The chat will start when you send the first message.
1Mimi Paulo niliye mtume wa Kristo Yesu kwa hayo, Mungu ayatakayo, nawaandikia ninyi watakatifu mlioko Efeso, nanyi mliomtegemea Kristo Yesu:[#Rom. 1:7; 1 Kor. 1:2.]
2Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo!
3*Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetugawia mema yote ya kiroho yatokayo mbinguni kwake Kristo![#Ef. 2:6.]
4Kwani ulimwengu ulipokuwa haujaumbwa bado, alituchagua sisi kuwa wake yeye, tuwe watakatifu machoni pake pasipo kilema.[#Ef. 5:27; Yoh. 15:16; Rom. 8:28-30.]
5Kwa hivyo, anavyotupenda, alitutenga kale, tupokelewe kuwa wana wake mwenyewe tukimfuata Yesu Kristo; ndiyo yaliyompendeza, akayataka, yawepo.[#Yoh. 1:12.]
6Nasi huusifu utukufu wa kipaji chake, alichotugawia hapo, alipomtoa mpendwa wake.[#Mat. 3:17.]
7Katika damu yake yeye ndimo, tupatiamo ukombozi, maana twaondolewa makosa; hayo ndiyo magawio yake mengi[#Ef. 2:7; 3:8,16; Kol. 1:14.]
8yaliyotuongezea nasi werevu wote ulio wa kweli, hata ujuzi wote.
9Kisha akatutambulisha, ayatakayo, yaliyokuwa yamefichwa. Ndivyo, ylivyompendeza, akayaweka kale moyoni mwake,[#Ef. 3:3-6,9; Rom. 16:25; Kol. 1:26-27.]
10yatengenezeke, siku alizoziweka zitakapotimia, Kristo awe kichwa chao yote yaliyoko mbinguni nacho chao yaliyoko nchini.[#Gal. 4:4.]
11Yeye ndiye, ambaye tulipatiwa naye urithi wetu, tuliokatiwa kale na kuwekewa kale, maana yeye huyafanya yote, yawepo, kama ayatakavyo mwenyewe.[#Rom. 8:28; Kol. 1:12.]
12Kwa hiyo sisi tuliotangulia kumngojea Kristo ndio tutakaousifu utukufu wake.
13Nanyi mmelisikia Neno la kweli, ni ule Utume mwema wa wokovu wenu; napo hapo, mlipolitegemea, mlitiwa muhuri yake mlipompata Roho Mtakatifu, tuliyeagiwa.[#Ef. 4:30.]
14Huyu ni rehani ya urithi wetu, tujue: tumekombolewa, tu watu wake, utukufu wake upate wenye kuusifu.*[#2 Kor. 1:22; 5:5.]
15*Kwa hiyo mimi niliposikia, mnavyomtegemea Bwana Yesu, tena mnavyowapenda watakatifu wote,[#Kol. 1:4.]
16sichoki kushukuru kwa ajili yenu kila, niwakumbukapo nikiomba.
17Nawaombea, Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye utukufu, awape roho ya werevu wa kweli na ya ufunuzi, mmtambue yeye alivyo.
18Namo mioyoni mwenu atiemo macho yaliyoangazwa, mpate kujua, kilivyo hicho kingojeo, mlichoitiwa naye, tena mwujue nao utukufu wa urithi wake, aliowawekea watakatifu, ulivyo mwingi.
19Mpate kuujua nao uwezo wake, unavyokua kuupita wote mwingine ulioko; huo akatupa sisi tumtegemeao kwa kuhimizwa na nguvu zake kuu.
20Ndizo, alizozitumia alipomfufua Kristo katika wafu na kumketisha kuumeni kwake mbinguni[#Sh. 110:1.]
21na kumpa cheo kuupita ukubwa na ufalme na uwezo na ubwana wote na kuyapita majina yo yote yatakayotajwa siku hizi, nazo siku zote zitakazokuja.[#Rom. 8:38-39; Kol. 2:10.]
22Akayaweka yote kuwa chini migguni pake, naye mwenyewe akamfanya kuwa mkuu peke yake, awe kichwa chao wateule wote,[#Ef. 4:15; Sh. 8:7; Mat. 28:18.]
23maana wao ni mwili wake; huu ndio utimilifu wake yeye anayeyatimiza yote pia kwao wote po pote pasipo kusaza.*[#Ef. 4:10; Rom. 12:5; 1 Kor. 12:27.]