Waefeso 2

Waefeso 2

Wokovu ni gawio tu.

1Nanyi mlikuwa mmekufa kwa ajili ya maanguko na makosa yenu,[#Luk. 15:24; Kol. 2:13.]

2mliyoendelea nayo kale kwa desturi za watu walio wa ulimwengu huu tu; ndivyo, mwenye kuzitawala nguvu za angani atakavyo, ni yule pepo anayetenda nguvu hata sasa mwao waliokataa kutii.[#Ef. 6:12; Yoh. 12:31; Tit. 3:3.]

3Nasi sote kale tulikuwa wenzao tulipoendelea na kuzifuata tamaa za miili yetu na kuyafanya, miili na mioyo yetu iliyoyataka, nasi kwa hivyo, tulivyokuwa hapo, tulikuwa wana waliomkasirisha kama wale wengine.[#Kol. 3:6.]

4*Lakini Mungu alikuwa ametulimbikia huruma kwa kuwa na upendo mwingi wa kutupenda;

5kwa sababu hiyo akaturudisha uzimani pamoja na Kristo hapo, tulipokuwa tumekufa kwa ajili ya maanguko; hivyo wokovu wenu ni gawio tu.[#Luk. 15:24,32.]

6Alipokwisha kutufufua pamoja naye akatukalisha mbinguni pake Kristo Yesu.[#Rom. 8:10; Fil. 3:20.]

7Maana siku zitakazokuja anataka kuonyesha, magawio yake yanavyokuwa mengi, yasipimike akituendea kwa utu tu katika Kristo Yesu.[#Ef. 1:7.]

8Kwani wokovu wenu ni gawio tu, mlilopewa kwa ajili ya kumtegemea, nako hakukutoka mwenu, maana nako ni kipaji chake Mungu,[#Gal. 2:16.]

9nacho hamkukipata kwa kazi zenu, mtu asipate kujivuna.[#1 Kor. 1:29.]

10Kwani sisi tu kazi yake yeye, namo mwake Kristo Yesu ndimo, tulimoumbiwa, tufanye matendo mema, Mungu aliyotutengenezea kale, tuyafuate.*[#Tit. 2:14.]

Hatu wageni, ila wenyeji.

11Kwa hiyo yakumbukeni: kale mlikuwa wamizimu kwa hivyo, miili yenu ilivyo; mkaitwa mapumbavu nao wale waliojiita makungwi, kwa sababu walikuwa wametahiriwa na mikono ya watu miilini mwao.[#Ef. 5:8.]

12Kumbukeni: siku zile mlikuwa hamnaye Kristo, tena mlikuwa mmekatazwa kuwa wenyeji kwao Waisiraeli, mkawa wageni, msiyajue maagano, waliyoagiwa kuyapata. Mlikuwa hamnacho kingojeo, wala hamnaye Mungu huku ulimwenguni.[#Rom. 9:4.]

13Lakini sasa kwa kuwa wake Kristo Yesu nanyi mliokuwa kale mbali mmeletwa na damu ya Kristo, mfike karibu.[#Sh. 119:155.]

14Kwani yeye ni utengemano wetu, maana yale makundi mawili aliyageuza kuwa moja, akiuvunja ukingo uliotutenga, tuchukizane.[#Yes. 9:6; Gal. 3:28.]

15Ilikuwa hapo, alipoyatangua mwilini mwake yale maonyo na maagizo yaliyokuwa ya miiko tu. Akataka kuwaumba hao wote wawili kuwa mtu mmoja mpya aliye wake yeye; kwa hiyo aliwapatanisha,[#2 Kor. 5:17; Kol. 2:14.]

16akawa kole yao wote wawili alipomlipa Mungu madeni yao yeye mmoja mwilini mwake, alipowambwa msalabani; huko ndiko, alikoyaua yale machukivu.

17Kisha akaja kuipiga hiyo mbiu njema ya utengemano kwenu ninyi mliokuwa mbali, nako kwao waliokuwa karibu.[#Yes. 57:19; Zak. 9:10.]

18Kwani kwake yeye sote wawili tumepata njia ya kumfikia Baba, tukiwa wenye Roho moja.[#Ef. 3:12.]

19*Kwa hiyo sasa ham wageni tena, wala wenye kukaa kando, ila m wenyeji pamoja nao watakatifu, tena m wa nyumbani mwake Mungu.[#Ef. 3:6; Ebr. 12:22-23.]

20Mmejengwa juu ya msingi wao mitume na wafumbuaji, ambao Kristo Yesu ni jiwe lake la pembeni.[#Yes. 28:16; Mat. 16:18; 1 Petr. 2:4-6.]

21Kwa nguvu yake yeye jengo lote linaunganishwa, lipate kukua, mpaka liwe nyumba takatifu, Bwana alimo.

22Humu nanyi mnajengwa pamoja na wengine, mwe kao lake Mungu la Kiroho.*[#1 Petr. 2:5.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania