The chat will start when you send the first message.
1Kisha akatengeneza kwa mbao za migunga meza ya kuteketezea ng'ome za tambiko; urefu wake ulikuwa mikono mitano, nao upana wake ulikuwa mikono mitano, pande zote nne zilikuwa sawa; nao urefu wake wa kwenda juu ulikuwa mikono mitatu.
2Penye pembe zake nne akatengeneza pembe zilizoipasa, nazo hizo pembe zake zilikuwa za mti uo huo mmoja; kisha akaifunikiza shaba.
3Akatengeneza navyo vyombo vyote vya meza ya kutambikia: nyungu na majembe na vyano na nyuma na sinia; vyombo vyake vyote akavitengeneza kwa shaba.
4Kisha akaitengenezea meza ya kutambikia kikingio kilichofanana na wavu wa shaba, akauweka chini ya ukingo wake kuelekea chini, ufike mpaka katikati ya meza ya kutambikia.
5Kisha akatengeneza mapete manne kwa kuyeyusha shaba, akayatia katika hizo pembe nne za wavu wa shaba ya kutilia mipiko.
6Kisha akatengeneza mipiko ya migunga, akaifunikiza shaba.
7Hiyo mipiko akaitia katika hayo mapete yaliyokuwa pande mbili penye meza ya kutambikia, itumike ya kuichukulia. Hivyo meza ya kutambikia aliitengeneza kwa mbao, iwe yenye mvungu ndani ulio wazi.
8Kisha akatengeneza birika la shaba pamoja na wekeo lake la shaba, akitumia vioo vya shaba vya wanawake waliotumika hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano.[#2 Mose 30:18-21.]
(9-20: 2 Mose 27:9-19.)9Kisha akatengeneza ua upande wa kusini ulio wa juani; nguo za ua huo akazitengeneza kwa bafta ngumu, urefu wao ulikuwa mikono mia.
10Nguzo zao ishirini zilikuwa zenye miguu ishirini ya shaba, lakini vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu vilikuwa vya fedha.
11Hata upande wa kaskazini ulikuwa vivyo hivyo: nguo zilikuwa zenye urefu wa mikono mia, nazo nguzo zao ishirini zilikuwa zenye miguu ishirini ya shaba, lakini vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu vilikuwa vya fedha.
12Nao upande wa ua unaoelekea baharini ulikuwa wenye nguo za mikono hamsini, nazo nguzo zake zilikuwa kumi zenye miguu kumi, navyo vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu vilikuwa vya fedha.
13Nao upande wa maawioni kwa jua ulikuwa mikono hamsini.
14Nguo ya upande wa huku ilikuwa ya mikono kumi na mitano, nazo nguzo zake zilikuwa tatu zenye miguu mitatu.
15Nao upande wa huko nguo yake ilikuwa ya mikono kumi na mitano, maana hapo pa kuuingilia ua ulikuwa upande wa huku na upande wa huko, nazo nguzo zake zilikuwa tatu zenye miguu mitatu.
16Nguo zote za kuuzunguka ua zilikuwa za bafta ngumu.
17Miguu ya nguzo ilikuwa ya shaba, lakini vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu vilikuwa vya fedha, navyo vichwa vyao walivifunikiza fedha, nazo nguzo zote za ua zilikuwa zimeungwa kwa vijiti vya fedha.
18Hapo penye lango la ua palikuwa na pazia lililokuwa kazi ya fundi wa kufuma kwa nyuzi za rangi, nalo lilitengenezwa kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu, urefu ulikuwa mikono ishirini, nao upana wa kwenda juu ulikuwa mikono mitano, sawasawa kama nguo nyingine za ua.
19Nguzo zake nne pamoja na miguu yake minne zilikuwa za shaba, lakini vifungo vyao vilikuwa vya fedha, navyo vichwa vyao viliuwa vimefunikizwa fedha, navyo vijiti vyao vya kuziungia juu vilikuwa vya fedha.
20Lakini mambo zote za Kao lenyewe na za ua kuuzunguka wote zilikuwa za shaba.
21Hii ndio hesabu ya mali za kulitengeneza hilo Kao lililokuwa Kao la Ushahidi, nazo zilihesabiwa kwa agizo la Mose; walioifanya kazi hii ndio Walawi, nao waliangaliwa na Itamari, mwana wa mtambikaji Haroni.[#4 Mose 4:28.]
22Besaleli, mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa shina la Yuda, alifanya yote, kama Bwana alivyomwagiza Mose.[#2 Mose 31:1-11.]
23Pamoja naye alifanya kazi Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa shila la Dani; naye alikuwa fundi wa kuchora na wa kuvumbua kazi nzuri za ufundi na wa kufuma kwa nyuzi za rangi za nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na za bafta ngumu.
24Dhahabu zote zilizotumika za kufanya kazi zote za kupatengeneza Patakatifu, zilikuwa dhahabu zilizotolewa kuwa vipaji vya tambiko vya kupitishwa motoni, nazo zilikuwa jumla talanta 29 na sekeli 730, pamoja ndio frasila 80 zikipimwa kwa mizani ya patakatifu.[#2 Mose 30:13.]
25Nazo fedha zilizotolewa na mkutano kwa kukaguliwa zilikuwa jumla talanta 100 na sekeli 1775, pamoja ndio frasila 244 zikipimwa kwa izani ya Patakatifu.
26Kila kichwa walilipa beka moja, ndio nusu ya fedha au shilingi mbili kwa kipimo cha fedha cha Patakatifu; ndivyo, kila mmoja alivyolipa alipofika kukaguliwa kuwa ni mwenye miaka ishirini na zaidi, nao walikuwa watu 603550.
27Zile talanta 100 za fedha zilitumika za kuitengeneza miguu ya Patakatifu na miguu ya pazia kwa kuziyeyusha, miguu 100 kwa talanta 100, talanta moja ya mguu mmoja.
28Nazo zile sekeli 1775 zilitumika za kuvitengeneza vifungo vya nguzo na za kuvifunikiza vichwa vyao na za vijiti vya kuziungia juu.
29Nazo shaba vipaji vyake vya tambiko vya kupitishwa motoni vilikuwa talanta 70 na sekeli 2400, pamoja ndio frasila 230.
30Hizi zilitumika za kutengeneza miguu ya hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano na meza ya shaba ya kutambikia na wavu wa shaba uliotiwa kwake na vyombo vyote vya meza ya kutambikia,
31nayo miguu ya pande zote za uani na miguu ya langoni penye ua na mambo zote za Kao lenyewe na mambo za pande zote za uani.