The chat will start when you send the first message.
1Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2Mwana wa mtu, ielekezee milima ya Seiri uso wako na kuifumbulia yatakayokuwa![#Ez. 25:8,12.]
3Iambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Utaniona, nikikujia, mlima wa Seiri; nitakukunjulia mkono wangu, nikugeuze kuwa mapori yaliyo peke yao!
4Miji yako nitaivunja, iwe mabomoko tu, nawe utakuwa mapori tu; ndipo, utakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
5Kwa kuwa umeshika uchukivu wa kale na kale, ukawabwaga wana wa Isiraeli kwenye panga siku zile, waliposhindwa, ni siku zile, walipolipishwa manza zao, walizozikora.
6Kwa hiyo Bwana Mungu anasema: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, nitaimwaga damu yako, nazo damu zitakukimbiza; kwa kuwa hukuchukiwa na kumwaga damu, damu zitakukimbiza.[#Ufu. 16:5-6.]
7Nitaigeuza milima ya Seiri kuwa mapori yaliyo peke yao, nikitowesha kwao wapitaji wanaokwenda na kurudi.
8Milima yao nitaijaza mizoga yao waliouawa, katika vilima vyako na katika mabonde yako na katika makorongo lyako yote wataanguka waliouawa na panga.
9Nitakugeuza kuwa mapori ya kale na kale, miji yako isikae watu tena; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
10Kwa kuwa ulisema: Hayo mataifa mawili nazo nchi zao mbili zitakuwa zangu, tuzichukue! naye Bwama alikuwa yupo;
11kwa hiyo Bwana anasema: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, nitakufanyizia yayo hayo, uliyoyataka kuyafanya kwa makali yako na kwa wivu wako, uliyoyatenda kwa hivyo ulivyowachukia; ndipo, nitakapojulikana kwao, nitakapokuwa nimekwisha kukuhukumu.
12Ndipo, utakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana. Nimeyasikia maapizo yako yote, uliyoyasema na kuiapiza milima ya Isiraeli kwamba: Na iwe mapori, tupewe sisi kuila!
13Ndivyo, mlivyovikuza vinywa vyenu mbele yangu, nayo maneno yenu, mliyoyasema mbele yangu, yakawa ya majivuno tu; mimi nimeyasikia.
14Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nchi yote nzima itafurahi, nitakapokugeuza kuwa mapori tu.
15Kama wewe ulivyofurahi, fungu lao walio mlango wa Isiraeli lilipogeuzwa kuwa mapori, hivyo ndivyo, nitakavyokufanyzia: utakuwa mapori tu, mlima wa Seiri, pamoja na nchi yote nzima ya Edomu; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.[#Ez. 25:3; Sh. 137:7.]