The chat will start when you send the first message.
1Hayo yamenipeleka mimi Paulo kifungoni kuwa mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi wamizimu.[#Fil. 1:7,13.]
2Labda mmesikia, Mungu alivyonipa utunzaji wa magawio yake, niwagawie nanyi.[#Ef. 1:9-10; Gal. 1:12.]
3Nilifumbuliwa, niyatambue yale yaliyofichwa tangu kale, kama nilivyowaandikia kidogo hapo kwanza.
4Mkiyasoma mwaweza kuuona ujuzi wangu wa fumbo la Kristo.
5Siku zilizopita zote wana wa watu hawajatambulishwa fumbo hilo, ambalo mitume na wafumbuaji wake watakatifu walifunuliwa sasa na Roho,[#Kol. 1:26.]
6hilo la kwamba: Wamizimu nao ndio wenye urithi pamoja nasi, kwamba: Nao wamo pamoja nasi mwilini mwake, kwamba: Nao ni wenye kiagio, tulichopewa katika Kristo Yesu tulipotangaziwa Utume mwema.[#Ef. 2:13,18-19; Tume. 15:7-9.]
7Ndio, niutumikiao nami kwa hivyo, Mungu alivyonigawia kipaji changu, nilichopewa hapo, niliposhindwa na nguvu zake.[#Tume. 9:15.]
8Mimi niliye mdogo kuliko watakatifu wote nikapewa gawio hili, niwapigie wamizimu mbiu njema ya mema yote ya Kristo yaliyo mengi, yasiwezekane kupelelezeka yote;[#Ef. 1:7; 1 Kor. 15:9-10; Gal. 1:16.]
9kisha niueleze vema utunzaji wa lile fumbo lililokuwa limefichwa tangu zamani zote kwake Mungu aliyeviumba vyote.
10Maana siku hizi sharti wakubwa na wanguvu wote walioko mbinguni watambulishwe na wateule, ujuzi wake Mungu ulivyo mwingi sana.[#Rom. 11:32-33; 1 Petr. 1:12.]
11Mwenyewe aliviweka hivyo kale kabisa moyoni mwake, vitimie katika Kristo Yesu, Bwana wetu;[#Ef. 1:11.]
12kisha akatuongoza njia ya kumwendea pasipo woga wowote, mpaka tumfikie tukiwa tumejishikizia kwake yeye kwa kumtegemea.[#Yoh. 14:6; Rom. 5:1-2; Ebr. 4:16.]
13Kwa hiyo naomba, msichoke kwa ajili ya maumivu yangu, niliyopatwa nayo kwa ajili yenu, maana yanawapatia utukufu.[#Kol. 1:24.]
14Kwa sababu hii nampigia Baba na Bwana wetu Yesu Kristo magoti;
15kwani kila aliye baba, kama yuko mbinguni au yuko nchini, hujiita na jina hili la baba.
16Nawaombea, kwa wingi wa utukufu wake awape, mtu wenu wa ndani apate nguvu akikuzwa na Roho wake.[#Ef. 1:7; 6:10.]
17Tena awape, Kristo akae mioyoni mwenu kwa hivyo, mnavyomtegemea, mpate kushusha mizizi katika upendo, mshikizwe nayo![#Yoh. 14:23; Kol. 2:7.]
18Kisha awape, mweze kupima pamoja na watakatifu wote, upendo ulivyo mpana na mrefu, tena unavyoingia chini, hata unavyokwenda juu;
19ndivyo, mtakavyoutambua upendo wake Kristo, ya kuwa unaupita utambuzi wote, mpate kuujaa katika mambo yote, kama Mungu alivyoujaa.
20Lakini yeye kwa hivyo, nguvu yake inavyokaza mwetu, anaweza kufanya kuyapita yote, tuyaombayo nayo tuyawazayo,
21yeye atukuzwe kwao wateule walio wake Kristo Yesu siku zote zitakazokuwapo kale na kale pasipo mwisho! Amin.*