Ezekieli 24

Ezekieli 24

Mafumbo ya maangamizo ya Yerusalemu.

1Neno la Bwana likanijia katika mwaka wa 9 katika mwezi wa kumi siku yake ya kumi kwamba:[#2 Fal. 25:1; Yer. 52:4.]

2Mwana wa mtu, jiandikie jina lake siku hii siku hiihii ya leo! Kwani mfalme wa Babeli ameufikia Yerusalemu siku hii ya leo.

3Nao mlango huu mkatavu uutungie fumbo ukiwaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Iteleke nyungu! Ndiyo, iteleke! Kisha itie nayo maji!

4Tena vikusanye vipande vyake vya kutia ndani, vyote viwe vipande vizuri tu vya paja na vya mkono, ijaze mifupa iliyochaguliwa!

5Chukua kondoo tu waliochaguliwa kwa uzuri! Tena chini yake hiyo nyungu patupie mifupa, iwe chungu! Zitokose kabisa nyama, nayo mifupa iliyomo sharti ichemke sana.

6Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Yatakupata, wewe mji wenye hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Yatakupata, wewe mji wenye damu, u nyungu yenye kutu, nayo kutu yake inakataa kuondoka kwake! Zitoe zile nyama kipande kwa kipande, msizipigie kura![#Ez. 24:9.]

7Kwani damu zilizomwagwa mwake zimo bado, ni hapohapo penye mwamba ulio wazi, alipozimiminia, hakuzimwaga penye mchanga, zikafunikwa kwa mavumbi.

8Kusudi ziyainue makali yangu yenye moto ya kulipiza lipizi, kwa hiyo nimeacha, azimiminie hizo damu penye mwamba ulio wai, zisifunikwe.

9Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Yatakupata, wewe mji wenye damu, nami nitaupangia chungu kubwa la kuni.[#Nah. 3:1.]

10Lete kuni nyingi, uwashe moto! Zitokose nyama kabisa na kuziunga kwa viungo! Mifupa na iungue!

11Nyungu ikiwa tupu, iweke penye makaa yake ya moto, chuma chake kipate moto kabisa, mpaka kiungue, taka zake zilizomo ziyeyuke, kutu nayo iondoke kabisa.

12Lakini ni kujisumbua bure, kutu haitoki kwake kwa kuwa kutu ni nyingi, namo motoni hiyo kutu yake inakaa.

13Ni kwa ajili ya uchafu wako wa uzinzi; kwa kuwa nilitaka kukutakasa, ukakataa kutakata uchafu wako ukikutoka, kwa hiyo hutatakata tena, mpaka niyatimize kwako makali yangu yenye moto.[#Ez. 5:13.]

14Mimi Bwana nimeyasema, kwa hiyo yatakuja nitakayoyafanya. Sitachoka, wala sitakuonea uchungu, nikuhurumie; kwa hivyo, njia zako zilivyo, tena kwa hivyo, nayo matendo yako yalivyo, watakuhukumu; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.

15Neno la Bwana likanijia la kwamba:

16Mwana wa mtu, tazama, ayapendezaye macho yako nitamchukua kwako kwa mara moja nikimpiga; nawe usimwombolezee, wala usimlilie, machozi yasikutoke machoni![#Ez. 24:18.]

17Piga kite usiposikiwa; lakini aliyekufa usimfanyizie matanga! jifunge kilemba chako, kavae viatu miguuni pako! Lakini usiufunike udevu wa midomoni, wala usile chakula, watu watakachokuletea!

18Asubuhi nilikuwa nikisema na watu, tena jioni mke wangu akafa, kesho yake asubuhi nikafanya nilivyoagizwa.

19Watu wakaniuliza: Mbona hutuelezi yatakayokuwa kwetu, wewe ukifanya hivyo?

20Nikawaambia: Neno la Bwana limenijia la kwamba:

21Uambie mlango wa Isiraeli: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikipapatia uchafu Patakatifu pangu palipo majivuno yenu makuu na tamaa ya macho yenu na upendeleo wa roho zenu. Nao wana wenu wa kiume na wa kike, mliowaacha, wataangushwa kwa panga.

22Ndipo, mtakapofanya, mimi nilivyofanya: Hamtazifunika ndevu za midomoni, wala hamtakula chakula, mtakacholetewa na watu.

23Navyo vilemba vyenu vitakuwa vichwani penu, navyo viatu miguuni penu; hamtaomboleza, wala hamtalia machozi, ila kwa manza zetu, mlizozikora, mtayeyuka, tena mtapigiana kite kila mtu na ndugu yake.

24Naye Ezekieli atawawia kielekezo, nanyi myafanye yote, aliyoyafanya yeye, yatakapotimia. Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu.[#Ez. 12:11; 24:27.]

25Nawe mwana wa mtu, isiwe hivyo? Siku, nitakapoyachukua kwao yaliyowapa nguvu, yaliyokuwa furaha yao kwa kuwapa utukufu, macho yaliyoyatamani, yaliyowashika mioyo yao wana wao wa kiume na wa kike,

26siku ile atakuja kwako mtu aliyekimbia, ayasimulie masikioni pako.[#Ez. 33:21.]

27Siku ile kinywa chako kitafumbuliwa papo hapo, yule mtoro atakapofika kwako, useme, usinyamaze tena; ndipo, utakapowawia kielekezo, nao watajua, ya kuwa mimi ni Bwana.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania