Ezekieli 15

Ezekieli 15

Mti wa mzabibu usiofaa.

1Neno la Bwana likanijia la kwamba:[#Yer. 2:21.]

2Mwana wa mtu, mti wa mzabibu unaipita miti yote kwa nini? Au liko, tawi lake linalolipata likikaa kwenye miti ya mwituni?

3Je? Huchukuliwa mti wake wa kutumiwa kwa kazi yo yote? Au watu huuchukua, wautumie kuwa mambo tu ya kutungikia vyombo vyao?

4Mtauona, nikiutoa kuwa kuni za moto; moto ukiisha kuzila pande zake mbili za mwisho, nacho kipande cha katikati kikiungua, Je? Iko kazi, utakayotumikia?[#Yoh. 15:6.]

5Tazameni! Ungaliko mzima bado hautumiwi kwa kazi yo yote; sembuse moto ukiisha kuula na kuunguza, hautatumiwa kabisa kwa kazi yo yote.

6Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kama mti wa mzabibu ulioko kwenye miti ya mwituni nilivyoutoa kuwa kuni za moto tu, ndivyo, nitakavyowatoa wakaao Yerusalemu.

7Nitawakazia macho yangu: ijapo wametoka motoni, moto ndio utakaowala; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapowakazia macho yangu.

8Nayo nchi hii nitaigeuza kuwa peke yake tu, kwa kuwa wamevunja maagano; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania