The chat will start when you send the first message.
1*Mimi niliyefungwa kwa ajili ya Bwana nawaonya ninyi, mfanye mwenendo unaopatana na wito, mlioitiwa.[#Kol. 1:10.]
2Mwe wenye unyenyekevu wote na upole na uvumilivu, mvumiliane mkipendana![#Kol. 3:12.]
3Kwa hivyo, Roho alivyowageuza kuwa mmoja, mjikaze kujiunga kwa mapatano!
4Mwili ni mmoja, nayo Roho ni moja, nacho kingojeo cha wito wenu, mlichoitiwa, ni kimoja.[#Rom. 12:5; 1 Kor. 12:4-6.]
5Bwana ni mmoja, nalo tegemeo ni moja, nao ubatizo ni mmoja,[#Yoh. 10:16; 1 Kor. 8:6.]
6naye Mungu ni mmoja, ndiye Baba yao wote, ni mwenye kuwatawala wote, ni mwenye kuwaendesha wote, ni mwenye kuwakalia wote.*[#1 Kor. 12:6.]
7Lakini sote tumegawiwa kipaji, kila mmoja chake yeye, kama Kristo alivyompimia cha kumpa.[#Rom. 12:3,6; 1 Kor. 12:11.]
8Kwa hiyo yamesemwa:
Alipopaa juu aliteka mateka, akawapa watu vipaji.
9Basi, neno hili: “alipaa” ni kwambaje isipokuwa kwamba: Alishuka kwanza kwenda pande za kuzimuni kwa nchi?[#Yoh. 3:13.]
10Aliyeshuka ndiye yule yule aliyepaa kuzipita mbingu zote, apate kuyatimiza yote.
11*Naye akawapa wengine kuwa mitume, wengine wafumbuaji, wengine wapiga mbiu njema, wengine wachungaji na wafunzi,[#Tume. 21:8; 1 Kor. 12:28.]
12maana watakatifu watengenezwe, wajue kuzifanya kazi za utumishi; ndizo kazi za kuujenga mwili wake Kristo,[#1 Petr. 2:5.]
13mpaka sisi sote tutakapofikia kuwa mmoja wa kumtegemea na wa kumtambua Mwana wa Mungu; huko ndiko kukua kwenyewe na kuutimiza umri unaoweza kuutambua wingi wote wa vipaji vya Kristo.
14Hivyo hatutakuwa tena wachanga wanaochukuliwa kama mawimbi na kupelekwa huko na huko na mafunzo ya watu yanayogeukageuka kama upepo, maana ni ya uwongo na ya udanganyi wa watu wanaotaka kutupoteza kwa werevu mbaya.[#1 Kor. 14:20; Ebr. 13:9.]
15Ila tutakuwa wenye kupendana kweli, katika mambo yote tumkalie yeye Kristo aliye kichwa chetu.[#Ef. 1:22; 5:23; Kol. 1:18.]
16Naye ndiye mwenye kuunganisha mwili wote, ukishikamizwa na mafundo yote yanayoutia nguvu, kila fundo moja, kama lilivyopimiwa kazi yake; hivyo mwili hukua, ukijengwa kuwa mzuri kwa kupendana.*[#Kol. 2:19.]
17Neno hili sasa nalisema na kumtaja Bwana, awe shahidi wangu: Msiendelee tena, kama wamizimu nao wanavyoendelea na kufuata mambo wasiyoyajua maana![#Rom. 1:21-24.]
18Mawazo yao yameguiwa na giza, uzima wa Mungu ukawa kitu kigeni kwao kwa ajili ya ujinga, walio nao, na kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao.[#Ef. 2:12.]
19Hivyo, walivyokufa ganzi la mioyo, wakajitia katika uasherati, wakayafanya machafu yote wakijipatiamo mali.
20Lakini ninyi hamkufundishwa mambo ya Kristo kuwa hivyo.
21Kwani mmesikia, mkafundishwa Neno lake kwamba: Iliyo ya kweli imo mwake Yesu.
22*Kwa hivyo, mlivyoendelea kale, mvueni mtu wa kale aliyejiponza kwa kuzifuata tamaa za udanganyifu![#Rom. 8:13; Gal. 6:8; Kol. 3:9.]
23Kisha mawazo ya mioyo yenu yarudishiwe upya wa Kiroho,[#Rom. 12:2.]
24mmvae mtu mpya aliyeumbwa kuwa wa Kimungu mwenye wongofu na utakatifu wa kweli![#1 Mose 1:26.]
25Kwa hiyo uvueni uwongo, mwambiane yaliyo ya kweli kila mtu na mwenzake! Kwani tu viungo, kila mmoja kiungo cha mwenzake.[#Zak. 8:16.]
26Mioyo inapojaa makali, msikose! Jua lisiwachwee, mkingali na makali yenu,[#Sh. 4:5; Yak. 1:19,20.]
27wala msimpe Msengenyaji mahali pa kukaa mwenu![#1 Tes. 4:11.]
28Aliyekwiba asiibe tena! Ila sharti ajisumbue na kufanya kazi kwa mikono yake mwenyewe, ajipatie mema, naye aone ya kumgawia mwenye kuyakosa!
29Maneno yo yote yaliyo maovu yasitoke vinywani mwenu! Ila kama liko neno zuri lifaalo la kujenga palipojenguka lisemeni, liwapendeze wenye kulisikia![#Ef. 5:4; Kol. 3:16-17; 4:6.]
30Msimsikitishe Roho Mtakatifu wa Mungu! Kwani ndiye, mliyepewa kuwa muhuri yenu ya siku ya ukombozi.[#Ef. 1:13-14; Yes. 63:10.]
31Uchungu wo wote na mifundo ya mioyo na makali na mateto na matusi na yaondoke kwenu pamoja na uovu wote![#Kol. 3:8.]
32Mwendeane kwa utu na kwa upole, mkiacha kulipishana, kama Mungu naye alivyoacha kuwalipisha ninyi kwa kuwa wake Kristo!*[#Mat. 6:14; 18:22-35; Kol. 3:12-13.]