The chat will start when you send the first message.
1Mkono wa Bwana ukanishika, Bwana akanitoa kirohoroho, akanipeleka na kuniweka katikati ya hilo bonde, nalo lilikuwa limejaa mifupa.
2Akanipitisha po pote pande zote, ilipokuwa, nikaiona kuwa mingi sana humo bondeni juu ya mchanga, nami nikaiona kuwa mikavu sana.
3Akaniuliza: Mwana wa mtu, inakuwaje? Mifupa hii itaweza kuwa yenye uzima tena? Nikajibu: Bwana Mungu wewe unajua.
4Akaniambia: Ifumbulie mifupa hii yatakayokuwa! Iambie: Ninyi mifupa mikavu, sikieni neno la Bwana!
5Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyoiambia mifupa hii: Tazameni, nitawaletea pumzi ndani yenu, mpate kuwa wenye uzima tena.[#Sh. 104:30.]
6Nitatia mishipa juu yenu, tena nitaotesha nyama juu yenu, nitawafunika kwa ngozi, kisha nitawatia pumzi; ndipo, mtakapokuwa watu wazima, mtajua, ya kuwa mimi ni Bwana.[#Yes. 26:19.]
7Nikafumbua, kama nilivyoagizwa; ikawa, sauti ya kufumbua kwangu iliposikilika, pakawa na vishindoshindo, mifupa ikarudiana kila mfupa kwa mfupa mwenziwe.[#Ez. 37:10.]
8Nilipotazama, nikaona kwao mishipa, nazo nyama zikaja kuwa juu yao, kisha ngozi zikazifunika pande za juu, lakini pumzi hazikuwamo mwao.
9Akaniambia: Ufumbulie upepo! Fumbua, mwana wa mtu, ukiuambia upepo: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Wewe upepo njoo na kutoka pande zote nne za upepo, uwapuzie hawa waliouawa, wapate kuwa wazima tena!
10Nikafumbua, kama nilivyoagizwa; ndipo, pumzi zilipowaingia, wakawa wazima, wakasimama kwa miguu yao, wakawa kikosi kikubwa sanasana.
11Akaniambia: Mwana wa mtu, mifupa hii ndiyo mlango wote wa Isiraeli. Tazama, husema: Mifupa yetu imekauka, kingojeo chetu kimepotea, tumekatwa roho.
12Kwa hiyo wafumbulie ukiwaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikiyafunua makaburi yenu, niwatoe mle makaburini mwenu ninyi mlio ukoo wangu! Kisha nitawapeleka katika nchi ya Isiraeli.
13Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa mle makaburini mwenu ninyi mlio ukoo wangu.
14Nitawatia Roho yangu, mpate kuwa wazima tena, kisha nitawapeleka katika nchi yenu, mtulie huko; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, niliyoyasema ninayafanya; ndivyo, asemavyo Bwana.
15Neno la Bwana likanijia la kwamba:
16Mwana wa mtu, jipatie kijiti kimoja, ukiandike: Cha Yuda na cha wana wa Isiraeli walio wenziwe! Kisha jipatie kijiti kingine, ukiandike: Cha Yosefu! maana ni kijiti cha Efuraimu na cha mlango wa Isiraeli walio wenziwe![#Ez. 4:1.]
17Kisha vibandike kimoja kwa mwenziwe, vishikamane kuwa kwako kijiti kimoja tu, hivyo viwili viwe kimoja kabisa mkononi mwako!
18Kama wana wao walio ukoo wako watakuuliza kwamba: Hutuambii maana yao hayo, uliyo nayo?
19waambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona mimi, nikikichukua kijiti cha Yosefu kilichomo mkononi mwa Efuraimu nayo makabila ya Waisiraeli walio wenziwe, niwatie pamoja na kijiti cha Yuda, niwafanye kuwa kijiti kimoja tu; ndipo, watakapokuwa kimoja mkononi mwangu.
20Navyo vijiti, ulivyoviandika, sharti viwe mkononi mwako machoni pao.
21Kisha uwaambie: Hivi ndivyo Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikiwachukua wana wa Isiraeli kwenye wamizimu, walikopelekwa, niwakusanye na kuwatoa pande zote; kisha nitawapeleka katika nchi yao.[#Ez. 36:24.]
22Huko nitawafanya kuwa kabila moja katika nchi hiyo kwenye milima ya Isiraeli. Naye mfalme wao wote atakuwa mmoja tu, hawatakuwa tena makabila mawili, wala hawatagawanyika tena kuwa nchi mbili zenye wafalme.[#Yes. 11:12-13; Yer. 3:18; Hos. 1:11.]
23Wala hawatajipatia uchafu tena kwa kuyatambikia yale magogo yao wala kwa kuyafanya machukizo yao na mapotovu yao yote; nami nitawaokoa na kuwatoa mahali pao pote palipowakosesha, niwatakase; ndipo, watakapokuwa ukoo wangu, nami nitakuwa Mungu wao.[#Ez. 36:28.]
24Naye mtumishi wangu Dawidi atakuwa mfalme wao, yeye peke yake atakuwa mchungaji wao wote; ndipo, watakapoyafuata mashauri yangu na kuyashika maongozi yangu, wayafanye.[#Ez. 34:23; 36:27.]
25Hivyo watakaa katika nchi hiyo, niliyompa mtumishi wangu Yakobo, waliyoikaa baba zenu; ndiko, watakakokaa wao na wana wao na wajukuu wao kale na kale, naye mtumishi wangu Dawidi atakuwa mfalme wao kale na kale.
26Nitafanya nao agano la kuwapa utengemano, nalo litakuwa la kale na kale kwao; nami nitawapa kukaa na kuwa wengi, hata Patakatifu pangu nitapaweka, pawe katikati yao kale na kale.[#Ez. 34:25; Yes. 54:10.]
27Hapo patakuwa Kao langu la kwao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa ukoo wangu.
28Ndipo, wamizimu watakapojua, ya kuwa mimi Bwana ndiye anayewatakasa Waisiraeli, Patakatifu pangu patakapokuwa katikati yao kale na kale.[#Ez. 36:36.]