The chat will start when you send the first message.
1Ikawa katika mwaka wa 12 siku ya kwanza ya mwezi wa kumi na mbili, ndipo, neno la Bwana liliponijia la kwamba:
2Mwana wa mtu, mtungie Farao, mfalme wa Misri, ombolezo la kwamba: Ulifananishwa na mwana wa simba alioko kwenye mataifa, nawe ulikuwa kama mamba aliomo kwenye maji mengi, mara kwa mara ulitokea kwa nguvu katika mito yako, ukachafua maji kwa miguu yako na kuivurugavuruga mito yao.[#Ez. 27:2; 29:3.]
3Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitautanda wavu wangu juu yako kwenye mkutano wa makabila mengi ya watu, nao watakupandisha pakavu kwa jarife langu.[#Ez. 17:20.]
4Kisha nitakuacha hapo penye nchi kavu nikikutupa porini; kisha nitaleta ndege wa angani wote, wakukalie, nao nyama wote wa nchi hiyo nitawashibisha kwako.
5Hata milimani juu nitazipeleka nyama za mwili wako, nayo mabonde nitayajaza uvundo wa kwako.
6Nchi nitainywesha mafuriko yako yatokayo kwa damu yako, yafike hata milimani, nayo makorongo yatajazwa hayo yatokayo kwako.
7Hapo, nitakapokuzima, nitaifunika mbingu, nazo nyota zake nitazitia giza, hata jua nitalifunika kwa wingu, hata mwezi hautaangaza mwanga wake.[#Yes. 13:10.]
8Mianga yote iangazayo mbinguni nitaitia giza kwa ajili yako, hata nchi yako nitaieneza giza; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
9Kisha nitasikitisha mioyo ya watu wa makabila mengi, nitakapopeleka habari za kuvunjwa kwako kwa mataifa katika nchi, usizozijua wewe.
10Hivyo nitastusha makabila mengi kwa ajili yako, nao wafalme wao watapigwa na bumbuazi kwa ajili yako, nitakapouchezesha upanga wangu mbele yao; ndivyo, watakavyoingiwa na woga mara kwa mara, Kila mtu kwa ajili ya roho yake, siku ile, utakapoangushwa.
11Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Upanga wa mfalme wa Babeli utakujia.
12Kwa panga za wapiga vita wenye nguvu nitawaua watu wako, ingawa wawe wengi, kwani wale wote ndio wakali kuliko mataifa mengine; watayapoteza majivuno ya Wamisri, watu wao walio wengi watakapoangamizwa.
13Nao nyama wao wote nitawatowesha kwenye yale maji mengi, mguu wa mtu usiyachafue tena, wala nyama asiyachafue kwa kuyavurugavuruga.
14Ndipo, nitakapoyachuja maji yao, nayo majito yao nitayaendesha kama mafuta yanavyokwenda; ndivyo, asemavyo Bwana.
15Nitakapoigeuza nchi ya Misri kuwa pori tu, nchi itakapokuwa peke yake tu, yote yaliyoko yakitoweka, nitakapowapiga wote wakaao huko, ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
16Hili ndilo ombolezo la kuimba kwa kuomboleza; wanawali wa mataifa waliimbe kwa kuiombolezea nchi ya Misri, nao watu wake wengi watawaombolezea hivyo; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
17Ikawa katika mwaka wa 12 siku ya kumi na tano ya mwezi, ndipo, neno la Bwana liliponijia la kwamba:
18Mwana wa mtu, walilie hao watu wengi wa Misri, uwashushe pamoja na wanawali wa mataifa wenye utukufu kuwafikisha mahali palipo chini ya nchi kwao washukao shimoni.[#Ez. 31:16.]
19Unampita nani kwa uzuri? Shuka tu, ulazwe kwao wasiotahiriwa![#Yes. 14:11-19.]
20Wataanguka katikati yao waliouawa kwa panga; panga za kuwaua zimekwisha tolewa; ivuteni hiyo nchi pamoja na watu wake wote walio wengi![#Ez. 21:9.]
21Ndipo, wapiga vita wenye nguvu walioko kuzimuni watakapomwambia yeye nao waliomsaidia: Wameshuka kulala hawa wasiotahiriwa waliouawa kwa panga.[#Yes. 14:9.]
22Wako Waasuri na makundi yao yote ya watu, makaburi yao yanapazunguka pale po pote, wote wamekufa kwa kuumia wakiangushwa kwa panga.
23Wamepata makaburi yao kuzimuni pembeni, nayo makundi yao ya watu yanayazunguka makaburi yao wenyewe; hao wote wamekufa kwa kuumia wakiangushwa kwa panga; nao ndio waliostusha watu wakubwa katika nchi yao walio hai.[#Yes. 14:15.]
24Wako Waelamu nao watu wao wengi; wanalizunguka kaburi lake; hao wote wamekufa kwa kuumia wakiangushwa kwa panga, wameshuka pasipo kutahiriwa mahali palipo chini ya nchi; nao ndio waliostusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai, sasa wanashikwa na soni kwao walioshuka shimoni.
25Katikati yao waliouawa kwa panga wamewapa pa kulala penye watu wao wengi, nayo makaburi yao hawa yanawazunguka wenyewe. Wote ni watu wasiotahiriwa waliouawa kwa panga, kwani walistusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai, lakini sasa wanashikwa na soni kwao walioshuka shimoni, katikati yao waliouawa kwa panga wamepata mahali pao.
26Wako Wameseki na Watubali nao watu wao wengi, makaburi yao hawa yanawazunguka wenyewe; hawa wote ni watu wasiotahiriwa, walikufa wakiumia kwa panga; kwani walistusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai.[#Ez. 38:2.]
27Hawatalala pamoja na wapiga vita walioanguka kwao wasiotahiriwa, walioshuka kuzimuni pamoja na vyombo vyao vya vita wakiziweka panga zao chini ya vichwa vyao, lakini maovu, waliyoyafanya, yanaifunika mifupa yao, kwani hao wapiga vita walistusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai.
28Hivyo wewe nawe utavunjwa katikati yao wasiotahiriwa, ulale nao waliokufa wakiumia kwa panga.
29Wako Waedomu, wafalme wao na wakuu wao, waliokuwa wenye nguvu za kupiga vita, lakini nao wamepewa mahali pao kwao waliokufa wakiumia kwa panga, walale nao kwao wasiotahiriwa walioshuka shimoni.[#Ez. 25:12-14.]
30Wako wakuu wa kaskazini wote pamoja na Wasidoni wote walioshuka kwao waliokufa wakiumia kwa panga; walikuwa wakistusha watu kwa nguvu zao za kupiga vita, lakini soni za kushindwa zikawapata nao, sasa wanalala pasipo kutahiriwa kwao waliokufa wakiumia kwa panga wakishikwa na soni kwao walioshuka shimoni.[#Ez. 28:21-23; 38:6.]
31Farao atakapowaona hao atajituliza kwa ajili ya watu wake waliokuwa wengi. Farao na vikosi vyake vyote watakufa wakiumia kwa panga; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.[#Yes. 14:10.]
32Kwani nalimpa kustusha watu, alipokuwa katika nchi yao walio hai, lakini naye atalazwa katikati yao wasiotahiriwa pamoja nao waliokufa wakiumia kwa panga, yeye Farao nao watu wake walio wengi. Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.