. 33:12; 144:15.]