The chat will start when you send the first message.
1Kisha Mose akatoka kwenye mbuga za Moabu, akaupanda mlima wa Nebo ulio mrefu zaidi kuliko milima mingine ya Pisiga, unaoelekea Yeriko. Huko Bwana akamwonyesha nchi yote ya Gileadi mpaka nchi ya Dani,[#5 Mose 3:27.]
2nayo nchi yote ya Nafutali, nayo nchi ya Efuraimu, nayo ya Manase, nayo nchi yote nzima ya Yuda mpaka kwenye bahari ya machweoni kwa jua,
3nayo nchi ya kusini, nayo nchi ya tambarare ya bondeni karibu ya Yeriko, ule mji wenye mitende, mpaka Soari.
4Kisha Bwana akamwambia: Hii ndiyo nchi, niliyomwapia Aburahamu na Isaka na Yakobo kwamba: Nchi hii nitawapa wao wa uzao wako. Basi, nimekuonyesha, uione kwa macho yako, lakini hutavuka kuiingia.[#1 Mose 12:7.]
5Kisha Mose, mtumishi wa Bwana, akafa huko katika nchi ya Moabu, kwa kuwa Bwana aliviagiza hivyo.[#5 Mose 32:50.]
6Akamzika huko katika bonde la nchi ya Moabu kulikoelekea Beti-Peori, lakini hakuna mtu anayelijua kaburi lake mpaka siku hii ya leo.[#Yuda 9.]
7Mose alikuwa mwenye miaka 120 alipokufa, macho yake yalikuwa hayakufifia, nazo nguvu zake za mwilini zilikuwa hazikupunguka.
8Wana wa Isiraeli wakamwombolezea Mose siku 30 katika mbuga za Moabu, hata siku za maombolezo ya matanga ya Mose zikatimia.[#4 Mose 20:29.]
9Naye Yosua, mwana wa Nuni, alikuwa amejazwa roho ya werevu wa kweli, kwa kuwa Mose alimbandikia mikono yake. Kwa hiyo wana wa Isiraeli wakamsikia, wakafanya, kama Bwana alivyomwagiza Mose.[#4 Mose 27:18.]
10Kwao Waisiraeli hakuinuka tena mfumbuaji kama Mose, Bwana aliyejuana naye uso kwa uso,[#2 Mose 33:11; 4 Mose 12:6-8.]
11wala hakuna aliyefanana naye kwa kufanya vielekezo na vioja vyote, Bwana alivyomtuma katika nchi ya Misri kumfanyizia Farao nao watumishi wake wote na wenyeji wote wa nchi yake,
12wala hakuna aliyefanana naye kwa kufanya matendo yote ya nguvu za mikono yake wala kwa yale makuu yote ya kustusha, Mose aliyoyafanya machoni pao Waisiraeli wote.