The chat will start when you send the first message.
1Mwigeni Mungu, kama inavyowapasa watoto wapendwa![#Mat. 5:48.]
2Tena mwendeane na kupendana, kama Kristo alivyowapenda ninyi! Akajitoa kwa ajili yetu sisi kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuuawa, Mungu asikie mnuko mzuri.[#Ef. 5:25; Gal. 2:20; Ebr. 10.]
3Lakini mambo ya ugoni na ya uchafu wo wote na ya choyo yasitajwe kwenu kamwe, kama inavyowapasa watakatifu;
4wala matusi wala mapuzi wala mafyozi mabaya, maana siyo yafaayo; yafaayo ni ya kushukuru.
5Kwani haya yajueni na kuyatambua vema: hakuna mgoni wala mchafu wala mwenye choyo aliye mtambikia vinyago atakayepata fungu katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.
6Pasioneke mwenye kuwadanganya na maneno yasiyo na maana! Kwani kwa ajili yao makali ya Mungu huwajia wakataao kutii.
7Kwa hiyo msichanganyike nao!
8Kwani kale mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa mwanga kwa kuwa naye Bwana. Mwendelee, kama iwapasavyo wana wa mwanga![#Ef. 2:11,13; 1 Petr. 2:9.]
9Kwani matunda yanayozaliwa mwangani ndio wema wo wote na wongofu na ukweli.*[#Mat. 5:16; Luk. 16:8; Yoh. 12:36.]
10Pambanueni, kama ni mambo gani yampendezayo Bwana![#Ef. 5:17; Rom. 12:2.]
11Msiwe wenzao wenye kuzifanya kazi za giza zisizofaa, ila mkaze kuwaumbua!
12Kwani hutia soni kuyataja tu yanayofanywa nao na kuyafichaficha.[#Rom. 1:24.]
13Lakini yote hufunuliwa yakiumbuliwa na mwanga, kwani kila kitu kinachofunuliwa huangazika.[#Yoh. 3:20-21.]
14Kwa hiyo husema:
Amka, wewe uliyelala!
Inuka, utoke kwenye wafu!
Kisha Kristo atakuangaza.
15*Kwa hiyo angalieni sana, mtakavyoendelea! Msiwe wenye ujinga, ila mwe wenye werevu wa kweli![#Mat. 10:16; Kol. 4:5.]
16Mzitumie vema siku za sasa! Kwani siku hizi ndizo mbaya.
17Kwa hiyo msipumbae, ila mjijulishe, Bwana ayatakayo![#Ef. 5:10.]
18Wala msilewe pombe! Kwani hazikomeki tena! Ila mjijaze Roho![#Luk. 21:34.]
19Mwongeleane na kuambiana shangwe na nyimbo na tenzi za Kiroho, mkimwimbia Bwana na kumshangilia mioyoni mwenu,[#Sh. 33:2-3; Kol. 3:16.]
20mkamshukuru Mungu Baba po pote kwa ajili yao yote, mliyoyapata katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo!
21Kisha na mnyenyekeane kila mtu na mwenziwe kwa hivyo, mnavyomwogopa Kristo!*[#1 Petr. 5:5.]
22Ninyi wanawake, watiini waume wenu, kama mnavyomtii Bwana![#1 Mose 3:16; Kol. 3:18; 1 Petr. 3:1.]
23Kwani mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo alivyo kichwa chao wateule, maana yeye ndiye aliyeuokoa mwili.
24Lakini kama wateule wanavyomtii Kristo, vivyo hivyo nao wake sharti wawatii waume wao katika mambo yote![#1 Kor. 11:3.]
25Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyowapenda wateule, akajitoa mwenyewe kwa ajili yao,[#Kol. 3:19.]
26awatakase na kuwang'aza akiwaosha maji, kama alivyoagana nao.[#Tit. 3:5.]
27Ndivyo, alivyotaka kujitengenezea mwenyewe wateule wenye tukuzo hilo la kwamba: Hawanalo doa wala kunjo wala lo lote lifananalo nayo yaliyo hivyo, maana ndio watakatifu pasipo kilema.[#Sh. 45:14; 2 Kor. 11:2.]
28Ndivyo, inavyowapasa nao waume kuwapenda wake zao, kama ni miili yao. Kwani mwenye kumpenda mkewe hujipenda mwenyewe.
29Kwani toka kale hakuna mtu ye yote aliyeuchukia mwili wake mwenyewe, ila huulea na kuutunza, kama Kristo naye anavyowafanyia wateule;
30kwani sisi tu viungo vya mwili wake.[#Ef. 1:23; 1 Mose 2:23; 1 Kor. 6:15.]
31Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake,
agandamiane na mkewe, nao hao wawili watakuwa mwili mmoja.
32Fumbo hili ni gumu la kulifumbua, lakini mimi nasema la Kristo na la wateule!
33Lakini hata ninyi kila mmoja wenu na ampende mkewe, kama anavyojipenda mwenyewe! Lakini mke amche mumewe!