The chat will start when you send the first message.
1Sikiliza, Isiraeli! Unataka leo kuuvuka Yordani, uingie huko kuchukua nchi ya mataifa yenye watu wengi walio na nguvu kuliko wewe, nayo miji ni mikubwa yenye maboma yanayofika hata mbinguni.[#5 Mose 1:28.]
2Wako nao wana wa Anaki walio watu wengi na warefu, wewe nawe unawajua, ukasikia mwenyewe, watu wakisema: Yuko nani atakayesimama mbele ya wana wa Anaki?[#2 Mose 13:22.]
3Kwa hiyo ujue leo hivi, ya kama Bwana Mungu wako ndiye atakayekutangulia kuvuka kuwa moto ulao, awaangamize na kuwaangusha chini mbele yako, upate kuwafukuza na kuwatowesha upesi, kama Bwana alivyokuambia.[#5 Mose 4:24.]
4Bwana Mungu wako atakapowakimbiza mbele yako, usiseme moyoni mwako kwamba: Ni kwa ajili ya wongofu wetu, Bwana akituleta huku, tuichukue nchi hii, iwe yetu. Kwani ni kwa ajili ya uovu wao hao wamizimu, Bwana akiwafukuza mbele yako.[#5 Mose 8:17; 1 Mose 15:16.]
5Si kwa wongofu wako wala kwa unyofu wa moyo wako, wewe ukiingia kwao kuichukua nchi yao, iwe yako, ila kwa ajili ya uovu wao hao wamizimu Bwana Mungu wako amewafukuza mbele yako, alishikize lile neno, alilowaapia baba zako Aburahamu na Isaka na Yakobo.
6Kwa hiyo jua, ya kuwa si kwa ajili ya wongofu wako, Bwana Mungu wako akikupa nchi hiyo njema kuichukua, iwe yako. Kwani ninyi m watu wenye kosi ngumu.[#2 Mose 32:9.]
7Kumbuka, usisahau, ulivyomkasirisha Bwana Mungu wako nyikani! Tangu siku ile, ulipotoka katika nchi ya Misri, mpaka mlipofika mahali hapa, mlikuwa mkikataa kumtii Bwana.
8Nako kule Horebu mlimkasirisha Bwana, Bwana akawatolea makali yake alipotaka kuwaangamiza.[#2 Mose 32.]
9Ilikuwa hapo, nilipopanda mlimani kuzichukua zile mbao za mawe zilizokuwa mbao za Agano, Bwana alilolifanya nanyi. Nami nikakaa mlimani siku 40 mchana kutwa na usiku kucha, sikula chakula, wala sikunywa maji.
10Ndipo, Bwana aliponipa mbao mbili za mawe zilizoandikwa kwa kidole cha Mungu maneno yote sawasawa, kama Bwana alivyoyasema nanyi huko mlimani toka motoni siku ile, mlipokusanyika.
11Zile siku 40 za mchana kutwa na usiku kucha zilipokwisha, Bwana akanipa zile mbao mbili za mawe, ndio mbao za Agano.
12Kisha Bwana akaniambia: Ondoka, ushuke upesi, kwani walio ukoo wako, uliowatoa Misri, wamefanya vibaya, wameondoka upesi katika hiyo njia, niliyowaagiza, wakajitengenezea kinyago cha kuyeyushwa.
13Tena Bwana akaniambia kwamba: Nilipowatazama watu hawa, nikawaona kuwa watu wenye kosi ngumu.
14Niache, niwaangamize na kulifuta jina lao, litoweke chini ya mbingu! Kisha nitakufanya wewe kuwa taifa lenye nguvu, tena lenye watu wengi kuliko wao.
15Ndipo, nilipogeuka na kushuka mlimani, nao mlima ulikuwa ukiwaka moto, nazo hizo mbao mbili za Agano zilikuwa katika mikono yangu miwili.
16Nilipotazama niliona, ya kuwa mlimkosea Bwana Mungu wenu kwa kujifanyia kinyago cha ndama kilichoyeyushwa; ndivyo, mlivyoondoka upesi katika hiyo njia, Bwana aliyowaagiza.
17Ndipo, nilipozikamata zile mbao mbili, nikazitupa, zitoke katika mikono yangu miwili, nikazivunja hivyo machoni penu.
18Nikamwangukia Bwana kama ile mara ya kwanza siku 40 mchana kutwa na usiku kucha, sikula chakula, wala sikunywa maji kwa ajili ya makosa yenu yote, mliyoyakosa na kufanya yaliyokuwa mabaya machoni pake Bwana, yaliyomkasirisha.[#2 Mose 34:28; 5 Mose 10:10.]
19Kwani niliyaogopa makali na machafuko ya Bwana kwa hivyo, alivyowakasirikia akitaka kuwaangamiza ninyi; lakini Bwana akanisikia hata mara hiyo.[#Ebr. 12:21.]
20Naye Haroni Bwana akamkasirikia sana, akataka kumwangamiza naye; lakini nikambembeleza siku hiyo hata kwa ajili yake Haroni.
21Kisha nikaichukua ile ndama, mliyoitengeneza kwa ukosaji wenu, nikaiteketeza kwa moto nilipokwisha kuikatakata na kuiponda kabisa, mpaka ikawa vumbi tupu; kisha nikayatupa hayo mavumbi yake katika kijito kilichoshuka mlimani.
22Nako Tabera na Masa na kwenye Makaburi ya Uchu mkamkasirisha Bwana,[#2 Mose 17:7; 4 Mose 11:3,34.]
23alipowaagiza kutoka Kadesi-Barnea akisema: Pandeni, mwichukue hiyo nchi, nitakayowapa, mkakataa kukitii kinywa cha Bwana Mungu wenu, maana hamkumtegemea, wala hamkuisikia sauti yake.[#4 Mose 13:2,31; 5 Mose 14:1-4.]
24Mlikuwa wenye kukataa kumtii Bwana tangu siku hiyo, ninapowajua ninyi.[#5 Mose 9:7.]
25Hapo, nilipokuwa nimemwangukia Bwana hizo siku 40 mchana kutwa na usiku kucha, nilizolala chini, kwa kuwa Bwana alitaka kuwaangamiza ninyi,[#5 Mose 9:18.]
26nikambembeleza Bwana kwamba: Bwana Mungu wangu, usiwaangamize walio ukoo wako, uliojipatia kuwa wako na kuwakomboa kwa ukuu wako ulipowatoa Misri kwa mkono wako wenye nguvu.
27Wakumbuke watumishi wako Aburahamu na Isaka na Yakobo, usiungalie ugumu wa watu hawa, wala uovu wao, wala ukosaji wao,
28watu wa nchi hiyo, ulikotutoa, wasiseme: Bwana hakuweza kuwaingiza katika nchi ile, aliyowaagia, ila aliwatoa tu kwa kuwachukia, apate kuwaua nyikani.[#4 Mose 14:16.]
29Nao ni ukoo wako, uliojipatia kuwa wako mwenyewe ulipowatoa kwa nguvu zako kuu na kwa kuukunjua mkono wako.