The chat will start when you send the first message.
1Akanirudisha kwenda kwa jengo la lango la nje la Patakatifu lielekealo maawioni kwa jua, nalo lilikuwa limefungwa.
2Bwana akaniambia: Lango hili sharti likae limefungwa, lisifunguliwe, wala asiingie mtu humo, kwa kuwa Bwana Mungu wa Isiraeli aliingia humo; kwa hiyo liwe limefungwa.
3Naye atakayekuwa mkuu, yeye mkuu peke yake atakaa humu, ale chakula mbele ya Bwana, ataingia kwa njia ya ukumbi wa hilo jengo la lango, kisha atatoka kwa njia ileile.[#Ez. 45:7.]
4Kisha akanipeleka kwenda kwa jengo la lango la kaskazini la hiyo Nyumba. Nilipotazama nikaona, utukufu wake Bwana, ulivyoijaza Nyumba, nikaanguka kifudifudi.[#Ez. 43:5.]
5Bwana akaniambia: Mwana wa mtu, yaweke moyoni mwako utakayoyaona kwa macho yako nayo utakayoyasikia kwa masikio yako, yote nikayoyasema na wewe kwa ajili ya maongozi yote yaipasayo Nyumba ya Bwana na kwa ajili ya maonyo yake uyaweke moyoni mwako, ujue, mtakapoiingia Nyumba hii, napo pote, mtakapopatoka hapa Patakatifu.
6Nao walio mlango wa Isiraeli ulio mkatavu waambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Ninyi mlio mlango wa Isiraeli, yaacheni machukizo yenu yote, mliyoyafanya! Kwani ni mengi.
7Mwalileta wageni wasiotahiriwa wala mioyo wala miili, wapaingie Patakatifu pangu, waipatie Nyumba yangu uchafu, mliponiletea chakula changu cha tambiko, cha mafuta na cha damu; hivyo ndivyo, mlivyolivunja Agano langu kwa kuyafanya hayo machukizo yenu yote.
8Wenyewe hamkutumika na kuushika utumishi wa vitakatifu vyangu, mkawaweka wao kuwa mahali penu watumishi wa kutumikia Patakatifu pangu.
9Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mgeni yeyote asiyetahiriwa wala moyo wala mwili asipaingie tena Patakatifu pangu, ijapo awe mmoja wao wale wageni wote wakaao kwa wana wa Isiraeli katikati.
10Ila Walawi walioniacha na kujiendea mbali hapo, Waisiraeli walipopotea, watatwikwa manza zao, walizozikora, ndio wale waliopotea kwa kuniacha wakiyafuata magogo yao ya kutambikia.
11Hao watapatumikia Patakatifu pangu na kuyangoja malango ya Nyumba hii na kuwa watumishi wa humu Nyumbani; ndio watakaozichinja ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima nazo zile nyingine, watu watakazozitoa za tambiko; hapo ndipo, watakaposimama mbele yao, wawatumikie.
12Kwa kuwa waliwatumikia watu mbele ya magogo yao ya kutambikia, wakawakosesha hivyo walio mlango wa Isiraeli, wakore manza, kwa sababu hii nimewaapia kwa kuuinua mkono wangu kwamba: Watatwikwa manza zao, walizozikora; ndivyo, asemavyo Bwana.
13Lakini wasinikaribie na kufanya kazi za utambikaji, wala wasivikaribie vitakatifu vyangu vyenyewe; hivyo watashikwa na soni kwa kutwikwa machukizo yao, waliyoyafanya.
14Kwa hiyo nitawaweka kuwa watumishi wa kutumikia humu Nyumbani, waufanye utumishi wake wote na kazi zote zitakazofanyizwa humu.
15Lakini watambikaji wa Kilawi walio wana wa Sadoki, walioushika utumishi wa Patakatifu pangu, wana wa Isiraeli walipopotea na kuniacha, hao ndio watakaonikaribia, wanitumikie na kusimama mbele yangu, wakiniletea mafuta na damu; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.[#Ez. 40:46; 48:11.]
16Hao watapaingia Patakatifu pangu, waikaribie meza yangu wakinitumikia kwa kuushika utumishi wangu.
17Nao watakapoingia malangoni mwa ua wa ndani sharti wavae mavazi ya pamba, wasiwe na nguo zo zote za manyoya ya kondoo wakifanya kazi za utambikaji mle malangoni mwa ua wa ndani namo humu Nyumbani![#3 Mose 16:4.]
18Vichwani sharti wavae vilemba vya nguo za pamba, hata viunoni sharti wavae suruali za pamba, wasijifunge nguo zitoazo jasho.
19Lakini watakapotoka kwenda katika ua wa nje, ni ule ua wa nje, watu walipo, sharti wayavue mavazi yao, waliyoyavaa wakifanya kazi za utumishi, wayaweke katika vile vyumba vya Patakatifu, kisha wavae mavazi mengine, wasiwapatie watu utakatifu kwa hayo mavazi yao.[#Ez. 42:14.]
20Vichwa vyao wasivinyoe kabisa, wala wasiache mavunga, yakue kabisa, ila nywele zao za vichwani wazikatekate.[#3 Mose 19:27; 21:5.]
21Tena wote walio watambikaji wasinywe mvinyo watakapouingia ua wa ndani.[#3 Mose 10:9.]
22Wala wasichukue mjane wala mwanamke aliyeachwa kuwa wake zao, ila waoe wanawali walio wa uzao wa mlango wa Isiraeli au mjane aliye mjane wa mtambikaji.[#3 Mose 21:7,13-14.]
23Wawafundishe watu wangu kupambanua kilicho kitakatifu nacho kinachotumika kwa watu siku zote, tena wawajulishe kupambanua yaliyo machafu nayo yaliyotakata.[#3 Mose 10:10.]
24Tena watu wakigombana, hao ndio wanaopaswa na kuwasimamia na kuwaamua, nao wawaamue kwa mashauri yangu. Sharti wayashike Maonyo yangu na maongozi yangu kwenye mikutano yote ya sikukuu zangu, nazo siku zangu za mapumziko sharti wazitakase!
25Mtu aliyekufa wasimkaribie, wasijipatie uchafu! Wajipatie uchafu tu kwa baba na mama na mwana wa kiume na wa kike na kwa ndugu na kwa umbu asiyeolewa bado.[#3 Mose 21:1-4.]
26Atakapokwisha kueuliwa, wamhesabie tena siku saba!
27Kisha siku, atakapopaingia Patakatifu, auingie ua wa ndani kufanya kazi ya utumishi hapo Patakatifu, kwanza apeleke ng'ombe ya tambiko ya weuo; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
28Tena fungu litakalowapasa kuwa lao, basi, mimi nitakuwa fungu lao, kwa hiyo msiwape mali zo zote kwao Waisiraeli za kuzishika kuwa zao! Mimi ni mali zao za kuzishika kuwa zao.[#4 Mose 18:20.]
29Vipaji vya tambiko nazo ng'ombe za tambiko za weuo na za upozi wao watazila, navyo vyo vyote vitakavyokuwa mwiko kwao Waisiraeli kuvila vitakuwa mali zao.
30Nayo malimbuko yote pia yanayotolewa kwa kuwa ya kwanza, navyo vipaji vyenu vyote vingine, mtakavyovitoa, vitakuwa mali zao watambikaji nao unga wenu wa kwanza wa kupika mikate mtawapa watambikaji, mbaraka izikalie nyumba zenu.
31Lakini kila nyama aliyekufa kibudu au aliyeraruliwa na nyama mwingine, watambikaji wasile, kama ni ya ndege au ya nyama.[#3 Mose 22:8.]