The chat will start when you send the first message.
1Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2Mwana wa mtu, wafumbulie wachungaji wa Isiraeli yatakayowapata! Wafumbulie wachungaji ukiwaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Yatawapata, ninyi wachungaji wa Isiraeli mnaojichunga wenyewe! Tena sio kondoo wanaowapasa wachungaji, wawachunge?[#Ez. 13:2; Yer. 23:1-6.]
3Lakini ninyi hula maziwa yenye mafuta, huvaa nguo za manyoya yao, huchinja walionona, lakini kuchunga hamwachungi kondoo.
4Walio wanyonge humkuwatia nguvu, waliougua hamkuwaponya, waliovunjika hamkuwafunga vitambaa, waliokimbizwakimbizwa hamkuwarudisha, waliopotea kabisa hamkuwatafuta, ila mmewatawala kwa nguvu na kwa ukorofi.[#Zak. 11:16; 1 Petr. 5:3.]
5Hivyo wametawanyika, kwa kuwa hawana mchungaji, wakawa chakula cha nyama wote wa porini, wakatawanyika.[#Mat. 9:36.]
6kondoo wangu wakatangatanga milimani po pote napo po pote penye vilima vinavyokwenda juu; ikawa hivyo, kondoo wangu wakitawanyika katika nchi yote nzima, lakini hakuwako wala aliyewauliza, kama wako wapi, wala aliyewatafuta.
7Kwa hiyo, ninyi wachungaji lisikieni neno la Bwana!
8Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, kweli kondoo wangu wamepokonywa, kondoo wangu wakawa chakula cha nyama wote wa porini, kwa kuwa hawana mchungaji, kwa kuwa wachungaji wangu hawakuwatafuta kondoo wangu, wakajichunga wenyewe, wasiwachunge kondoo wangu.[#Ez. 34:2.]
9Kwa hiyo, ninyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana:
10Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikiwajia wachungaji, niwatafute kondoo wangu mikononi mwao, niwakomeshe, wasiwachunge kondoo wangu tena, wasiweze tena kujichunga wenyewe; nitawaokoa kondoo wangu vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao.
11Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikiwatafuta mwenyewe kondoo wangu, niwakague.
12Kama mchungaji anavyowakagua kondoo wake siku, anapokuwa katikati yao kondoo waliotawanyika, hivyo nami nitawakagua kondoo wangu, nitawaponya na kuwatoa mahali po pote, walipotawanyika siku ile iliyokuwa yenye mawingu meusi.[#Luk. 15:4.]
13Nitawatoa kwenye makabila ya watu na kuwakusanya katika hizo nchi, niwapeleke katika hiyo nchi yao; ndiko, nitakakowachunga Waisiraeli milimani kwao namo mabondeni napo pote, watu wanapokaa katika hiyo nchi.
14Nitawachunga penye malisho mema, tena mazizi yao yatakuwa juu ya milima mirefu ya Waisiraeli; huko watalala katika mazizi mema, wakilisha malisho ya kuwanonesha katika milima ya Isiraeli.[#Sh. 23:2.]
15Mimi mwenyewe nitawachunga kondoo wangu, nami nitawalalisha; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
16Waliopotea nitawatafuta, nao waliokimbizwakimbizwa nitawarudisha, nao waliovunjika nitawafunga vitambaa, nao waliougua nitawatia nguvu; lakini wenye mafuta na wenye nguvu nitawaangamiza, niwachunge na kuwapatiliza.
17Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Ninyi mliomo kundini mwangu mtaniona, nikiwaamua kondoo na kondoo, madume ya kondoo na ya mbuzi.[#Mat. 25:32.]
18Je? Haiwatoshi kulisha malisho mazuri, mkiyakanyagakanyaga kwa miguu yenu yaliyosalia malishoni penu? Mkinywa maji yaliyo safi nayo yaliyosalia mnayavurugiaje kwa miguu yenu?
19Kisha kondoo wangu wayalishe yaliyokanyagwakanyagwa na miguu yenu, tena wayanywe, mliyoyavuruga?
20Kwa hiyo Bwana Mungu aliye Mungu wenu anasema hivi: Mtaniona, nikiwaamua mwenyewe wale kondoo walionona nao hao kondoo waliokonda.
21Kwa kuwa mmewasukuma kwa mbavu na kwa mabega, mkawapiga kwa pembe zenu wote waliougua, mpaka mkiwatawanya huko nje;
22kwa hiyo mimi nitawaokoa kondoo wangu, wasipokonywe tena, nitakapoamua kondoo na kondoo.
23Ndipo, nitakapowainulia mchungaji mmoja, awachunge, ni mtumishi wangu Dawidi; yeye atawachunga, yeye atakuwa mchungaji wao.[#Ez. 37:24; Yoh. 10:12-16; Yer. 30:9; Hos. 3:5.]
24Nami Bwana nitakuwa Mungu wao, naye mtumishi wangu Dawidi atakuwa mkuu katikati yao; mimi Bwana nimeyasema.
25Ndipo, nitakapofanya nao agano la kuwapa utengemano, nitatowesha nyama wabaya wote katika hiyo nchi, wapate kukaa na kutulia hata nyikani, walale usingizi hata msituni.[#Ez. 37:26.]
26Nitawapatia mbaraka wao wenyewe nazo nchi zangu zenye vilima ziwazungukazo, nikizinywesha mvua, siku zake zitakapotimia; nazo hizo mvua zitakuwa mvua zenye mbaraka.
27Miti ya shambani itazaa matunda yao, nayo nchi itawapa mazao yake, watakaa katika nchi yao; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapoivunja miti ya makongwa yao na kuwaopoa mikononi mwao waliowatumikisha.
28Hawatatekwa tena na mataifa, wala hawataliwa na nyama wa nchi hiyo, watakaa salama, hatakuwako atakayewastusha.
29Nitaotesha kwao mashamba yatakayosifiwa kuwa mashamba, wasipatwe na njaa tena katika hiyo nchi, hawatatukanwa tena na wamizimu.[#Ez. 36:30.]
30Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu wao, niko pamoja nao, nao watakuwa ukoo wangu; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.[#Ez. 11:20.]
31Kwani ninyi m ukoo wangu, m kondoo wangu, ninaowachunga; ninyi m watu, nami ni Mungu wenu; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.[#Sh. 100:3.]